Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Kwani uongozi ndiyo chanzo cha umasikini au watu?

Au wanaoongoza nchi sio watu wanaoamini dini?
Hata huko kwengine nako wapo wengi tu wenye kuongoza nchi na ni watu wanaoamini,ila hawaongozi nchi kwa kutumia nchi imani zao na sie ni hivyo hivyo hatutumii imani zetu kuongoza nchi zetu.

Kwahiyo wote kwa pamoja tunahusika kwenye shughuli za maendeleo uwe mtu wa imani au usiwe wa imani,kwahiyo kama ni masikini huo umasikini wetu una sababu zake zengine na sio imani.
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Kama una majibu mbadala wake unaweza kuwa una hoja, lakini kama unaishia kusema hakuna Mungu na husemi kuna nini badala yake, ni heri ukaamini kuwa Yupo kama anavyoelezewa kwenye biblia takatifu
Uwepo wa Mungu unadhihirishwa na uwepo wa vitu alivyoumba. Mfano watu, maumbile asili-miti ,milima
Hoja yako namba moja kuwa watu wataungua mabilioni ya miaka, ni hoja ya kimapokeo Zaidi haina ushahidi wa biblia. kama una ushahidi weka hapa
Hoja nyingine kuwa ni kwanini aliruhusu Adamu ajaribiwe
Ni kwamba Adamu aliumbwa akapewa utaratibu wa kuishi Eden ,kwamba aache nini na ale nini. Vinginevyo labda tulitakiwa tuongozwe kama roboti
 
Kwani uongozi ndiyo chanzo cha umasikini au watu?

Au wanaoongoza nchi sio watu wanaoamini dini?
Kuna Tajiri mmoja muarabu dar alikuwa na magari jumla 120...ila nlishangaa alivyokufa hakuondoka hata na spea tire..hata nguo zake walimvua wakamzika na nguo moja nyeupe amefungwa kama pipi.
Tukifa hakuna tunachootoka nacho zaidi ya mali na vitu visivyo shikika mfano wema, ubaya nk utajiri maendeleo huwa vitabaki kwa watu wa kizazi ulichoacha
Je ntakuwa sinaakili endapo ntajitajirisha kwa ajili ya maisha ya Mbele (life after death) au nijitajirishe kwa maisha ya hapa hapa nihangaike kufanya maendeleo ya kukimbizana kuingiariba na mikopo (dhambi) ili ninufaishe watu wa duniani ...yaani niwe mshumaa kama unavyoteketea but watu wanapata mwanga..aaah hapana ni uchiraru.
Bora umasikini wa duniani kuliko wa future life.
 
Hi members,

Kimsingi namchukia sana mungu kwa sababu ama maswali yafuatayo ambayo yanaacha utata.Niseme tu kwamba mm sio muumini wa dini yoyote na siamini katika chochote.

kitokea nimekutana na mungu leo hii nitamuuliza maswali haya.

1.Dear God wewe ni muweza wa yote ,je ilikuwaje ukatumia siku sita kuumba ulimwengu?.Kwa maana ungeweza kuviweka vitu vyote mahala pake hata kwa sekunde moja maana wewe ni muweza wa yote.Kutumia siku sita inamaanisha kwamba ulikuwa unafikiri nini kifuate/nini cha kuumba.
Na kwa maana hiyo kuna source nyingine inayokuoa uwezo wa kufikiria(maana mungu wewe huhitaji kufikiria.Lakini Baba hivi ilikuwaje ukaamua kuumba?Wazo hilo ulitoa wapi?Na kwa nini hivi vitu havikuanza mara moja na wewe yaani vikatokea na wewe mwanzo kabisa.

Mungu lakini pia kila ulipokuwa unamaliza kuumba ulikuwa unakiona ulichoumba kwamba ni chema,je hukujua kabla kwamba kitakuwa chema.Wewe ni mungu kweli?
Pia baba ulisema hapo mwanzo roho yako ilikuwa inaranda randa kwenye vilindi vya maji je hayo maji ni tofauti na yale uliyokuja kuyaumba?au uliumba kabla.Na kwanini roho yako n k
?haikua na mahala pa kutulia?

