SoC01 Sababu zinachangia kufa kwa biashara za vijana wengi

Stories of Change - 2021 Competition

Neema Fidelis

New Member
Jul 16, 2021
1
13
Utangulizi
Binafsi nafurahi kuona vijana wengi wakike na wakiume wakijiongeza kiuchumi kwa kujiunga na ujasiriamali. Wameichagua moja ya njia inayoweza kutumika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini. Japo sio wote watapendezwa na uthubutu na mafanikio yao lakini bila kujari kufahamiana wapo watu wanaotamani kuona vijana wanafanikiwa kutimiza ndoto zao. Lakini kitu cha kusikitisha unakuta biashara za vijana zinakufa kitu ambacho kinakatisha tamaa na kuleta maswali mengi kwamba kwanini biashara zinakufa badala ya kukua. Kwa upande wangu napenda kuwaona vijana wa jinsi zote wakisonga mbele hasa kiuchumi ila matamanio haya yanapotea Mana biashara zao hazikui kiasi kwamba hata wao kukua kiuchumi inakua kama ndoto. Katika tafiti zangu nimegundua baadhi ya sababu ambazo kwa namna moja au nyingine zinachangia kuua biashara za vijana wengi nchini mwetu.
Sababu hizo ni Kama zifuatazo:

Kukosekana kwa sababu yenye mashiko ya kwanini wameanza biashara
Kitu imara hujengwa kwa msingi imara vivyo hivyo biashara imara inajengwa kwa msingi imara wa kwanini biashara hii na sio nyingine. Hiyo sababu yenye mashiko ndio itakuwa nguvu ya kukusogeza mbele pale ambapo nguvu itakosekana. Lakini unakuta vijana wengi wanaruka hii hatua na kuanza biashara kwa kukurupuka. Hawakai chini kujiuliza kwanini wafanye biashara ya kuuza chakula na sio kuuza mitumba. Na sababu za kufanya biashara Fulani zaweza kuwa nyingi labda mtu kaona ndoto zake ni kumiliki mgahawa mkubwa mbeleni kwa hiyo akifanya biashara ya kuuza maandazi, uji, au chakula chochote basi anajua yuko njiani kutimiza ndoto zake inamaana hata akikutana na dhoruba kwanza hazitamyumisha pili zitampa nguvu ya kuendelea mbele Zaidi mana atakuwa anajua anachotaka hapo mbeleni. Lakini kama mtu hana sababu basi kuanguka kwa biashara inakua rahisi mno mana hakuna nguvu ya ziada ya kumfanya aendelee mbele. Chukua mfano mtu kaanza biashara ya kuuza chai baada ya kusikia unaweza pata hata elfu ishirini kwa siku kupitia biashara hiyo, kwa hiyo pesa nyingi ndo sababu ya yeye kuanza biashara kwa hiyo akikuta mambo yako tofauti ni rahisi biashara yake kufa mana nguvu aliyoitegemea haipo imara tena.

Usimamizi mbovu
Usimamizi ni moja ya mambo muhimu katika kukuza biashara lakini watu wamekuwa hawachukulii uzito unaostahili. Labda mtu kafungua duka la bidhaa za nyumbani ameanza vizuri anashinda mwenyewe dukani, lakini baada ya muda mara akae mke wake, mdogo wake, mara watoto wake. Ina maana dukani kaweka usimamizi wa watu wenye malengo tofauti na yake, vipaumbele tofauti, matumizi tofauti na wasio na uchungu na biashara yake kwa hiyo hata biashara isipoenda vizuri wao hawajali na wakitumia pesa za mauzo bila utaratibu kwao ni sawa na wengine haswa watoto wanaweza acha duka bila muuzaji kwa muda labda kwa sababu ya michezo na mambo mengine ya kitoto kiasa kwamba ni rahisi kuibiwa pale dukani. Sisemi kwamba watoto wote au wake wote wana usimamizi mbovu lakini mara nyingi unakuta wanachangia kuharibu maendeleo ya biashara, kitu ambacho kinaiweka biashara kwenye msitari mwekundu na mpaka mhusika aje kushtuka biashara ina hali mbaya, mauzo hakuna na mwishowe inakufa.

