Sabaya ni ushahidi wa Taifa lilikokuwa linaelekea

#29October2020; nilimkosoa Sabaya kuhusu kutumia magari yenye namba "feki" za UN kuteka na kuumiza wananchi wa Hai.

#30October2020; Sabaya akanipigia simu mara 3 sikupokea. Akaniandikia sms ya matusi na kutishia kuniua.

#1November2020; Nikascreenshot ujumbe huo na kumtumia rafiki yangu aliyekua kiongozi serikalini, just in case lolote likinitokea.

#26December2020; tukiwa eneo moja Moshi mimi na Don Mbowe, baada ya kuondoka Sabaya alivamia eneo hilo na kudai aoneshwe tulipo. Alipoambiwa tumeondoka alikataa kukubali. Akapiga risasi hewani na kuvuruga biashara eneo hilo.

#28December2020; Akakutana na binamu yangu Moshi (wanafahamiana). Akamwambia mpigie Malisa mwambie aje hapa, lakini usimwambie tupo wote. Jamaa akakataa. Akampiga na kumlaza rumande. Akamnyang'anya simu na hajamrudishia hadi leo.

#13May2021; Mama Samia akamsimamisha kazi kwa tuhuma mbalimbali.

#04June2021; akapandishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Nimwambie nini Mungu?

Malisa GJView attachment 1808995

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka taifa lilishageuziwa kibla, hofu kwa kila MTU, wanaharakati wa kujitegemea walitukana kila mtu Na hapakua Na pa kushitaki, ulinzi kila sehemu, askari hawakuata sheria za barabarani wakageuka VIP eti kila wakati wako kwenye mission nyeti, siasa hakuna, chaguzi za waliokwenda kuunga juhudi zilikomba hela za watumishi wa umma, na wagombea wa upinzani wote ghafla wakageuka ngumbaro wasiojua kujaza fomu za kuomba kuteuliwa hivyo kustahili kuenguliwa wote. Wale waliosema atake asitake tutamuongezea muda nao hakuna aliyekaripiwa wala kupoteza kishikizo cha shati.
 
Tuhuma zinazomkabili aliyekuwa DC wa Hai kama zitathibitishwa mbele ya sheria itakuwa ushahidi usiokuwa na mashaka juu ya wapi taifa hili lilikuwa liekezwe siku za usoni. Sabaya aliyatenda haya yote bila kuwa na hofu ya kuchukuliwa hatua, alikuwa anapongezwa na kuonekana shujaa na hodari katika Kazi yake.

Inavyoonekana kuna baadhi ya wateule ambao walifanyakazi zao kama vile walikuwa na fununu kuwa awamu ya tano itakuwa ya milele. Hawakuwa na hofu ya mamlaka wala ya Mungu.

Kama ni kweli tuhuma hizi zinamhusu inashangaza kuona alifikaje hapa bila kuhojiwa wala kutenguliwa. Je, aliyoyafanya yalikuwa maagizo maalumu kwa kanda na wilaya ile kwa wakati ule?

Je, kama Mh. JPM angekuweko madarakani Sabaya angefikishwa hapo alipo sasa?

Je, akina Sabaya walikuwa wako wangapi kwenye awamu ya tano? Wako wapi? Nani awatolee malalamiko nao wachunguzwe?
Wamefurukuta wee mara Mkapa puu! Kijazi Puu! Jiwe Puu!! Sabaya puu! Mungu ameanza na wale Extremist kwanza.
 
Back
Top Bottom