Halafu baba Ilikuwaje ukaumba maji yasiyo na oksjeni?.maana oksjeni umeiumba ulipomuumba mtu(Adam)huku ukiwa tayar ushaumba maji,hayo maji yalikuwaje.Halafu baba ilikuwaje baada ya uumbaji ukapumzika ?.Kwani mungu unahitaji kupumzika?Huwa unachoka kumbe?au wanatudanganya tu wala hukupumzika?

2.Dear God,Tunajua kwamba binadamu na kila kiumbe vimeumbwa wewe ,je inakuwaje mtu anazaliwa bila miguu ama mikono ama mlemavu (hasikii,haoni,bubu n.k).Je huwa unakosea ama?Kule japani watu mpka leo wanazaliwa hawana baadhi ya viungo ,sisi tunasema ni kutokana na athari za mabomu yake ya nagasaki na yeroshima baba we unasemaje ?

Je ni kweli bado unaendelea kuumba mpaka sasa ama umesitisha?.Je Swala la wanadamu kutahiriwa ikiwa ni moja ya maagizo yako unalichukuliaje?Kwa nn hukutumba tukiwa tumetahiriwa?.Je hayo ni mapungufu ya uumbaji?
Je mungu swala Appendix unaliongeaje kwenye mafundisho yako?.Isingekuwa juhudi zetu sisi wanadam kugundua operation ingekuwaje?.Je baba ukoma bado ni laana kama kitabu chako(biblia) kinavosema?

3.Dear God,Hivi ni kweli ulituumba ili tukuabudu,tukutukuze?na mwisho tuje kwako mbinguni?.Mungu wewe ni mpenda sifa kama sisi?.Je wewe sio muweza na mwenye nguvu zote?.Unafaidika nini kwa ibada zetu na nyimbo tunazokuimbia?Mungu kwani unahitaji sifa zetu?

4.Dear god,ni kweli siku ya mwisho umepanga kuchoma watu moto.?Et kwa sababu hawakutenda mema?Kwani baba mungu hukujua kwamba hawatatenda mema?We si naskia unatujua hata kabla hujatuumba?.

5.Dear god,Hivi ilikuwaje ukamtuma yesu mwanao wa pekee(ambaye pia naskia ni wewe ila katika nafsi ya pili)aje duniani kuteseka na kupigwa vile?.kwani hukujua yatamtokea yale?.Halafu naomba kuuliza hivi sababu ya yeye kuja hasa ni ipi?.Dhambi gani katuondolea?.Mbona bado dhambi zipo na watu ndo wanazidi kukukimbia.Halafu mbona kitendo kile kama hakieleweki yaani akaja kutuokoa kutoka katika adhabu yako ya moto lakini wakati huohuo unayechoma moto ni wewe huyohuyo halafu ni wewe huyo huyo uliyekuja katika nafsi ya pili,(YOU CAME IN YOURSELF IN ODER TO SAVE US FROM YOURSELF.

6.Dear god,katika amri zako ulizompa mosses kuna ile inasema usiue!.Lakini mbona mosses ulimwamuru aue kila kitu on the way back to the promised land?.Hadi watoto wazee mifugo,walikuwa na kosa gani baba?.Kwa nini hao waisrael wasingeamka tu wakute wako Kwao we si muweza wa yote?.Halafu zile amri mbona kama ziko outdated?kwa mfano ile ya kutamani na kuzini,Wewe umetuumba na kutufanya tupevuke tukiwa around 12-15yrz Halafu unasema tusitamani wala kuzini hadi tuoe ama kuolewa hivi changamoto za mtaani unazijua baba?Ikiwa nitaamua kuo nikiwa na 35 yrz muda woote huo nisizini?.si nitapiga puli kitu ambacho ni kibaya pia.

