Sababu zitazoifanya CCM kuibuka kidume Arumeru Mashariki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu zitazoifanya CCM kuibuka kidume Arumeru Mashariki!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by chama, Mar 5, 2012.

 1. c

  chama JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pamoja na upinzani unaonyeshwa na Chadema katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki; CCM itaibuka na ushindi wa kati ya asilimia 51-55; zipo sababu nyingi lakini hizi ndizo hasa zitazoipa CCM ushindi

  1. Sera za CCM pamoja na kwamba serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza baadhi ya sera zake bado watanzania wana imani na chama chao na ukitilia maanani sera kubwa za wapinzani ni kuongelea ufisadi huku wakiacha kuelezea sera zao.


  2. Busara za CC na NEC ya CCM kumpitisha mshindi wa kura za maoni ndugu Siyoi; pamoja na kuwa rushwa ilitawala vyombo vya juu vya CCM viliamua kulifumbia macho jambo hilo ili kuondoa mtafaruku; na kuleta umoja ndani ya chama

  3. Katiba ya nchi bado inaipa nguvu chama tawala kushinda chaguzi; hapa hatuangalii tume huru lengo ni kushinda uchaguzi.

  4. Kushindwa kwa vyama vya upinzani kusimamisha mgombea mmoja; Chadema imeshindwa kuvishawishi vyama vingine vya upinzani kutosimamisha wagombea hii ni faraja kubwa kwa CCM; EVERY VOTE COUNT! Kinyang`anyiro hiki ni kikali CCM tayari inao mtaji wa kutosha tunahitaji msaada kidogo kutoka kwenye vyama vingine vya upinzani ambao tayri tumeshaupata.

  Kwa kumalizia tu ndugu Siyoi andaa suti ya kuingia nayo mjengoni.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,966
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  CCM kushindwa kutekeleza ahadi, Kumpitisha mtuhumiwa wa Rushwa kwa busara ya CC kama ndizo sababu ya Siyoi kuibuka Mshindi Mkuu umewadhalilisha Wameru! Unadhani Wameru hawaoni uchafu wote huo wa ccm na serikali yake?
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi wameru wanatofauti gani na watanzania wengine? haya ni marudio tu wameru wamefika CCM kama walimpa baba sasa watampa mwana; wameru CCM ndio nymbani kwao!

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ongeeni kwanza na madaktari
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hakuna umoja hapo kama si nguvu ya pesa huyu bwana asingengombea na yamkini atashinda kwa nguvu ya pesa

  hapa umesema ukweli kwani mshindi anaweza patikana na kwa hila akatangazwa mwingine
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 6,713
  Likes Received: 887
  Trophy Points: 280
  Ushindi wa ccm unapatikana kwa nguvu ya pesa na matumizi ya dola full stop ukisema sela ni unafiki.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,966
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ukiwa CCM uwezo wa kufikiri unapotea kabisa. Akili inadumaa unawaza upumbavu basi!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,012
  Likes Received: 6,024
  Trophy Points: 280
  Kama CCM inaweza kufumbia macho vitendo vya rushwa ili kuondoa mtafaruku na kuleta umoja ndani ya chama,
  1. Kwa nini Lowassa anaandamwa?
  2. Kwa nini Chenge anasakamwa?
  3. Kwa nini dogo Nape analalama?
  Alaaah, kumbe ndio maana....! Ni mshikamano kwenye rushwa, wizi na hata mauaji ndio maana huko Arumeru tumeshashuhudia rushwa na sasa tunasubiri wizi na ikibidi mauaji - naambiwa kikosi cha mauaji tayari kiko mbioni kinaelekea huko kikijiita polisi. Namsubiri Pasco afanye jitihada apate angalau picha ya Nape na Lowassa wakipeana mkono kwenye jukwaa la kampeni kwani rushwa imefuta dhambi zao na wamebaki wasafi kama theluji!
   
 9. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,685
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mkafie mbali magamba mtakacho kiona arumeru ndio utangulizi wa 2015'viva chadema viva wapamcnaji!!!!
   
 10. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa mnaenda kwenye uchaguzi kufanya nini?
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi mkuu kwa asilimia 70 kwani sasa sera ya vyama vyetu vya upinzani ni ufisadi kitu ambacho naona kama ni dalili za vyama hivi kupoteza mwelekeo
   
 12. K

  Kiraka Timothy Peter Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa tumjibu kwa hoja jamani..wacha nikupe sababu zinazonipa matumaini ya kukipoteza hiki chama chetu magumashi pale Arumeru.

  1.Daima CCM wamekuwa watoaji wazuri wa ahadi zisizotekelezeka.Wanapanga mipango na sera wakiangalia zaidi shibe ya leo bila kutazama njaa ya kesho..

  2.Kutokutekelezeka kwa ahadi hizi butu za CCM kumewafanya watanzania wengi kupoteza imani na chama hiki tawala..

