SABODO sasa ashauri fedha zibadilishwe, ampongeza Rais asema hakuna haja ya upinzani

Mimi kwa mtizamo wangu serikali ndio kisababishi cha fedha kutokuzunguka. Walipoamua kuweka pesa zake bank kuu badala ya bank za biashara ndio wameziba kila kitu.
 
5e347fc6d95c91d622171887cfb5be19.jpg

Wakati wananchi wakilia ukata mifukoni kwa madai fedha zimetoweka kwenye mzunguko, mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, huoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalum nyumbani kwake Dar es salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi

"Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi waliofikwa fedha nyumbani, watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha

Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na 10,000 hatua hiyo itasaidia kubadili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania mpya," alisema Sabodo

Aliongeza:"Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na nusu, watabainika wengi waliofikwa fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika".

Alifanunua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama ilivyo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao

"Watu wanaiba fedha nyingi, wanaficha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi". alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka waliofikwa fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahala pa kuzipeleka

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogapa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Chanzo: JamboLeo
Unaposema hakuna haja ya upinzani kwa upande wa pili wa sarafu moja hiyo hiyo ni kwamba vyama vyote vifutwe. Maadamu CCM pia ni chama kama vilivyo vyama vingine, afute vyama vyote abaki yeye na watendaji wake binafsi wasiojinasibu kwa chama chochote.

Unaposema kufuta upinzani na wakati huo wewe pia ni zao la chama, unatakiwa kupimwa akili. Who is Sabodo by the way?!!! Kuwa na hela ndio kuhalalishe mambo mengine haramu kwa nchi inayojinasibu kwa katiba ya mfumo wa vyama vingi? Mmjaze kiburi na ushuzi wa kutosha acute. Futa basi mamlaka unayo bwana mkubwa. Kumbuka kufuta na katiba na sheria mbalimbali zinazotambua Tanzania as a multiparty stPerioderiod
 
Ukiangalia kwa undani utadhani anasifia kumbe demokrasia ya awamu ya tano inachekwa hivi tukisema hakuna haja ya upinzani wakati nchi inaendeshwa kwa sheria ya vyama vingi ni udikteta huo kwaherini.
 
Halafu kuna watu wanajitahidi kupotosha tuu ukweli nchi haiwezi kujiendesha bila misaada sasa walikataa misaada kwa jeuri jumlisha wanatakiwa kupeleka bejeti shuleni, tofauti na awamu zilizopita hazikuhitaji hilo mbaya zaidi baadhi ya wahisani wamejitoa lazima magepu ya bajeti na ufinyu wa malipo uonekane mitaani.
 
Kwani ndani ya huo muda utakaotolewa, wenyewe hawawezi kuzibadili (kama wapo kweli walioficha madafu ndani)?
 
Anatafuta kiki asikike. Hachelewi kununua kurasa magazetini kuandika pongezi halafu anajipambanua na Unyerere.
 
Sabodo alitoa hela ya kujenga ofisi za chama fulani lakini mwenyekiti akajinunulia mafuso yake
 
Na walioficha fedha pale BOT nao washughulikiwe ili kudhibiti uhaba wa pesa kwenye mabank ya biashara
 
5e347fc6d95c91d622171887cfb5be19.jpg

Wakati wananchi wakilia ukata mifukoni kwa madai fedha zimetoweka kwenye mzunguko, mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, huoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalum nyumbani kwake Dar es salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi

"Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi waliofikwa fedha nyumbani, watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha

Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na 10,000 hatua hiyo itasaidia kubadili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania mpya," alisema Sabodo

Aliongeza:"Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na nusu, watabainika wengi waliofikwa fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika".

Alifanunua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama ilivyo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao

"Watu wanaiba fedha nyingi, wanaficha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi". alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka waliofikwa fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahala pa kuzipeleka

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogapa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Chanzo: JamboLeo
Hili ponjolo lilrudi India si limeshachuma. Hayo ni opportunistic tu. Yana passport kama kumi including Tanzania, India Canada UK.
 
Sasa hao walio ficha wakibadili Fedha zao kwenda Dollar, Utawakamatia wap Basi kuna haja ya Kubadilisha na dollar pia.. Ila kama Dollar ni hela Ya Tanzania hahaha Akili za kuamka.
Kama ni fedha haramu jeuri ya kwenda badilisha hutakuwa nayo maana state ikishatangaza ivyo itafanya monitoring mwenye mzigo mkubwa nani na kautoa wapi?
 
•je ni kweli fedha nyingi zimefichwa?.......
•je walioficha fedha ni wapuuzi kiasi cha kutokuzibadili kuwa Dollars?,Riale na pounds sterlings?
[HASHTAG]#AKILI[/HASHTAG] ZINGINE BANA....
Nakwambia hivi huko ni kumcheza shere president watu Wameshamaliza zamani kubadili pesa zao ndio kisa wametuma msemaji wao apime ikiwa Jamaa bado ana mawazo hayo au lah! hao watu they are very clever sio wa mchezo mchezo fuatilia history zao utaona sio wa vipindi vya miaka mitano mitano kabla uhuru mpaka kesho wapo tu wanacheza na saikolojia ya watu! Wala mkuu hasipokee kila ushauri kama dodoki ahoji kwa nini leo na siyo jana
 
Sasa kama iko kwenye mzunguko iliyofichwa ni ipi?
Iliofichwa ni elfu5 na elfu10, hata kama ukibadilisha kuwa dollar bado itarudi tu kwenye mzunguko, Rais kaficha fedha na wafanyabiashara wakubwa wameficha ela kwaiyo ngoma droo, tunaumia Wa hali ya kawaida ambao ndio tupo wengi.....
 
Back
Top Bottom