Sabaya tulia Mungu atatenda muujiza maana huwezi kupambana na ufisadi chini ya mfumo wa kifisadi

Sindano zenyewe ni butu na lizima ziwangie hata kwa kupaka oil chafu

Kweli kutesa ni kwa zamu. Raha tuliyo nayo sasa, pana watu wa awamu ile walikuwa nayo kipindi kile?!

Pia kuwa maumivu tuliyokuwa nayo kule sasa hivi yamewafika na wao akiwamo kinara Ole Lengai Sabaya?!

Ninakazia, "kweli kutesa ni kwa zamu!"
 
LENGAI OLE SABAYA, HUWEZI KUPAMBANA NA UFISADI NDANI YA MFUMO WA KIFISADI, UKABAKIA SALAMA:

Mfumo wa ufisadi, ulaji rushwa, uhujumu uchumi, ufanyaji magendo, na matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa umma ulianza kujikita mizizi serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi kuanzia miaka ya 1980 mara baada ya kumalizika kwa vita ya Kagera.

Ni kuanzia muda huo wafanya biashara wakubwa wanaofanya magendo walianza kufunga ndoa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake. Moja ya mambo yaliyofanywa na mfumo huu kwa kipindi hicho ni kuficha bidhaa na kusababisha uhaba wa bidhaa muhimu kwa matumizi ya binadamu ikiwemo sukari, mafuta ya kupikia, mafuta ya taa, sabuni, dawa za kupigia mswaki, na kibaya zaidi kundi hili lilificha hadi fedha majumbani bila kuzipeleka Benki, hatua iliyoilazimu serikali kuchapisha noti na sarafu mpya na kutangaza muda wa siku chache kwa watu wenye fedha za zamani majumbani kufika benki kuzibadilisha huku ikiweka kiwango maalum cha mwisho kwa mtu kubadili.

Manufaa ya mfumo huu wa kifisadi baada ya kujijenga serikalini pamoja na kwenye Chama ilikuwa ni kunufaika na kila aina ya fursa wanayoitaka, iwe ya kuagiza bidhaa nje ya nchi, kukwepa kodi, uporaji rasilimali za nchi, au vinginevyo. Ni kupitia mfumo huu ndiyo uliokifadhiri Chama cha Mapinduzi kipindi cha uchaguzi kwa kuchapisha sare za Chama bure ikiwemo khanga, vitenge, kofia, fulana, bendera nk kwa madhumuni ya wao kusamehewa kodi bandarini.

Baba wa taifa Mel. Nyerere kabla ya kung'atuka madarakani aliliona hilo, hivyo ikabidi amwandaye mtu jasiri na shupavu wa kuja kupambana na mfumo huo, na huyo hakuwa mwingine isipokuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo hayati Mhe. Edward Moringe Sokoine kwa kumpeleka kwanza masomoni nchini Sweden ili kuja kuchukua nafasi yake.

Mwaka 1984 katika hotuba yake ya kuhitimisha kikao cha Bunge Dodoma, Mhe. Edward Sokoine aliapa kupambana na wahujumu uchumi wanaoficha bidhaa na fedha. Kwa bahati mbaya sana akiwa njiani kurejea Jijini Dar es Salaam, alipata ajali Morogoro iliyochukua uhai wake baada ya msafara wake kugongwa na gari la wapigania uhuru wa Chama cha ANC lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Dumisani Dube. Japokuwa haikuwekwa wazi lakini inasadikika ajali hiyo ilikuwa ya kupangwa.

Kuanzia hapo Mwl. Nyerere akawa hana namna, na hivyo kuiacha nchi mikononi mwa manyang'au wakianza na kuvunjwa kwa Azimio la Arusha lililokuwa na miiko kwa viongozi ikiwemo kutojilimbikizia mali. Ni kupitia mfumo huu mafisadi waliweza kufanya lolote wapendalo.

Kwa upande wa Chama, waligombea nafasi za uongozi wakitumia ushawishi wao wa fedha ikiwemo ubunge, na kwenye serikali, ni wao walioelekeza kiongozi gani apangwe wapi. Kwenye eneo hili la kupangwa safu za uongozi, kiongozi aliyeonekana mzalendo kwa nchi kukwamisha azima yao ya kuitafuna nchi, aliondolewa mara moja kwenye nafasi yake. Nguvu ya mafisadi ilipanga na kupangua hadi nafasi za viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama hususani kwenye nafasi za Wakuu wa Polisi, ikafikia hatua wahalifu wakafunga njia katika baadhi ya maeneo ya nchi kwa watu kutosafiri baada ya saa 4 usiku.

Alipoingia madarakani mwaka 2015 kati ya maeneo aliyofanikiwa Rais Magufuli kuyasafisha ni utumishi wa serikali. Huku alipaweza, lakini kwenye Chama ambako ndiko walikojificha manyang'au wakubwa, aliogopa
kupagusa. Alichofanikiwa ni kupunguza ukubwa wa Kamati kuu pamoja na Halmashauri kuu ili kuwa na nguvu ya kupitisha maamuzi yake kirahisi, na kubwa kuliko yote ni kuhakiki mali za chama smbapo inaelezwa kwamba, iwapo ripoti ya tume iliyoundwa kuhakiki mali za chama ikiongozwa na Djt. Bashiru Ally Kakurwa, kama ingewekwa wazi ingesababisha mpasuko mkubwa ndani ya Chama.

Kwa miaka yote hiyo hatamu za Chama ziliendelea kushikwa na mfumo huo hadi 2015 huku nafasi za uongozi zikiwa ni biashara inayolipa ikiwemo mali za Chama kama vile viwanja, majengo kuhodhiwa na mafisadi kwa ajili ya kutumia mali hizo kuendeshea biashara zao kama vile vituo vya mafuta.

Kwa wale tunaofahamu ni kwamba vita ya kiuchumi aliyoianzisha Rais Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi, uporaji rasilimali, matumizi mabaya ya madaraka alikuwa peke yake pamoja na viongozi wachache aina ya Lengai Olle Sabaya huku kukiwa na kundi kubwa la wananchi wanyonge tunaomuunga mkono.

Vita hiyo ilikuwa ni sawa na mgonjwa wa virusi vya ukimwi anayetumia ARV ambapo siku akiacha, virusi humshambulia kwa kasi hadi kupelekea kifo chake.
Chai chai chai
 
Wewe Sabaya tulia.

Usiendelee kuwatia hasira watanzania kwa propaganda zako za kishamba.

Huu ni wakati wa kulipa uovu uliowafanyia watanzania.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Back
Top Bottom