  3.kutokana na kupoteza mwelekeo,wananchi wengi wameanza kuzitazama kwa makini sera za wapinzani ambazo nyingi zina kila dalili ya kutekelezeka kwa kuwa zinawapa nafasi wananchi kuwa na sauti juu ya mipango inayopangwa kwa ajili ya maendeleo yao.

  5.Jukumu msingi la kiongozi bora ni kutetea ustawi,uhuru,maendeleo na haki ya anaowaongoza.kwa kupinga ufisadi,wapinzani wanatupa ahueni ya hali mbaya tuliyonayo kwa rasilimali zetu kutumiwa vibaya kuwanufaisha wachache

  6.Serikali ya CCM imeshindwa kuyatolea tamko baadhi ya matatizo makubwa yanayowasumbua wananchi,watu wa Arumeru wakiwemo.

  7.Kumpitisha mtuhumiwa wa Rushwa bw.Siyoi dhidi ya mtu safi asie na harufu ya kashfa Bw.Nassari(MB) kunawapa watu wenye busara wanaomchukulia mbunge kama mwakilishi anaepaswa kua makini nafasi kubwa ya kumchagua Nassari..

  8.Siasa ni uwezo,sio kalamu ya kurithishana kindugu..Siyoi yuko hapo alipo sio kutokana na uwezo na utashi wake,bali nature inamnyanyua kwa misingi ya kuwa baba yake alikua mbunge,labda kwakua watanzania tunapenda kuwafariji waliofikwa na matatizo tutampa kura ziwe faraja.Lakini Nassari yuko makini na ana juhudi za kusonga mbele hata kama ni mtoto wa mfugaji...

  MUNGU IBARIKI TZ,
  MUNGU WABARIKI WATANZANIA,
  MUNGU WABARIKI WANA ARUMERU(MASH)
  MUNGU UBARIKI UPINZANI,
  MUNGU KIBARIKI CHADEMA,
  MUNGU MBARIKI MTEULE WAKO BW.NASSARI!
   
 13. c

  chama JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kiraka Timoth Peter
  Kama sikosei kabla ya kura za maoni Nassari alichangiwa na wapambe wake zaidi mil.10 hizo pesa zilikua ni kwa ajili ya kuwahonga wajumbe. Wananchi wanaelewa hizi chaguzi ndogo hazina ushindani kama zile zinazoambatana na uchaguzi wa raisi na zaidi wanafahamu fika wabunge hawana pesa za kupeleka maendeleo hivyo ni rahisi sana kwa kugombea kutoka chama tawala kushinda, serikali ndiyo inayopeleka maendeleo.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 14. c

  chama JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Magamba yapo Chadema pia kama huyajui sema tukufahamishe

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,346
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  sababu zako nyingi ulizozitoa zinaonyesha wazi kuwa unaipenda CCM kuliko nchi yako na hilo ndio tatizo kubwa la baadhi ya watanzania. huko tayari nchi iangazwe na rushwa ili mradi tu wala rushwa hao wanatoka CCM.

  Huko tayari kuona demokrasia ndani ya Tanzania inakandamizwa ili mradi tu anayenufaika na ukandamizaji huo ni CCM.

  Naninaamini kabisa huenda ukawa tayari kukubali ukabila na udini utumike kwenye siasa ili mradi tu CCM ishinde huku nchi ikiangamia. watu kama nyie ni aibu katika taifa lolote kwa maana mumeweka political expediences mbele kwa ajili ya tonge la ugali.
   
 16. l

  luckman JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  uwezo wako wa kufikiri nina wasiwasi nao, kama unadhani ujinga hapo juu kwenye colored lines hii inadhihirisha kuwa u mtupu kichwani, mtu mwenye uelewa hawezi kushabikia upuuzi wa kijinga namna hii!kajipange arumeru ishawashinda!
   
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,549
  Likes Received: 2,281
  Trophy Points: 280
  CCM kitu gani bwana,wanaweza wakagawa sana pesa na mwisho wa siku wakaambulia patupu,sio kila anayehongwa anaafiki matakwa ya mhongaji.
   
 18. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe kupenda kitu kiwe au kiende katika matamanio yako haimaanishi kwamba ni kweli itakuwa hivyo.Jitahidi kuelekeza reasoning yako kwenye uhalisia zaidi ya kutawaliwa na emotions za matamanio yako.Kama ingekuwa unavyofikiri wewe ni obvious majimbo yote yangekuwa ccm. Tafakari.
   
 19. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,090
  Likes Received: 3,462
  Trophy Points: 280
  Kama Sera hazijatekelezeka why washinde?Kama Sioa kapita kwa rushwa why ashinde?Arumeru ni wajinga wasione haya?
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,234
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chama,
  Mie nakubaliana na wewe kwenye namba 1 na namba 3 hivyo vigezo viwili tu vitaipa ushindi CCM Arumeru.
   
Loading...