Sabaya kaiaibisha Ikulu kwa kuihusisha na uhalifu alioshitakiwa nao

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
2,110
2,000
Hizi tuhuma ambazo zinatolewa na Sabaya kuwa mamlaka ya uteuzi ilihusika kumpa kazi maalumu kisha tuhuma za uhalifu zikatokea ni aibu kwa taifa letu.

Ikulu ambayo ndio mahala pa kuonyesha mamka ya wananchi kuwageuka wananchi na kumtuma Sabaya kufanya uhalifu ni aibu kubwa na fedheha kwa taifa letu.

Yaani wananchi wanapiga kura kisha kuteua mtu ambaye anapewa mamlaka ya kuwa rais ili aongoze taifa kwa niaba ya watanzania wote, alafu anatuma mtu au watu maalulu ili kwenda kutesa na kupora kwa kutumia siraha.

Hii ni aibu na fedheha kwa taifa letu.
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,679
2,000
Bado nataka kufahamu kwa nini kauli ya ANAUPIGA MWINGI inaanza kupotea, watu fulani humu mlikuwa mna kejeli sana wengine wanao onyesha kutomkubali boss wenu, kwani mko wapi?.
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,288
2,000
Dai katiba mpya acheni porojo

Siku ukijua kuwa alimuua kwa mkono wake ndani ya ikulu kisha mwili wake ukatupwa kwenye kisiwa cha chatu
Ndo utajua ikulu yetu ilinajisiwa
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
3,260
2,000
Halafu mataifa yote duniani yanafanya haya mambo, tofauti ni kuwa viongozi wao wana uzoefu na hivyo hawaruhusu mambo kama haya yawe wazi tofauti na sisi ambao tuna mkuu mweupe kichwani.
 
Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,726
2,000
Hizi tuhuma ambazo zinatolewa na Sabaya kuwa mamlaka ya uteuzi ilihusika kumpa kazi maalumu kisha tuhuma za uhalifu zikatokea ni aibu kwa taifa letu.

Ikulu ambayo ndio mahala pa kuonyesha mamka ya wananchi kuwageuka wananchi na kumtuma Sabaya kufanya uhalifu ni aibu kubwa na fedheha kwa taifa letu.

Yaani wananchi wanapiga kura kisha kuteua mtu ambaye anapewa mamlaka ya kuwa rais ili aongoze taifa kwa niaba ya watanzania wote, alafu anatuma mtu au watu maalulu ili kwenda kutesa na kupora kwa kutumia siraha.

Hii ni aibu na fedheha kwa taifa letu.
Sabaya hajaiaibisha ikulu, katoa picha khalisi ya namna katiba ya mwaka 1977 inavyoweza kumfanya mtawala akawa jambazi, mtekaji, mtunguaji na hayawani kabisa, na akifanya unyambilisi wake wote huo, hamna wa kumuuliza, wote mnaufyata mkia
 
SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
338
250
Ni ukweli usiopingika kwamba Sabaya katupa JIWE kwenye mzinga wa NYUKI! Salama ya nchi yetu kwa hili ni SABAYA kuadhibiwa!

Iwapo ataachiwa huru kutokana na kile alichodai uhalifu alioutenda ni MAAGIZO kutoka IKULU! Itadhihirisha wazi kwamba viongozi wa nchi hii ndo wanaohusika na genge la watu WASIOJULIKANA.

Hata kama ni MAAGIZO ya kufanya Opresheni Maalum, si amini kama alielekezwa kwenda kupiga, kupora na kujeruhi!

Acha tusubiri.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,835

Tatizo la Magu ilikuwa ni kutoa order: "...fanya lolote uwezalo ili mradi....". Hii ilifanya watu wafanye kila kitu ili mradi mzee anaridhika. Kweli wengi wameumia hata kupoteza maisha kwa mtindo huu.
 
boomgate

Senior Member
Jan 15, 2021
196
250
Mpunguzieni raisi nguvu kubwa alionayo na pia mifumo imara ya nchi, kama kiongozi anaweza toa oda ya operetiona za kihuni kufanyanyika bila kufuata taratibu na sheria kuna tatzo kwenye vyombo vya ulinzi, washauri wa raisi na usalama wa taifa, vitu vingine ni aibu kwa nchi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom