Keisha ang’olewa ujumbe Kamati Kuu ya CCM baada ya siku 396

chokaa nyeusi

Member
May 9, 2019
46
60
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumwondoa Khadija Shabani Taya maarufu ‘Keisha’ baada ya kukitumikia chombo hicho nyeti kwa siku 396.

keisha+pic.jpg

BY Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Advertisement

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumwondoa Khadija Shabani Taya maarufu ‘Keisha’ baada ya kukitumikia chombo hicho nyeti kwa siku 396.

Keisha, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, uteuzi wake kwenye Kamati Kuu ulionekana kama angekuwa kiungo cha kuleta uhamasishaji wa sera za chama kwa wasanii nchini.

Msanii huyo ambaye ni kada wa CCM aliteuliwa kuingia kwenye chombo hicho cha uamuzi Mei 28, 2018. Kamati Kuu ina wajumbe 24 wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Uamuzi wa Keisha kuondolewa ulitangazwa Ijumaa iliyopita Juni 28 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichokutana Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Magufuli.

Keisha aliteuliwa siku moja na wajumbe wengine wawili kutoka Tanzania Bara kuingia Kamati Kuu ambao ni Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na aliyewahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Makongoro Nyerere ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere

Pia, wajumbe watatu kutoka Zanzibar waliteuliwa siku hiyo hiyo ambao ni Afadhali Taibu Afadhali, Kombo Hassan Juma na Lailah Burhan Ngonzi.

Kikao cha Halmashauri Kuu kilitangaziwa uamuzi huo wa kuondolewa kwa Keisha na kuteuliwa kwa Munde Tambwe ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Tabora.

Mwananchi lilizungumza na Keisha kutaka kujua sababu ya yeye kuenguliwa kwake ambapo alisema,” hilo halipo kwenye nafasi yangu kulijibu, waulize walio kwenye nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya chama.”

Majibu hayo yalilifanya Mwananchi kumtafuta katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ambaye naye alisema atafutwe katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

“Kuna mgawanyo wa madaraka, mtafute Polepole au endelea kufuatilia taarifa zake, yeye ndiyo anaweza kutoka taarifa juu ya hilo,” alisema Dk Bashiru.

Mwananchi lilipomtafuta Polepole kutaka kujua kwa nini Keisha ameenguliwa kwenye nafasi hiyo, Polepole alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka ifuatavyo, “Halmashauri Kuu ya Taifa ina mamlaka ya kupanga na kupangua ili kuongeza tija na kutumia ujuzi na umahiri wa wajumbe katika kuongeza tija na ushindi wa CCM.”

Ingawa Polepole hakueleza kwa nini wamemuengua, kuna vyanzo vinavyodai kuwa Keisha ameondolewa katika chombo hicho cha juu chenye wajumbe 24 akituhumiwa kuvujisha siri za vikao mbalimbali vya chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1977.

Chanzo: Mwananchi
 
Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumwondoa Khadija Shabani Taya maarufu ‘Keisha’ baada ya kukitumikia chombo hicho nyeti kwa siku 396.

Keisha, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, uteuzi wake kwenye Kamati Kuu ulionekana kama angekuwa kiungo cha kuleta uhamasishaji wa sera za chama kwa wasanii nchini.

Msanii huyo ambaye ni kada wa CCM aliteuliwa kuingia kwenye chombo hicho cha uamuzi Mei 28, 2018. Kamati Kuu ina wajumbe 24 wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Uamuzi wa Keisha kuondolewa ulitangazwa Ijumaa iliyopita Juni 28 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichokutana Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Magufuli.

Keisha aliteuliwa siku moja na wajumbe wengine wawili kutoka Tanzania Bara kuingia Kamati Kuu ambao ni Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na aliyewahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Makongoro Nyerere ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Pia, wajumbe watatu kutoka Zanzibar waliteuliwa siku hiyo hiyo ambao ni Afadhali Taibu Afadhali, Kombo Hassan Juma na Lailah Burhan Ngonzi.

Kikao cha Halmashauri Kuu kilitangaziwa uamuzi huo wa kuondolewa kwa Keisha na kuteuliwa kwa Munde Tambwe ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Tabora.

Mwananchi lilizungumza na Keisha kutaka kujua sababu ya yeye kuenguliwa kwake ambapo alisema,” hilo halipo kwenye nafasi yangu kulijibu, waulize walio kwenye nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya chama.”

Majibu hayo yalilifanya Mwananchi kumtafuta katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ambaye naye alisema atafutwe katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

“Kuna mgawanyo wa madaraka, mtafute Polepole au endelea kufuatilia taarifa zake, yeye ndiyo anaweza kutoka taarifa juu ya hilo,” alisema Dk Bashiru.

Mwananchi lilipomtafuta Polepole kutaka kujua kwa nini Keisha ameenguliwa kwenye nafasi hiyo, Polepole alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka ifuatavyo, “Halmashauri Kuu ya Taifa ina mamlaka ya kupanga na kupangua ili kuongeza tija na kutumia ujuzi na umahiri wa wajumbe katika kuongeza tija na ushindi wa CCM.”

Ingawa Polepole hakueleza kwa nini wamemuengua, kuna vyanzo vinavyodai kuwa Keisha ameondolewa katika chombo hicho cha juu chenye wajumbe 24 akituhumiwa kuvujisha siri za vikao mbalimbali vya chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1977.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom