Sabaya awakana mabaunsa wake: Na iwe fundisho

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Huyu anayelia ni Daniel Bura mmoja wa mabaunsa wa Sabaya. Analia baada ya Sabaya kumkana mahakamani kwamba hamjui. Sabaya amedai hawajui washtakiwa wenzie na kwamba amekutana nao mahakamani na wengine alikutana nao gereza la Kisongo.

Ameiambia mahakama kuwa kati ya washtakiwa 6, anamfahamu mmoja tu Sylvester Nyegu (Kicheche) ambaye anadai alikuwa Mtumishi wa halmashauri ya wilaya Hai. Alipoambiwa "Kicheche" hakuwa mtumishi wa umma, amedai alikua akimuona ofisi za halmashauri hivyo akajua ni mmoja wa watumishi.

Kuhusu Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Jackson Macha, Nathan Msuya na Daniel Bura, Sabaya amesema hawafahamu kabisa na alikutana nao kwa mara ya kwanza Juni 4, 2021 walipofikishwa mahakamani.

"Siku nilipokamatwa na kuletwa mahakamani walinifuata na kuniuliza mimi ndiyo Sabaya? Nikajibu Ndio. Wakasema tumeunganishwa kwenye kesi yako. Hapo ndio ilikuwa mara ya kwanza kuwaona" Sabaya ameieleza mahakama.

Hata hivyo alipoulizwa mbona alikua akionekana na vijana hao maeneo mbalimbali alipokua DC amesema si kweli. Alipooneshwa picha amesema zimehaririwa.

Alipooneshwa video ya CCTV akiwa na mabaunsa wake wakimshambulia mfanyabishara Ally Asaad Ajirin, amesema hakuna ushahidi wa kiteknolojia unaoweza kuthibitisha kuwa wanaooneka kwenye video hiyo ni wao.

Bura alishindwa kujizuia na kuanza kudondosha machozi mahakamani hapo. Yeye ni miongoni mwa mabaunsa watiifu wa Sabaya walioshirikiana kufanya vitendo vingi vya kikatili mkoani K'njaro na Arusha.

Walimvamia Diwani wa Narumu, Nicodemus Mbowe wakamvunja mguu na kumkata sikio mwanae. Walimteka Mchungaji Swai na kumpeleka nyumba ya mateso Arusha. Kwa kushirikiana na polisi wa USA River walimuwekea Profesa Maeda kipande cha mhogo (kilichopakwa polish) na kudai wamemkamata na pembe za ndovu. Wakamchomoa 100M kuzima kesi. Leo Sabaya amewakana wahuni wenzie.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumika vibaya kwa maslahi ya wengine. Ipo siku huyo anayekutumia atakukana maji yakimfika shingoni. Heri wafuasi wa Zumaridi waliokataa dhamana ili wabaki na "Mfalme" wao gerezani kuliko wa Sabaya ambao amewakana kabla hata kesi haijaisha. Asiyefunzwa na *****, hufunzwa na Jamhuri. Iwe Fundisho.!
FB_IMG_1646946650130.jpg
 
Back
Top Bottom