Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Sharti la msingi katika mengi,la kujiunga na EAC ni Utawala bora na kuheshimu haki za binadamu.
South Sudan, baada kukosa sifa za msingi, alikubaliwa kujiunga na EAC baada ya ushawishi mkali kutoka kwa waasisi na hasa Tanzania iliopelekea kufumbiwa macho masharti mengi kwa ahadi kuwa hayo masharti yatatekelezwa hatua kwa hatua.
Somalia ambayo inasafiri bahari moja ila kwenye vyombo tofauti tu, maombi yake yalitupiliwa mbali hasa kutokana na shinikizo kutoka Kenya na Uganda. Kikwete alizidiwa nguvu(?)na kusalim amri.
Wachunguzi wa mambo wakiyatafakari na kuyaweka kwenye mizani, wanaona kuwa sababu zinzotolewa za kuminywa kwa Somalia kuwa mwanachama ni nyepesi mno. Wachunguzi wanafikiria kumpa uanachama Somalia ungeweza hata kupunguza uhasama na jirani yake Kenya ambayo ina raia wengi wenye asili ya Somalia. Lakini sababu kuu ni inayowanyima Somalia kupata uanachama ni Udini. Hili jambo ni baya sana na tena la aibu.
Inanikumbusha pia Serikali ya Tanzania inapowawekea mikwamo wakati Zanzibar inapotaka kuwa mwanachama halisi wa kujitegemea,bila ya kubaki kwenye kwapa ya Tanzania.
Serikali ya Zanzibar inahoji kuwa ilikuwa mwanzilishi wa EAC iliovunjika (?) na iliendelea kuwa hivyo ndani ya muungano na kulikuwa hakuna tatizo lolote.Iweje leo iwe tatizo? mbona Zanzibar inabaki kuwa mwanachama anayojitegemea wa "EA Challenge Cup ( Kagame)"
Zanzibar ilidai haki hiyo kutokana na ukweli kuwa mambo mengi yasiokuwa ya muungano yana jadiliwa ndani ya EAC, hivyo haipati uwakilishi stahiki. Kumbe kubanwa kule ni sawa na Somali na kwa sababu ambazo zinalingana?
Kwa vile South Sudan imeshindwa kabisa kutimiza masharti ya kuwa mwanachama, hatuoni sasa umefika wakati muafaka wa kuisimamisha uanachama mpaka hapo itakapoweza kutimiza masharti kikamilifu.
Tanzania ina nafasi kubwa ya kuzishawishi wanachama wengine, hasa tukitilia maanani kuwa Mwenyekiti wa EAC wakati huu ni Tanzania.