7.Dear god ,kwani wewe unajipambanua katika kitabu kipi hasa?.Maana vipo vingi sana na dini zaidi ya mia.Tukufuate wapi hasa?.Baba mungu kwani wewe ndo huyo huyo ALLAH? Mbona kule unakuwa na hasira sana lakini huku pengine hata bia poa tu ila usilewe.Kwani baba una double standard ?Hivi ni kweli wale wanajilipua kwenye kadamnasi wanakujaga kwako?.Baba hivi wali mabudha wa india wote utawachoma moto?maana wanaabudu ng'ombe ama hujastukia?

8.Dear god Hivi watoto wadogo wachanga kabisa kwa nini wanakufa hata hawajaona jua?Halafu huwa wanaenda wapi vile?Kwan baba wanakosa gani wale au ni ile dhambi ya asili?
Lakini kwa nini watoto wafe na wewe upo kwa nini huwalindi angalau wafikie miama kadhaa.

9.Dea god,Ile freewill unayosema kwenye vitabu vyako kwamba umetupa tuchague baya na jema una uhakika kwamba ulitupa?.Binafsi ungenipa freewill ningeomba kutokuumbwa kabisa kwa nini unaniumba bila ridhaa yangu halafu unichome moto et kwa sababu ya shetani?

Maana nabebeshwa mizigo ambayo hata siijui na wala sikuwepo..Mfano baba DHAMBI ya asili inanihusu nini mimi na wala sikuwepo?.Kwa nini hukumalizana nao hao wakina Eva na Adam,yaani kosa lao mpaka leo tunasafa.Halafu baba kwa nn hukuwasamehe ?Mbona wewe unasisitiza msamaha saba mara sabini?.Wewe kosa moja ukawahukumu mazima.Lakini hata hivyo baba si ulijua kabisa kwamba watakosa ?mbona uliwahukumu?.

10.Dear god,Baba hivi ni kweli shetani amekushinda?Huyu si kiumbe wako?.Si ulimuumba wewe sasa mbona mnatufanyia hivi.Wote hamuonekani mmetuacha tunafarakana.Kwani si umuue kabisa atoke hapa ulimwenguni?.Ama na wewe unafurahia anavotupelekea kutenda maovu.Lakini baba ilikuwaje shetani akaasi ?.Lile wazo la kuasi alitoa wapii maana hakukuwa na shetani kabla

11.Dear god hivi wanyama nao wana roho?.Hivi wakifa roho zao zinaenda wapi?.Hivi na wenyewe watafufuliwa siku ya mwisho au nn sisi tu na kwa nn?.Mbona unanifanya niamini kwamba HAUPO na hiz ni theory tu na uoga wetu.?
Je wanyama watachomwa moto?.

12.Dear god Ukishatuchoma moto sisi wakosefu utafaidika na nini?.Je kuna maisha baada ya moto maana navojua adhabu lengo lake ni kufundisha mtu asifanye tena kosa hilo!.Sasa mbona hujasema kama kuna maisha baada ya moto?

13.Dear god sasa ni miaka 10,000 tangu uumbe dunia(japo sio kweli maana hakuna ushahidi kwa kuwa carbon 14 inatuambia dunia imefanyika miaka 13.7 bilions ago.) niaje hakuna tena miracles ?kwa nini matukio ya miujiza hakuna tena kulikoni.Mbona sanamu hazitoe tena machozi?Mama mariam mbona hawatokei watu tena kama kule safina?,ingekuwa vizuri atokee saiv watu tupige ma selfie tutupie fb baba kuweka kumbukumbu sawa.Ama zilikuwaga ni KIK?
Mi nadhani wakati huu ndo muafaka maana tuna satellite na cameras tunaweza tukapiga picha tukatupiana fb ama watsapp ili kuamini zaidi.Lakini cha ajabu hakuna tena baba.Baba sikuizi mtu akisema umemtokea ama sijuia mwanao kamtokea tunaenda kumpima akili Milembe maana tunajua amechizi

Baba maswali ni mengi ila kwa leo ni hayo tu.

............Free ideas..........
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Kweli shetani hakosi wafuasi,,

yaani kuna watu wametoa like za kutosha,, kutia nguvu uzi huu uliojaa dhihaka mbele ya MUUMBA WA MBINGU NA RADHI NA VILIVYOMO..

kweli dunia haishiwi maajabu.
 
