Wanabodi,
Najaribu kujiuliza kwanini Magufuli hakwenda Zanzibar kwenye sherehe ya Mapinduzi na badala yake akawa Shinyanga. Najua alilifafanua hilo kwa kusema anavunja utamaduni ili sherehe ziwe kitaifa zaidi.
Lakini nikiangalia mahudhurio ya viongozi kule Zanzibar, napata shida kidogo, kwani kwangu mimi ile ilikuwa fursa adimu iliyokutanisha Maraisi wote wastaafu wa Muungano na Visiwani. Mwinyi, Mkapa, Kikwete , Karume , na mwenyeji wao Shein.
Ukijumlisha na Mama Samia, ni kwamba nchi yote ilikuwa kule
Hapo bila shaka wangepata muda wa kupata chakula pamoja, na katika hapo yangeanza matani na pengine serious talk ya kila mmoja kutoa uzoefu wake katika uongozi wa nchi, na pengine wangepata kujadili hili au lile kwa mustakabali wa nchi.
Hoja yangu hapa, je Magufuli hakuona umuhimu wa kuwa pamoja na wenzake kule Zanzibar? Najua alikuwepo Mama Samia, lakini Makamu hawi Raisi mpaka Raisi asiwepo. Maana yake kuna baadhi ya mambo hawezi kuyatolea ufafanuzi wa moja kwa moja mpaka amuulize mkuu wake.
Labda mie nawaza tofauti, lakini hembu nisaidieni ma GT wa humu....nina sababu ya kuwa na duku duku hili?