Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,312
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Bw. Ole Njorai amesema mambo ya msingi yaliyowafanya Wanigeria kumtosa Rais Goodluck ni
: 1) Ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Katika kila vijana 10 wanaohitimu masomo ya chuo kikuu ni vijana 4 tu wanaopata nafasi ya kuajiriwa.
2)Serikali kwa ujumla wake ilikuwa imejaa rushwa na kwa kiasi kikubwa ilishindwa kupiga vita rushwa.
3) Kuzorota kwa usalama. Sababu hizi zinashabihiana au kurandana kwa kiasi kikubwa na malalamiko ya watanzania wengi juu ya serikali ya CCM.
Kama ni rushwa imetamaraki kiasi cha wala rushwa wakikitisha chama chao "eti" majina yao yakikatwa patajimbika. Suala la Ukosefu wa ajira limekuwa haliwekewi mikakati thabiti ya kuliondoa zaidi ya vijana kushauriwa kufuga nyuki. Usalama wa raia na Mali zao umekuwa uzizorota kila uchwao.
Kila siku ni taarifa za majambazi kupora bunduki za polisi badala ya polisi kukamata majambazi. Ni wakati muafaka wa CCM kujitathimini vinginevyo wataishia kupiga propaganda zisizo na kichwa wala miguu. Ooooohhh Maalim Seif Kaishagombea mara Nyingi, Slaa ni padri.
Akitoa neno baada ya kutangazwa kushinda, Generali mstaafu na Rais mteule Bw. Bohali amesema "wanaijeria wameungana pamoja bila kujali huyu ni yoruba, ibo au vingine".
Ni hakika kwa kuchochwa na matatizo yanayowakabili watanzania wataungana bila kujali tofauti zao.