Sababu za Wanawake na Wanaume 'Kujiachia' kingono; Je yako ni ipi?

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,855
4,786
Hapa ninaposema kujiachia sina maana kujiachia wakati wa faragha kufurahia tendo. Bali nazungumzia kujiachia kwa bahati mbaya ama makusudi na kutojali ama kuzingatia ni idadi ngapi ya watu unashirikiana nao iwe kwa siku, juma (wiki), mwezi ama hata mwaka.

Suala lililopo hapa (hasa kwa akina mama/dada) wengi hujiweka katika kundi la kutokujiachia ovyo. Kwako msomaji naomba tulia na jitafakari ukiwa mkweli kwa nafsi yako kama upo kundi hili la kujiachia.

Kujiachia kupo tofauti, kuna kujiachia unakuwa na mpenzi mmoja mmoja lakini hadumu zaidi ya miezi mitatu hivyo kukufanya uwe umelala na walau watu 4-6 kwa mwaka (hivo kama ulianza huo mchezo kaika umri wa miaka 17 na upo miaka 25 ina maana umeshawahi lala na wanaume si chini ya 25). Pia kuna kujiachia kwa kuchanganya wapenzi ama kutoka nje ya mahusiano ya mpenzi/mwenza wako. Huku kutoka kama ni kubadilisha kila siku huko nje ndiyo kujiachia kwenyewe na nafuu huwepo kwa yule ambaye ana-maintain mtu huyo anayetoka naye.

Hata hivyo tuangalie sababu ambazo hutufanya tujiachie ni zipi…


1. Kuwa na Mpenzi asiyemridhisha, inaweza tokea mtu ana mtu wake anampenda sana na wapo pamoja kama couple ila hatosheki kabisa wanapokuwa faraghani. Siku za mwanzo atajitahidi kuvumilia, ila inapotokea tayari starehe ya kutaka kufikishwa imemvaa, aweza jikuta akajiachia kwingine.

2. Kuwa na tamaa ya vitu hivyo kujiachia kwa kuhongwa kama namna ya kupata alicholenga. Hii ilikuwa sana kwa wanawake, ila tokana na kushuka kwa maadili kasi inaongezeka na kwa vijana wa kiume pia. Anaweza kuwa na mpenzi wake ama wapenzi wengi kwa ajili ya kuwa na machimbo tofauti ya kupata pesa ya kujikimu tamaa zake za vitu. Kwa vijana mara nyingi hutolewa na wamama maarufu kama Jimama.

3. Kuwa desperate sana na kutoweza ishi bila Mpenzi, kila anapoachika mara kishampata mwingine. Kuna kundi la watu hawawezi kabisa kuweka nafasi (gap) kubwa kati ya mpenzi wake ambaye kaachana naye na mpenzi mpya. Hii husababisha mhusika kujikuta yupo katika mahusiano na mtu ambaye hamfai na hivyo kuachika na kutafuta tena. Mwisho wa siku ndani ya mwaka wapenzi siyo chini ya 6.

4. Kuwa addicted kwa ngono (Hii ni wachache kwa wanawake na wengi wa wanaume) Huyu mtu anataka kufanya ngono mara kwa mara. Inapotokea mtu mpenzi wake hayupo atajitahidi kwa kila namna atafute mbadala ili kujiridhisha.

5. Kuwa tu na hulka ya Umalaya/Uhuni. Anakuwa kishazoea kuwa na wapenzi wengi… Hawezi kuwa na mpenzi mmoja, hawezi tulia katika mahusiano, kila siku kutafuta sababu za kuwa na mtu zaidi ya mmoja. Na huona kuwa hiyo ni part ya maisha yake na kuwa afanyalo ni sawa.

6. Ushawishi wa makundi. Inaweza kuwa kama mzaha na wengine wakadhani kuwa mtu mzima huwa na akili yake independent katika maamuzi. Kwa mtazamo wangu, makundi yanachangia sana kwa baadhi ya watu kujenga tabia ya kujiachia na kuona ni sawa hali awali asingeweza thubutu.

