mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 284
- 232
Wakati mmoja humu tutakuja kuzungumza kuhusu Ufahamu Kristu na Ujazi...mose I think you would like to see this ✌️
Kuna vitu havifahamiki kwa watu wengi angali hawa wakidhani 'wanajua'. Hii ni kwa kuwa maarifa kwa mambo ya kiroho ya ukweli 'yalishadukuliwa' ili kutengeneza kile tunachoweza kukisema: 'Njia iionekanayo ni njema sana katika mtu na hali ya umauti'...
Dini nyingi za duniani na labda zote tu-- ni 'sayansi jamii' zilijitukiza kulingana na viumbe watu wa kigeni wenye nia njema ama isiyonjema kuiingilia maisha ya watu hapa duniani kupitia 'vichwa vya manabii'.
Uzi huu : Kusafiri Kiwakati 101...--unaelekea kuja kuonesha ushahidi kwa hili kadri utavyokuja hata kurefuka siku zijazo.
Unahitaji kukomaa kiakili na kiroho ili uweze kujikwamua na usadikifu pofu wa kimakundi. Ukibarikiwa, siku moja waweze kuuishi kama mtu huru... Hauhitaji kujinasibu na dini hii ama ile, ufuasi kwa hili ama lile -- lenye kuja kwa makusudi ya kibinadamu mwenye kuamini anaishi katika ulimwengu wa vikomo...
Kuna mengi tu katika 'vitabu vya injili' yenye uwalakini wa tafsiri na kumbukumbu kwa maisha, maneno na matendo ya Yesu, kwa mfano.
Wengi wanadhani 'wanamjua' na 'kumpenda Yesu' na hali katika ukweli wa jambo ni kuwa Yesu wanayejishirikishia ni 'roho ingine'--japo siku, tukibarikiwa tutamulika ni namna gani wanavyokuwa 'wanaamini' na kufuga fikra huwa wanahuluku 'viumbe majini'... Natumia neno 'majini' lakini siku za mbele tutatubuni neno sahihi kwa jambo hili. Vitu vyote watu wanavyotengenezea hisia na fikra juu wazo, wanaumba. Hili linafanania na mithali isemayo: zimwi likujualo, halikuli likakwisha... Mtu yeyote anayeumba kitu na kukipa nguvu kwa akili na hisia zake, anaishi 'kunyonywa damu' na hicho...
Tutakukapokuwa tukitafuta kujua kilicho ni hasa, wengi wetu watajukuta inawabidi wapambane na 'majini' yao yenyewe... Wengi wanaojihusisha na ukristo kama dini siajabu watajikuta inawapasa 'kutengeneza amani na Yesu'... Kwa kuwa itaanza kuwa wazi kwao, kuna mengi wamefikiri ni ya Yesu na hali ilikuwa ni muakisiko wa hofu, madhaifu na utegemezi kwa 'mwokozi'...
Yesu halisi, katika wakati na umahala huu, ni 'roho ya ufahamu' si 'nafsi' hasa... Na katikati ya nasibu ya hivi viwili ni namna 'umaizi wa dhahania ya ukuwa na kuwa' katika yule anayenasibika kung'amua mafumbo ya uzima.
Sasa, kuna vitu ambavyo utapata kuvisikia ama kusema umevisoma kuhusu maneno aliyopata kuyasema Yesu, alipokuwa akiishi kama mtu, kwa kukosa kitovu kimoja na 'ufahamu kristu' vinapelekea tafsiri 'isiyo na msaada' juu ya ukweli wa mambo. Labda 'itadukuliwa' kunyonya damu fikra na hisia za udhaifu na mapungufu ya kisaikia.
Huu uzi unazungumzia 'sababu za kubakia maskini'...
Ujazi ni neno ambalo ufahamu wa Kristo ukiaanza kufanyika katika wewe unang'amua kuwa kuishi si ulemavu--Roho ya Kristu hutufikia ili tuwe na ujazi...
Ujazi ni sifa na hali kuwa ama kupata kile unachostahili kuwanacho pale wakati hasa unapokuwa wakihitaji... Na kuishi katika hali ya neema ni sala. Ni namna ya kuishi ambayo utashuhudia wapata kile ambacho chakufaa pale inapofaa...
Yesu alifundisha siri ya hili. Na wakati mmoja, nitafunua lugha ya alama iliyomo katika 'Sala ya Bwana'... Kwa hivi, usiishi kutegemea mtu aliye hai ama mfu, mganga, mpiga ramli, malaika ama hata 'mungu' kwa maneno ya ulimi ama fikara... Kwa kuwa sala ya maneno, labda ni ufunguo tu. Usipoishi kung'amua ukweli wa jambo utaangukia katika kuumba 'majini' yako...
Yesu aliposema yeye ni mungu, si jambo la kujitenga. Ufahamu Kristu katika wewe utakudhahirishia wewe ni mungu pia. Sisi wote ni Mungu. Lakini tumejisahau... Labda twahitaji kukumbushwa halafu tufanye hima 'Kujikumbuka'...
Kutupa fikara la mungu kwa watu wengi 'ni mtihani'. Hii ni kwa kuwa mizizi ya fikara la namna hii imekomaa sana katika saikia watu--hasa wale wenye kujinasibu na usadikifu pofu wa kimakundi... Mungu hana budi kufutiliwa mbali katika saikia za watu ili neema ya kweli na ufunuo vimfikie mtu. Kweli ndicho kinachomuweka mtu huru kwelikweli...
Na huku ndiko kuzungumzia liberiti... Akina Jefferson kule Amerika walikusudia kuasisi Taifa ambalo Liberiti itakuwa ni mbadala wa utumwa wa dini na misingi ya mtu kujichagualia... Lakini Jefferson alikuwa ni mjumbe wa Waashihuru. Hawa wanazofunguo nyingi kuhusu mtu na 'Mungu' kwa mapokeo ya kiarifu yaani ginosia. Wao kwa mfano, walitaka kijenga taifa ambalo watu wataishi, kustawi na kuitafuta furaha... Japo 'walimtanguliza Mungu' ile ilikuwa ni lugha ya alama tu... Mungu kama 'Jicho lenye kuona kote'. Sasa jicho hili lipo ndani ya kila mtu... Hili ndilo hasa Yesu alipata kulizungumza kufanyika pale mtu afanyapo macho yake mawili kuwa jicho moja....
Tukibarikiwa nafasi nitafunua namna gani jicho hili ndicho kiini kwa maada yote, unafasishi, wakati na nishati. Kubaini mambo yenye kupitiliza mwonekano wa nje wahitaji dhahania ya vipeo vya ukomo. Kihisabati huendana dhahania za 1 na 0 na pia matendo × x ÷ - . Hili nitakuja kubayanisha kadri tutakavyokuwa tukimulika sayansi ya maumbo na ukomo wa vina vya tafsiri akilini.
Hmmm