Sababu zilizo nifanya niache kumkubali Raisi Magufuli baada ya kuingia madarakani!

MWAKITWINO

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
227
121
Kwanza niseme ukweli kabla ya mh Raisi huyu kuingia madarakani mimi nilikuwa moja ya supporters wake wakuu, mara tu alipoingia madarakani na kuanza kuona mwenendo wake nikaamua kuto kuwa upande wake hata kidogo!

1) Sababu ya kwanza nilijiuliza hivi kama huyu jamaa ni mzalendo mbona hataki mifumo ya kuhoji? na anaiua kabisa mfano ofisi ya CAG. Je anataka tumuamini yeye tu? akainyima bajeti ofisi hii muhimu iliyo tusaidia kujua Richmond escrow epa mv bagamoyo etc.

Kiukweli huwezi kuwa na credibility ya kutaja wizi bila back up ya CAG maana yake ile ESCROW au EPA isinge kuwa na nguvu yoyote kama kusinge kuwa na taarifa za CAG nikaweka kiulizo??

2)Bunge live hataki mhh! Nikajiuliza bunge limetusaidia kukamata na kuwafahamu wezi wa Skendo zote za ufisadi yeye hataki liwe huru hata wewe jiulize mbwa anaekusaidia kukamata wezi unamchukiaje??? Yes mfano kafulila unamchukiaje kwa mfano??

3)Marafiki zake mhh! Mbona haendi Marekani? Mbona haendi uingereza au sweden ambao hata bajeti zetu wanachangia??

MY TAKE
Raisi ni binadamu kama wengine na tumeshuhudia viongozi wakubwa duniani tena kwenye nchi kubwa wakifanya madudu sasa kama mifumo haitakuwepo tutajuaje ikiwa atabadilika? Hizo ni chache tu wanajamvi nikaamua kuto kuwa suporter wake nisije kupata laana ya watoto wangu
 
Back
Top Bottom