Sababu zipi, zinazokupelekea wewe kwenda kunywa pombe maeneo ya starehe?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,340
40,203
Ni sababu zipi, zinazokuvutia wewe kwenda kunywa pombe bar, pub au club? Kwa nini usiagize vinywaji ukanywea nyumbani?

Wengi tunaamini, kama utaamua kuagiza vinywaji na kunywea nyumbani kuna faida nyingi sana; mojawapo ni kubana matumizi, kwa sababu hutoshawishika kutumia zaidi ya bajeti uliyoipanga.

Lakini bado watu wanashawishika kwenda kunywa pombe maeneo ya starehe kama vile; bar, pub, club n.k

Sasa tunataka tujue, ni sababu zipi zinazokupelekea wewe kwenda kunywa pombe maeneo ya starehe?
 
mimi ni kubadili mazingira mfano ufukweni mf capetown fish yaani mazingira yanavutia kulipo mazingira ya nyumbani,na pia company kwani kuna baadhi ya watu huwezi kuwakaribisha home kunywa na kuongea frequently, pia utulivu ukiwa na ishu zako za kutafakari unakwenda zako bar zenye utulivu.
ninakwendaga bar ila sio zile bar za kupiga miziki yenye makele yaani kulipo huko ni kheri niende kwenye viosk vya mangi kwa jirani
 
Kuna muda huwa napanga kunywea nyumbani, lakini ugimbi ukishaanza kupanda kichwani nitaondoka tu niende bar ya mbele kidogo nikanywe bia huku nikihudumiwa na wahudumu wenye matacle makubwa.
Ila bia za mchana na asubuhi huwa nashitulia tu kwa mangi sina.
Majibu yameanza kupatikana, kumbe kinachotupeleka maeneo ya starehe sio pombe tu?
 
Kuna muda huwa napanga kunywea nyumbani, lakini ugimbi ukishaanza kupanda kichwani nitaondoka tu niende bar ya mbele kidogo nikanywe bia huku nikihudumiwa na wahudumu wenye matacle makubwa.
Ila bia za mchana na asubuhi huwa nashitulia tu kwa mangi sina.
Ugimbi wa nyumbani hapana bora kwenda kutalii bar
 
Kilaji humu DJ anafanya yake nyimbo zinaenda nyororo swaafi kabisa..unaongeza zingine na zingine...
 
Muziki hata nyumbani unaweza kuwepo, kwa hiyo sababu uliyoitoa inaweza kuwa sio jibu sahihi
 
Ni sababu zipi, zinazokuvutia wewe kwenda kunywa pombe bar, pub au club? Kwa nini usiagize vinywaji ukanywea nyumbani?

Wengi tunaamini, kama utaamua kuagiza vinywaji na kunywea nyumbani kuna faida nyingi sana; mojawapo ni kubana matumizi, kwa sababu hutoshawishika kutumia zaidi ya bajeti uliyoipanga.

Lakini bado watu wanashawishika kwenda kunywa pombe maeneo ya starehe kama vile; bar, pub, club n.k

Sasa tunataka tujue, ni sababu zipi zinazokupelekea wewe kwenda kunywa pombe maeneo ya starehe?
Kwanza vibe yaan linaweza likapigwa goma moja kabambe likakukumbusha mbali sanaa mpaka ukaanza kukata viuno bar nzima wakabak midomo waz cha pili kampan unaweza kuonana na marafiki zako ambao uliwai kuwaona zaman sanaa tatu kama unapendwa makachumbari yapo ya kila aina yanapita pita na nguo za kila namna
 
Kwa mtazamo wako ni kipi kisikosekane katika maeneo ya starehe?
 
Mziki yaan burudan pili manzingira yaan mandhari tatu vibe hili linatokana na uchnagamfu wa sehem husika kwa ujumla mda mwingi huchangiwa na mambo mawili ya juu yaan mazingira yaa marembo marembo na mziki yaan curent song maana unaweza kwenda bar leo wanapiga nyimbo za diamond za mwaka 2009 mwisho wahudumu wawe mashamalaah maana ukilewa kuwaona tu raha
 
Back
Top Bottom