Sabaya akithibitisha Mahakamani kuwa Mbowe na genge lake walitaka kumuua itakuwaje?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Katika utetezi wake Sabaya alidai kuwa alikuwa na maadui wengi wa kisiasa huko Hai na walitaka kumuua ndio maana alikuwa akimiliki bastola aina ya Glock 17. Na ameenda mbali akadai hata kesi yake ni fabricated sababu hao maadui zake walipanga kummaliza kisiasa.

Tumepigwa na butwaa kumbe maadui wa Sabaya ni Mbowe na genge lake. Sasa wapo mahakamani kwa tuhuma za kutaka kumdhuru Sabaya na ugaidi.

Mmoja wa mashaidi wa utetezi ni Sabaya Ole Sangai. Je akifika mahakani akasema Mbowe na wenzake walipanga kumuua na kumdhuru utetezi wa akina Mbowe utakaa vipi?

N.b Sabaya alimshughulikia kisiasa Mbowe huko Hai mpaka akanyoosha mikono.
 
Sio kila Jambo ni maelekezo na uteuzi. HAKI hucheleweshwa tu na wadwanzi.
 
Athibitishe lini tena? Amemaliza utetezi sijasikia kokote akisema Mbowe alitaka kumuua. Kinachosubiriwa sasa ni maamuzi ya mahakama.
 
Katika utetezi wake Sabaya alidai kuwa alikuwa na maadui wengi wa kisiasa huko Hai na walitaka kumuua ndio maana alikuwa akimiliki bastola aina ya Glock 17. Na ameenda mbali akadai hata kesi yake ni fabricated sababu hao maadui zake walipanga kummaliza kisiasa...
Kwani ni kutamka pekee ndo kunatosha!?
 
Katika utetezi wake Sabaya alidai kuwa alikuwa na maadui wengi wa kisiasa huko Hai na walitaka kumuua ndio maana alikuwa akimiliki bastola aina ya Glock 17. Na ameenda mbali akadai hata kesi yake ni fabricated sababu hao maadui zake walipanga kummaliza kisiasa...
Kwa hiyo Mbowe ndiye aliye mvuruga kiasi cha kwenda kuvamia maduka ya watu na kupora mali!! baada ya kupanga kumuua na kumdhuru!!

Bila shaka una mahaba niue kwa Sabaya. Ngoja kwanza ale mvua za kutosha mwezi ujao, then akili yako itatulia tu.
 
Ushahidi wake hautakua na mashiko, asubuhi na mapema upande wa utetezi (Kibatala na Wenzake) watampa za uso na kumjeruhi kisawasawa.

Kwanza wataanza kumrarua rarua na Character Assassination, watamchafua kwa kuwa na rekodi za kutenda makosa ya jinai (Criminal Records), matumizi mabaya ya Ofisi za Umma kama kiongozi mteule, na uonevu kwa raia.

Pili, baada ya kumrarua kwa kutumia rekodi zake za jinai, watampasua pasua kwenye mashiko ya ushahidi wake (Credibility Of Witness & Evidence), wataishawishi mahakama kwamba sio shahidi wa kuaminika kutokana na historia yake, hatokua shahidi wa kuaminika na mahakama (Sio Credible Witness).

Asipokua makini, watamkunja kunja na anaweza hata kuishia kujitia (Inciminate) yeye mwenyewe kwenye makosa ya jinai mengine. Anaweza kujizulia matatizo mengine.

Kibatala (Wakili Kiongozi), Generali Ulimwengu (Wakili Kivuli) na Fatma Karuma (Wakili Kivuli), Tundu Lissu (Wakili Kivuli) na kuna mawakili wengine wanaomtetea Freeman Mbowe ni wauwaji kwenye kupiga maswali mashahidi.

Ni upumbavu wa kiwango cha lami kumpeleka Ole Sabaaya kama shahidi wa Jamhuri. Anaweza akaiharibu kesi kwa upande wa Jamhuri badala ya kuitengeneza kesi.

NOTE THAT: Ole Sabaaya akiulizwa; Wewe ni mhalifu na una rekodi ya kutenda makosa ya jinai na kuvunja uaminifu wako wa kiapo, kwanini mahakama ikuamini kama awali uliwahi kuaminiwa na hukuaminika?

*Wakili kivuli ni ambae hasimami yeye kama yeye mbele ya mahakama kwenye kesi, ila ushauri na mtazamo wake unatumika na mawakili wengine kwenye kesi.

IGP Sirro na Ole Sabaaya kama watatoa ushahidi basi ndio watakaompa ushindi Freeman Mbowe katika kesi hii.
 
Katika utetezi wake Sabaya alidai kuwa alikuwa na maadui wengi wa kisiasa huko Hai na walitaka kumuua ndio maana alikuwa akimiliki bastola aina ya Glock 17. Na ameenda mbali akadai hata kesi yake ni fabricated sababu hao maadui zake walipanga kummaliza kisiasa....
Si Sabaya tu.

Unaonaje na wewe kama ukienda kuongezea kwa Sirro kuwa na wewe ulikuwa kwenye list hiyo ya kuuliwa?
 
Jambazi lililokiri lilikuwa linatumwa na mwendazake leo linadanganya wajinga lilikuwa linatishiwa uhai wake, lilikiri nchi hii aliekuwa anaongea nalo ni marehemu pekee wengine wote walikuwa kama watoto kwake, leo linajichanganya na kudai lilikuwa linawindwa, atakaeliamini hilo ni mjinga tu.
 
Yani Sabaya awe na udhibitisho kuwa alitaka kuuliwa na Mbowe alafu akae na huo ushahidi tangu July 2020 alafu Mbowe awe free hadi wamkamate July 2021??

Yani Sabaya awe na ushahidi wenye udhibitisho kuwa Mbowe alitaka kumuua alafu mwendesha mshtaka asimuweke kwenye list ya mashahidi wa jamuhuri??

CCM na Step Maa wenu kama tu hii charge sheet yenu mmeshindwa kuiona ilivyo na matobo ya kuicha jamuhuhuri uchi ni bora mkae kimya mpakane shedo.
 
Je Sabaya akiulizwa yeye ndiye alitaka kumuuwa Mbowe analo la kujitetea? na kuaminisha mahakama sio kweli?
 
Yani Sabaya awe na udhibitisho kuwa alitaka kuuliwa na Mbowe alafu akae na huo ushahidi tangu July 2020 alafu Mbowe awe free hadi wamkamate July 2021??

Yani Sabaya awe na ushahidi wenye udhibitisho kuwa Mbowe alitaka kumuua alafu mwendesha mshtaka asimuweke kwenye list ya mashahidi wa jamuhuri??

CCM na Step Maa wenu kama tu hii charge sheet yenu mmeshindwa kuiona ilivyo na matobo ya kuicha jamuhuhuri uchi ni bora mkae kimya mpakane shedo.

Naunga mkono hoja:

"CCM na Step Maa wenu kama tu hii charge sheet yenu mmeshindwa kuiona ilivyo na matobo ya kuicha jamuhuhuri uchi ni bora mkae kimya mpakane shedo."

Hiiiiii bagosha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom