Sababu zinazopelekea kukataliwa kuposa/Kuchumbia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
KUKATALIWA KUPOSA/KUCHUMBIA AU KUCHUMBIWA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Mmekutana chuoni, au mjini, hisia zenu zikavutana kwa nguvu ya mapenzi, mkaanza kuhusiana; hisia zenu zikifurahia kukutana kwenu. Mkafahamiana kwa majina ya siri baada ya kufuta majina ya uongo mliodanganyana siku ya kwanza mliyoonana. Sasa ni dhahiri kila mmoja anahisi kuwa bila mwenzake maisha hayawezekani. Wingu la mvua ya mapenzi limetanda mioyoni mwenu, kuna kila dalili matone ya ndoa yatadondoka chini na kuotesha familia nzuri iliyostawi. Lakini baadaye mkagundua kuwa matone hayo ili yawe ya baraka hakuna budi kwenda nyumbani kwa wazazi kujitambulisha na kuonyesha adhma yenu ya kutaka kuishi pamoja kama mume na mke, mkifanya maisha pamoja kwa upendo mlionao.

Lakini haiwi ikawa, dosari mbaya ya uchungu inavamia penzi lenu motomoto. Wazazi wa upande mmoja wanakataa katakata kuhusu kuoana kwenu. Na hima bila kupima hisia zenu wanataka muziondoshe hizo hisia zenu za mapenzi kabla wao wenyewe hawajafanya hivyo.
Nakuona jinsi machozi ya uchungu yakikutoka, nauona moyo wako ukipiga kwa kite huku akili yako ikimezwa na roho ya chuki kwa wazazi wako au pengine wazazi wa mwenza wako. Inauma! Tena inafisha mishipa ya upendo moyoni.

Nafahamu kupenda, tena kupenda kwa mara ya kwanza ndiko kupenda halisi. Najua jinsi hisia za mapenzi ya kwanza kabisa jinsi zilivyo. Hisia utawala akili na mwili mpaka roho kukosa mhimili. Siio ajabu mtu kujitoa kufa kisa mapenzi katika awamu ya kwanza ya mapenzi, tena uyafumanie mapenzi kwa mwenza mwenye sifa za kiithibati.

Utasema nataka kujua kwa nini HAMUMTAKI HUYU AWE MWEZA WANGU WA MAISHA? Hata hivyo swali hilo hutaliuliza kwa akili isipokuwa HISIA za mapenzi ndizo zitakuwa zikikuongoza. Hakuna sababu ya kimantiki utakayoisikia kwa sababu akili yako itakuwa haifanyi kazi muda huo. Akili itakayokuwa ikifanya kazi ni ile itakayokuambia kuwa Wazazi wako hawakupendi na wanatumia mabavu kuingilia maisha yako.

Usifikiri, wala usiwaze labda unyamaze kuipa akili yako utulivu unisikie kwa uchache,
Sababu zitakazo ukataliwe ukweni kuposa, au kuchumbia au kuchumbiwa ni kama Ifuatavyo;

1. IMANI
Jambo la kwanza kabisa na nyeti ambalo litazingatiwa litakalokufanya upigwe Technical Knockout ni suala la utofuati wa Kiimani.
Na wazazi wako wanayohaki zote za msingi kukukatalia na kukuonya dhidi ya tukio unaloenda kulifanya.
Imani ni nguzo ya lazima ndani ya ndoa, imani ndio inaelekeza mtu akupendeje, akujalije, akuheshimuje, na pakiwa na matatizo imani ya ndoa hasa yale makubwa imani ndio huwa kimbilio.

Ukioa mtu mwenye imani za kishirikina na ulozi wakati wewe huna imani na mambo hizo unajikaanga mwenyewe. Mlozi na mshirikina huamini kila kitu ndani ya ndoa hutokea kwa sababu ya kulogwa au kuchezewa. Muumini wa ushirikina huamini kuwa ili mapenzi yanoge basi haina budi kwenda kwa waganga akamtengeneze mume wake. Kupewa limbwata, kulishwa uchafu wa kichawi na mwenza wako mwenye imani za kishirikina ni ishu za kawaida unazopaswa uzitarajie.
Mkeo akiwa mshirikina haoni shida kuwekewa uchawi kwenye uke wake ili ukimuingilia upagawe.

Kama mumeo ni muumini wa ushirikina na ulozi, sio ajabu akaenda kwa waganga kuchanjiwa kwenye uume wake ili akuingiliapo uzidi kumfurahia na kumpenda zaidi. Mwanaume mlozi ni kawaida kuoa wanawake zaidi ya mmoja tena mpaka saba na wakakaa pamoja bila kugombana. Ila wewe mwenzangu na miye hutaweza usije ukajaribu utajuta.

Mwenza mwenye imani ya ALLAH hawezi kuishi na mwenza mwenye imani ya YAHWE au Yesu wa Nazareth.
Allah anaruhusu Kuoa Wake wengi wakati YAHWE au Yesu wa Nazareth huruhusu Mke mmoja.
Allah anaruhusu Talaka wakati YAHWE anasema ni mpaka kifo kiwatenganishe.
Asije mtu akakudanganya au ukajidanganya kisa hisia zako za mapenzi ziko juu kwa muda huu, huwezi kuwa na mwenza ambaye tofauti na wewe kiimani.

