kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,293
- 12,593
Tuhuma zinazomkabili aliyekuwa DC wa Hai kama zitathibitishwa mbele ya sheria itakuwa ushahidi usiokuwa na mashaka juu ya wapi taifa hili lilikuwa liekezwe siku za usoni. Sabaya aliyatenda haya yote bila kuwa na hofu ya kuchukuliwa hatua, alikuwa anapongezwa na kuonekana shujaa na hodari katika Kazi yake.
Inavyoonekana kuna baadhi ya wateule ambao walifanyakazi zao kama vile walikuwa na fununu kuwa awamu ya tano itakuwa ya milele. Hawakuwa na hofu ya mamlaka wala ya Mungu.
Kama ni kweli tuhuma hizi zinamhusu inashangaza kuona alifikaje hapa bila kuhojiwa wala kutenguliwa. Je, aliyoyafanya yalikuwa maagizo maalumu kwa kanda na wilaya ile kwa wakati ule?
Je, kama Mh. JPM angekuweko madarakani Sabaya angefikishwa hapo alipo sasa?
Je, akina Sabaya walikuwa wako wangapi kwenye awamu ya tano? Wako wapi? Nani awatolee malalamiko nao wachunguzwe?