Sabaya asomewa mashtaka mapya ya Uhujumu uchumi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ameipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 27/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita iliyopangwa kwa watuhumiwa kusomewa hoja za awali Septembe 16 mwaka huu.

Baada ya kupewa mamlaka hiyo leo watuhumiwa wote walisomewa mashitaka mapya matano ikiwemo kuongoza genge la Uhalifu ,matumizi mabaya ya madaraka ,Utakatishaji fedha haramu na kuomba rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Francis Mrosso wakati wakijua wazi kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Awali kesi hiyo iliahirishwa baada ya taratibu za kisheria kutokukamilika na Mwendesha Mashitaka wa serikali,Felix Kwetukia aliiomba mahakama kuhairisha kesi hiyo hadi jana ndipo taratibu zilipokamilika za mahakama hiyo kuisikiliza kesi hiyo yenye mvuto wa watu Jijini Arusha.

Mbali ya Sabaya watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na mshitakiwa wa pili Enock Togolani Mnkeni {41} Mkazi wa Arusha,mshtakiwa wa tatu Watson Mwahomange {27} maarufu kwa jina la Malingumu ,Mshtakiwa wa nne, John Odemba Aweyo Mshitakiwa wa tano Syliverster Nyengu{26} mshitakiwa wa sita,Jackson Macha{29} Mkazi wa Msaranga Moshi Kilimanjaro na mshitakiwa wa saba Nathan Msuya{31} mkazi wa Msaranga Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Akisoma shitaka la Kwanza linalowahusu washtakiwa wote,Mwendesha Mashitaka wa Serikali ,Tasilia Gervas mbele ya Hakimu Mkazi,Patricia Kisinda alidai kuwa mnamo januari 22 mwaka huu Sabaya aliongoza genge la uhalifu na wenzake huku akijua ni mtumishi wa Umma Kwa maksudi walijipatia shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Gervas alisoma shitaka pili linalomkabili Sabaya mwenyewe kama mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni kujihushisha na rushwa kwa kumshawishi Mfanyabiashara Mrosso kutoa kiasi cha shilingi milioni 90 ili aweze kumsaidia katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi ya serikali iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara huyo.

Shitaka la tatu linalomkabili Sabaya ni kuchukua au kupokea rushwa ya shilingi milioni 90 ili asitoe taarifa za kesi ya jinai ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili Mfanyabiashara Mrosso mkazi wa Kwa Mrombo Jijini Arusha.

Mwendesha Mashitaka wa serikali alisoma shitaka la nne linalomkabili Sabaya kama mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia nafasi yake ya Ukuu wa wilaya januari 22 mwaka huu alimtisha Mfanyabiashara Mrosso kumfungulia mashitaka ya ukwepaji kodi iwapo atagoma kutoa kiasi cha shilingi milioni 90 alizohitaji.

Gervas alisoma shitaka la tano linalowakabili washitakiwa wote saba ni Utakatishaji fedha haramu shilingi milioni 90 ambapo watuhumiwa hao wote wanatuhumiwa katika nyakati tofauti ndani ya Jiji la Arusha kufanya uhalifu huo.

Watuhumiwa wote walikana mashitaka hayo mbele ya Hakimu Kisinda na Mwendesha Mashitaka aliomba tarehe ya kusoma maelezo ya awali kwa watuhumiwa wote na Hakimu alihairisha kesi hiyo hadi septemba 16 mwaka huu.

IMG_20210909_115146_752.jpg
IMG_20210909_115204_416.jpg
IMG_20210909_115206_588.jpg
 
Baaaaaaado sana hayo mashtaka ni sehemu ndogo mno ya ushenzi wa huyu Sabaya.
 
Back
Top Bottom