7. Ngono kuwa ndicho chanzo cha kipato cha kila siku, hii ni kwa wale ambao ngono hutumika siyo tu kwa starehe. Ngono huwa ni chanzo cha kipato… Makundi yametofautiana, kuna wale ambao ni wa hali ya juu na huchaji kwa bei za juu na pia kuna wale wa viwango vya chini na viwango vya chini pia wote tegemeana na maeneo wanayopatikana.

8. Kutojitambua na hivyo kuwa na huruma sana ya kumfanya kutoweza kabisa kukataa akiombwa tunda lake. Hii ni kwa wanawake ambao hawawezi kabisa kusema ‘NO’. Hata kama hamtaki huyo mtu yeye humuonea huruma na kuona ni kheri tu akamalizane naye akamsaidie haja zake.

9. Kuwa na kilevi katika maungo ya watu wawavutiao. Mfano kuna mwanaume akiona mwanamke mwenye makalio makubwa anachanganyikiwa kabisa na hujitahidi kwa kila namna ampate huyo mwanamke. Kama vile baadhi ya wanawake wanavyoweza changanyikiwa kabisa na kifua, sura ama hata sauti ya mwanaume to the extent atajitahidi kwa kila namna kuweka mazingira ya huyo mwanaume amtongoze ili atimize kiu yake.

Kwa wanaume zinaongezeka;

Kuongeza kujiamini (confidence) na Ufahari kuwa yeye ni mwanaume kamili na lijali – Cha kusikitisha hapa ni kuwa siyo wanaume wote ambao wanalala ovyo wana uwezo wa 6/6. Ila sababu mara nyingi wanawake tumejenga utamaduni wa kujificha hisia za kweli wakati wa tendo, wengi sababu ni wa kupita tu kwa huyu mwanaume humezea tu rohoni kwa uwezo wake mbovu katika uwanja huo wa faragha… Hasa kama ana pesa ndiyo kabisa!

Je sababu zako za kujiachia ni zipi?

Chanzo: NGONO: Wanawake na Wanaume tunapoamua ‘kujiachia’ na Madhara yake… | FikraPevu
 
Ngono si mbaya jamani ndiyo maana watu wazima wote tunafanya isipokua kwa wafia dini. Tuache kui-demonize as long as habakw mtu, mtu anafanya ngono salama basi, idadi ya ulio fanya nao sio ishu.
 
Mambo uliyoorodhesha could be true lakini ukweli ni kwamba Nyakati Zimekaribia Kufika Mwisho.

Iliandikwa: Wanawake watakosa aibu.
 
Wasichana wengi hujiachia sana na wanaume tofautitofaut kutafuta uzoefu maana vijana wa kileo wanataka wasichana mafundi kitandani bila kujali huo uzoefu unapatikanaje, hongereni dada zangu Wachagga mnalalamikiwa wachovu kitandani kumbe sababu ni ninyi sio Malaya, hamna uzoefu.
 
Kumrizisha mwanamke wa kileo lazima uwe na vitu viwili wewe mwanaume, 1)Uweze kumkaza vizuri msichana wako/mkeo.
2)Uweze kuhimili mahitaji yake yote yanayohusiana na pesa. Huna hivi vitu viwili, usijidanganye upo peke yako.
Hapa nilikuwa nazungumzia point yako no 1.
 
Mambo uliyoorodhesha could be true lakini ukweli ni kwamba Nyakati Zimekaribia Kufika Mwisho.

Iliandikwa: Wanawake watakosa aibu.
Unataka kusema ni wanawake pekee wanajiachia?
 
Mmh kwa upande wangu ni siri ya kambi siwezi kukutajia zote ila kuna chache hapo zimenigusa
 
Yaani unamkuta mtu mkubwaaaaa yupo uc.i anakata mauno, vikalio kavibana Kama skonzi, afu anapiga yowee anatoka maneno flani Kama anatambika, anasimamia ukucha macho yamemtoka, mi jasho kibao, mwingine ka kunja kama kilema hivi, wanatoaga sauti za ajabu...baadae ukiwaona unaweza usiamini...
 
Back
Top Bottom