Point yako ya msingi nlio note ni moja "Je, Watu wanamwabudu Mungu kwa kupenda kufanya ivyo Au wanamwabudu kwasabab wanaogopa ule MOTO wa milele
.
.
I'm sure Wengi wetu tunaogopa ule Moto thats why wengi wanampinga mtoa mada
 
Kweli shetani hakosi wafuasi,,

yaani kuna watu wametoa like za kutosha,, kutia nguvu uzi huu uliojaa dhihaka mbele ya MUUMBA WA MBINGU NA RADHI NA VILIVYOMO..

kweli dunia haishiwi maajabu.
Usifadhaike, hao wanaitwa Atheists, hawajawahi kujua chochote Kuhusu Mungu, wapo wengi sana.
Hawajawahi kutambulishwa kwa Mungu wala kuona uwepo wake wala nguvu zake.
Wala hawahitaji kumtafuta, wala kukubali kuelezwa na kutafititi ukweli huo bila kuegemea upande wao.
Ni Atheism.
 
Usifadhaike, hao wanaitwa Atheists, hawajawahi kujua chochote Kuhusu Mungu, wapo wengi sana.
Hawajawahi kutambulishwa kwa Mungu wala kuona uwepo wake wala nguvu zake.
Wala hawahitaji kumtafuta, wala kukubali kuelezwa na kutafititi ukweli huo bila kuegemea upande wao.
Ni Atheism.
Duu!! Aisee!!
 
Yani dunia bn,jamaa kaongea point japo kosa lake moja kumchukia mungu. Maswali anayo jihoji ni maswali ambayo kama haujawahi kujiuliza basi kuna mengine kama hayo ushajiuliza kuhusu mungu, na kama haujawahi jiuliza chochote kuhusu mungu ukakosa majibu basi bado utakuwa mchanga ( mtoto). Kujiuliza sio kukufuru nikuitafta Suruhu na usahihi wa swali linalo kutatiza.

Kinacho tuponza watu wengi ni kuwa tumeambiwa na watumishi wa mungu tuamini pasipo kuhoji, kwakusingizia kumkosea mungu.
comment nyingi mnamtisha halafu mnajifanya nyie wema, najiuliza kwa wema upi kama mmeshindwa kuleta vifungu na kumweka kwenye mstali. mngekuwa wema kwanini msimuelekeze mkamtoa kwenye maana zake mbaya na kumukosoa kwa kumpatia neno na ushahidi wa vifungu vya manene ya mungu. hakika nyie ndo mtaenda motoni. yaani unamuona mtu anamkosea mungu na unajua halafu unazidi kumpoteza zaidi halafu unambie utapona.

ndugu mtoa mada, maswali unayo jiuliza hauko peke yako. watu wengi tushajiuliza tukakosa majibu. tukajaribu kuuliza watu wakatupa majibu yasiyo ya maswali tuliyo uliza. majibu yao ni kuwa unakufuru mungu

Usikute hawajua hata maana ya kukufuru. Neno kufuru limeandikwa mala 33 kwenye biblia mala 13 kwenye agano la kale na mala 20 kwenye agano jipya.

Nini maana ya kufuru.
KUFURU; ni kitendo au kosa la kusema vibaya juu ya Mungu au vitu vitakatifu; mazungumzo mabaya. (the action or offence of speaking sacrilegiously about God or sacred things; profane talk.)

Na biblia inasema nini kuhusu kufuru:
Mathayo 12:31 Kwa sababu hiyo na waambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
Marko 3:28-29.

Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;

bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
Biblia inatuambia ukimkufuru mungu hauna msamaha milele. Angepatikana mtu wa dini kuielezea kuwa ni kwa anayejua au na asiye jua.

mimi naomba kukujibu lakini nijibu swali moja kwanza UNAAMINI KAMA MUNGU YUPO? kama hauamini jibu SIAMINI, kama una amini weka na majibu ya kwanini unaamini yupo? then majibu yako yataleta mwanga wa maswali yako unayo juliza.
 