Kukosa vipaumbele katika matumizi ya fedha
Hili inamaanisha mtu yuko katika kutafuta na kupambania ndoto zake lakini hajaweka vipaumbele katika matumizi ya fedha, kwamba pesa anazopata zitagawanyika kwa utaratibu upi. Sio kwamba huyu mtu hana malengo ambayo tulitegemea yamnyime usingizi lahasha anakua nayo labda ana lengo la kununua kiwanja ajenge nyumba. Lakini hajaweka utaratibu maalum ambao hata kama akitaka kutumia pesa vibaya kuna kitu kinamshtua kwamba huo sio utaratibu uliojiwekea. Kwa kukosa vipaumbele kwenye matumizi ya kipato ndo unakuta mwanamke anafanya biashara lakini mapato yake ananunua mawigi, nguo yani kipaumbele chake ni kuvaa na kupendeza na sio kukuza biashara yake. Au mwanaume anahonga pesa zote wala hawazi kuwekeza katika biashara yake Ili ikue Zaidi. Hivyo mwisho wa siku biashara haitasonga mbele mana hakuna uwekezaji unaofanyika kuhakikisha wigo wa kukua unaongezwa. Na watu wa namna hii hujaa malalamiko kwamba biashara mbaya, kipato hakitoshi au hata kuleta Imani mbaya katika biashara. Kumbe hawaribifu ni wao na matumizi yao mabovu yaliyokosa vipaumbele. Kwa hiyo kama biashara haiongezewi hatua mbele kwa uwekezaji madhubuti ni dhahiri haitasonga mbele na hatima yake ni kufa (labda mhusika akijitambua na kubadilika) wala sio kukua.

Kufanya biashara kwa mazoea
Hii inamaanisha mtu anakuwa anafanya biashara kwa namna ile ile iliyozoeleka. Haongezi thamani wala utofauti wowote katika biashara yake. Ni wazi sikuizi hakuna biashara mpya nyingi zilishakuwepo kwa hiyo ili mtu apate wateja inabidi aonyeshe utofauti lakini watu hawafanyi hivyo. Mfano; mtu anaanza kuuza maandazi katika eneo Fulani na wauzaji wengine katika eneo hilo labda wanauza maandazi ya ngano nyeupe hasa badala ya kujitofautisha ili kuvutia wateja (waje na wabaki kuwa wateja wake), anabaki kwenye ngano nyeupe wakati angeweza kujitofautisha kwa kutumia ngano nyeusi na ambapo angepata wateja wengi hasa wanaopenda vitu asilia au atumie ngano nyeupe lakini aweke nazi kwenye maandazi yake kuongeza ubora haswa radha. Kwa hiyo kama hatochagua kuwa tofauti kwa namna moja au nyingine basi atakosa umaajabu ambapo hatakua na wateja wengine kiasi kwamba mtu anaweza kata tamaa na kuamua kufunga biashara.

• Kuanza na kidogo sana

Kwa miaka mingi tumekuwa tukishauriwa kuanza biashara na mtaji mdogo ili kama dhoruba zitatokea zisituharibie kila kitu. Ni ushauri mzuri na umewasaidia wengi na utaendelea kusaidia. Lakini tatizo ni kwamba kuna watu wanatumia utaratibu huu vibaya na ni kwa sababu hawajauelewa vizuri. Yani mtu anaanza na kidogo sana mpaka hapati faida. Mfano: mtu anafungua biashara ya chipsi. Analipia pango na kununua vifaa vya biashara na ni wazi anakuwa kawekeza pesa nyingi. Lakini kwenye kazi yenyewe ya chipsi ananunua viazi lita nne/lita kumi na anategemea kurudisha faida. Huu ni utani kabisa yani faida haitotokea na uelekeo wa hii biashara ni mbaya. Kwasababu anategemea kurudisha fedha nyingi na faida lakini kaweka uwanda mdogo kuingiza hizo hela. kiasi cha kukatisha tamaa useme biashara haina faida lakini kumbe utaratibu ndo mbaya. Kwa hiyo tunashauri kununua vitu kwa uchache ambao unaleta faida labda kama ni chipsi basi viazi viwepo hata gunia, mafuta dumu kubwa kiasi vikiisha faida inakuwepo ya kueleweka itakayochangia kukuza biashara.

• Kukosa watu sahihi wa kuambatana nao.
Kuambatana na watu wenye mchango chanya kwenye yale tunayofanya bado ni changamoto kwa watu. Biashara imejaa kupanda na kushuka ambapo kama hutakuwa na watu sahihi basi kuanguka ni rahisi. Lakini pia biashara inahitaji ujuzi mwingi ambao njia moja wapo ya kuupata ni kupitia watu hawa sahihi. Ukiwa umepanda viwango kwenye biashara unahitaji nguvu zaidi kuendelea kupanda juu asa kama hujazungukwa na watu sahihi wakukupa muongozo na moyo kwamba inawezekana kupanda juu na unapandaje, inawezekana ukaishia ulipo au ukashuka chini pia. Au labda umeanguka na mauzo hayako vizuri watu sahihi ndo watakuvusha hapo ila kama uko na watu bora mradi watu ndo watakuvunja moyo kwamba tulishakwambia hutaweza acha kupoteza muda asa maneno kama haya bila kujitambua unataka nini au bila msaada wa nje mtu anaishia kupoteza mweleko na biashara inakufa.