Ndio maana wazazi wanawaze kukukatalia hata uje na mapesa yako.

Imani ipo kiwango cha kidunia. Twende kitaifa.

2. UTAMADUNI
Wazazi wanaweza wakakukatalia kuolewa au kuoa mwenza ambaye kwao kunautofauti mkubwa wa kiutamaduni na kwenu.
Wazazi wanazo haki hizo na wanayomamlaka ya kukataa wewe usoe wala usiolewe na mwenza wako huyo hata kama unampenda kufa.
Kwa mfano zipo tamaduni ambazo ni Matrilineal societies ambazo Upande wa mwanamke ndio unatawala. Mifumo ya jamii hizi kwa sehemu kubwa hutofautiana na mifumo ya Patrilineal societies.
Huwezi oa mwanamke anayetoka jamii za matrilineal society alafu ukalalamika kwa nini anakutawala labda uwe kichaa, au kwa nini familia yake inaingilia ndoa yenu.
Zipo jamii ambazo tamaduni zao zinamruhusu Mjomba mtu kumbikiri mwenza wako ndipo wewe umchukue. Halikadhalika zipo jamii ili uoe unapaswa ulale na Shangazi mtu ili apime nguvu zako za kiume kwamba unaweza kummudu mtoto wao.
Zipo jamii kulala na mabinamu zao sio shida.
Zipo jamii ni desturi kuachika kwenye ndoa ya kwanza kisha ndio aolewe rasmi.
Zipo jamii matambiko na kuabudu mizimu ni sehemu ya ibada.
Zipo jamii mwanamke kwenda kwenye vigodoro na kubambiwa na wanaume wengine mbele ya mume wake ni jambo la kawaida.

Hivyo wazazi wanapoona upo utofauti mkubwa wa kiutamaduni baina yako na mwenza wako wanaweza wakakataa ndoa yako.
Ndio maana katika maswali ya awali utakayoulizwa na wazazi wako, utaulizwa mwenza wako kwao wapi au anaasili ya wapi.

3. KAZI
Unaweza kukosa mke/mume kama huna kazi.
Sifa mojawapo ya mke au mume bora ni kazi. Hakuna mzazi anayejielewa na anayekupenda ambaye ataruhusu mwanaye afunge ndoa na mwenza asiye na kazi. Ndio maana katika maswali matatu ya mwanzoni kabisa utakayoulizwa ni pamoja na kazi ya mwenza wako.

Ipo Kasumba kuwa Mwanamke hafanyi kazi, sio kweli na inategemea na jamii hasa zile jamii masikini. Ndio maana nikaeleza hapo juu kuwa inategemea na IMANI na TAMADUNI. YAHWE anasema katika vitabu kuwa MKE MWEMA sharti awe mchapakazi yaani lazima awe mfanyakazi.
MITHALI 31:
10Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;
Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22Hujifanyia mazulia ya urembo;
Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;
Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

Halikadhilika na Mume bora lazima awe mfanyakazi, awe mchapakazi, asiwe zoba. Anaweza kuwa amejiajiri au ameajiriwa ila sharti awe mfanyakazi.

Unaweza nyimwa mke kwa sababu huna kazi, au jamii unayotoka inasifa za watu wavivu wasiopenda kufanya kazi.

4. AFYA NA MAUMBILE.
Unaweza kukosa mke/mume na kukataliwa kwao kwa sababu ya Afya yako na maumbile yako. Na hili huja baada ya mwenza wako kufika nyumbani kutambulishwa. Huwezi ulizwa swali la afya na maumbile ya mwenza wako pindi akiwa hayupo, isipokuwa siku utakayoenda kumtambulisha kwenu ndio siku inayosubiriwa kwa hamu zote na wazazi, ndugu na jamaa.
Siku hiyo mwenza wako atakaguliwa kwa macho ya nje hasa kutazama maumbile yake, kama ni mrefu au mfupi, kama ni mweupe au mweusi, kama anavutia au havutii miongoni mwa mambo mengine. Unaweza ona naongea mambo yasiyo na maana lakini waliooa wanaelewa kile nikisemacho.

Kama umepeleka msichana mzuri kupindukia alafu wewe hauna uzuri huo na wala hauna pesa, ninakuhakikishia wazazi wako watakuambia usimuoe huyo mwanamke. Kwa sababu wanajua kinachofuata miaka kadhaa inayokuja. Hawataki uteseke.

Mwenza wako kama anamaradhi ya kurithi kama ukoma, kifafa kuna uwezekano mkubwa wa ndoa yenu kuvunjwa. Mwenza wako kama anaUKIMWI alafu wewe hauna, sio wazazi pekee watakayoivunja bali hata nyumba za ibada.

Mambo hayo ndio mambo makuu yanayoweza kukufanya ukataliwe UKWENI

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dodoma
 
Back
Top Bottom