Mungu hayupo so point zako ni invalid.

Kama yupo basi anavyosema ni mwenye rehema na upendo kuliko binadamu yeyote anatudanganya maana angekua nao dunia isingekua kwenye mess hii.

Ana paradox nyingi mno kiasi kwamba his own existence can't be possible in anyway. Anasema anajua yote yatakayokuja na yaliyokuwepo,hehe meaning story ya adam n eve ka ni kweli then anamlaumu eve bure tu maana yeye alijua wazi watakachokifanya na bado akaweka mti pale, kosa ni la kwake 100% ni sawa na mzazi kujua mtoto ukimpa wembe atajikata alafu unampa then anajikata unamtupia lawama na kumuongezea adhabu juu.

Siku nilipoachana na fix za dini akili ilifunguka, kuishi kwa uoga uoga tena hakuna, mtoto ukimjaza kitu utotoni anakishika kama kilivyo, acheni watoto wenu wakue then wachague, hamtobaki na mtu anayeamimi haya maduduwasha
POINT TUPU 100%
 
Kweli shetani hakosi wafuasi,,

yaani kuna watu wametoa like za kutosha,, kutia nguvu uzi huu uliojaa dhihaka mbele ya MUUMBA WA MBINGU NA RADHI NA VILIVYOMO..

kweli dunia haishiwi maajabu.

Kwanini unamwabudu Mungu? Unaogopa usiende motoni au una sababu gani ya kumwabudu?
 
Kwanini unamwabudu Mungu? Unaogopa usiende motoni au una sababu gani ya kumwabudu?
Namwabudu Mungu sababu yeye ndy mmiliki wa mbingu na ardhi..

Yeye ndy mmiliki wa pumzi na uhai huo unaokufanya ujione wewe ndy kila kitu hapa duniani.
 
Dini ni bangi ya kale iliyobuniwa na wenye akili iliyotumika kuwachanganya wanadamu wenye akili ndogo ili watawalike vizuri,
Hadith za Mungu na shetani zilitengenezwa,kubuniwa na wayunani wa kale,wayahudi wakazifanya dogmas na kuziweka kwenye vitabu na kufrem dini yao kama muongozo wa maisha yao,!


Povu liwe la buku jero wafia dini,
povu la laki mbili sina mabeseni ya kuhifadhia!
 
Tangu nimekua na akili sijawahi kusikia mtu akisema amemuona malaika (kwenye mazingira niliyokuli
 
Hata nchi tajiri sana duniani bado raia wake wengi ni wafuasi wa dini.
Mkuu wapi nimesema nafuata mkumbo?
Na huo mkumbo namfuata nani?
Na umejuaje mimi nafuata mkumbo?

Mimi nimetumia akili kusema dini ni moja ya chanzo cha umasikini africa na wewe tumia akili zako kupinga kwa hoja kwamba dini sio chanzo cha umasikini africa.
Sasa wewe badala ya kutumia akili yako kugundua kwanini nimesema dini ni chanzo cha umasikini africa still unamuuliza huyo uliyemuita mjinga kwamba unapata wapi ujinga wa kusema dini ni chanzo cha umasikini africa.
Sasa jiulize kati ya mimi na wewe nani hajatumia akili na nani mjinga.

Na hapo ndipo tutakapothibitisha kwamba dini ni chanzo cha umasikini africa sababu hata wewe umeshindwa kutumia akili yako zaidi ya kuendeshwa na ulichofundishwa kwenye dini kunijibu ulichoandika.


Sasa nijibu.

Dini zimefikaje africa?

Prove dini ipo kila kona ya galaxy..?

Na umejuaje dini ipo kila kona ya galaxy?

Na prove uwepo wa galaxy..

Dini inawafundisha kutukana watu?

Mimi nasema Ndio dini ni chanzo cha umasikini africa.

Sasa pinga kwa hoja na sio matusi na ujibu maswali yote niliyokuuliza.
 
Back
Top Bottom