• Kukosa elimu juu ya biashara husika

Kama ambavyo nyanja zingine zinavyohitaji ujuzi wa kutosha vivyo hivyo biashara inamhitaji muuzaji kuwa na ujuzi wa kutosha kuihusu. Na sio lazima iwe biashara kubwa ndo uhisi unahitaji maarifa hata biashara ya ususi inahitaji ujuzi wa kutosha. Ujuzi utasaidia kuifanya kazi kwa ufanisi na ubunifu mkubwa. Lakini watu hawajitoi kutafuta maarifa ya jinsi ya kufanya kazi zao vizuri mtu ana simu janja hata siku moja hajawahi ingia mtandaoni kujifunza jinsi wengine wanavofanya kazi. Au ajitoe kupata mafunzo ya biashara labda ya jinsi ya kuuza, itkupata wateja na mambo mengine. Mtu hajitoi tena ikiwa ya kulipia ndo hathubutu kabisa. Lakini katika biashara mtu inabidi uwekeze katika vingi ikiwemo ujuzi na maarifa na mtu akikosa ujuzi inachangia kuharibu maendeleo ya biashara. Mfano: mtu kafungua biashara ya kusuka wanawake lakini anajua baadhi ya mitindo tuu na ukute mitindo asiyoiweza ndio yenye wateja zaidi. Lakini hachukui hatua stahiki za kujifunza hiyo mitindo ili aongoze wateja zaidi. Mwisho wa siku anabaki kulalamika biashara ya kusuka haina pesa kumbe angejiongeza kuna utofauti angeuona katika biashara.

• Kuitegemea biashara moja kwa kila kitu

Hii inamaanisha kwamba mtu anakuwa anategemea pesa za mahitaji yake yote kutoka kwenye biashara moja tu. Kwamba apate pesa ya kodi, bili za umeme na maji, chakula, akiumwa, mavazi na vingine vingi kibaya Zaidi unakuta biashara bado changa. Kwa hiyo mwisho wa siku haiwezi kukua mana inaelemewa sana na itakufa kama mhusika hata shituka mapema.
Ili kuondokana na hali hii, inashauriwa kuwa na biashara mbadala itakayo kuhudumia ili biashara kuu iweze kukua. Mfano: huku kama una banda la kuuza maziwa ya mgando, unaweza ukauza na nguo pia ukatuma picha mtandaoni watu wakakuunga mkono na itakusaidia kumudu gharama za maisha na kukuza biashara kuu.

Kwa kuhitimisha niseme kwamba kuthubutu kufanya biashara haitoshi na haimaanishi uthubutu wako unatosha kukubakiza kwenye mfumo. Unahitajika kufanya kazi ya ziada ili kuendelea mbele na kwa hiyo nitoe rai vijana wenzangu tuwekeze katika kutafuta maarifa na ujuzi wa kibiashara. Siku izi vitabu vya biashara ni vingi na wanaofundisha biashara wako wengi tujiunge nao hata ikibidi kulipia pesa ili tuchote maarifa kwa faida yetu na biashara zetu. Lakini pia ili tukue kibiashara tuache sifa za kutaka kuonekana tunapambana peke yetu. Kwenye mafanikio hakuna mimi kuna sisi kwa hiyo ambatana na watu sahihi kuanzia kwenye mitandao ya kijamii mpaka kwenye maisha halisia ya kazi itakusaidia sana kupiga hatua kibiashara.

Asanteni.
 
Hii inamaanisha kwamba mtu anakuwa anategemea pesa za mahitaji yake yote kutoka kwenye biashara moja tu. Kwamba apate pesa ya kodi, bili za umeme na maji, chakula, akiumwa, mavazi na vingine vingi kibaya Zaidi unakuta biashara bado changa
Usimamizi mbovu
Usimamizi ni moja ya mambo muhimu katika kukuza biashara lakini watu wamekuwa hawachukulii uzito unaostahili

Kufanya biashara kwa mazoea
Hii inamaanisha mtu anakuwa anafanya biashara kwa namna ile ile iliyozoeleka
Hizo point ndio zinazofelisha wengi... hongera
 
Hiii ni zaidi ya degree jumbe imekolea sana shida kupata mitaji sasa ndio tatizo linaanzia hapo
 
Kwenye biashara ni kufanya kitu unachokipenda na unachokielewa, lakini usifanye kwa sababu kuna mtu umeona anafanya. Utafeli mapema. Asante sana kwa somo zuri kiongozi
 
Ishu nyingine ni kuiga kutoka kwa mwingine bila kujua changamoto zilizopo kwa biashara husika!!
 
Back
Top Bottom