Sababu za wanaume kutongoza kila mwanamke

Diana Bx

Member
Nov 19, 2015
17
3
Nashindwa kuelewa ni kwanini wanaume mnapenda kutongozaa kila mwanamke? Unakuta anakutongoza unamwambia mimi ni mke wa mtu lakini bado anang'ang'ania kukutongoza.

Badilikeni acheni hizo tabia mnakera sana.
 
Unapotongozwa ni ishara bado unalipa
hujazeeka sana

Unaonaje wanaume wakikuona wawe wanakupa tu shikamoo
halafu wanamtongoza shosti wako au housegirl wako?
utajisikiaje?

Vitu vingine ni baraka hujui tu......
 
mpo kwa ajili yetu sasa. kwani we lini mara ya mwisho kutongozwa?
 
Wengine wanafanya mazoezi ya kutongoza wasije wakasahau si unajua tena kuna kuachwa au kukimbiwa na mrembo
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini wanaume mnapenda kutongoz kila mwanamke? unakuta ankutongoza unamwambia mimi ni mke wa mtu lakin bado anang'ang'ania kukutongoza. Badilikeni acheni hizo tabia mnakera sana.

Is it possible kutongoza KILA mwanamke? Mfano kwa wanaoishi DSM au Mwanza yaani utongoze wanawake woote? Hata mtaani tu huwezi kutongoza wanawake wote. On the other hand msipotongozwa mnasema mnagundu, kaazi kweli kweli.
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini wanaume mnapenda kutongoz kila mwanamke? unakuta ankutongoza unamwambia mimi ni mke wa mtu lakin bado anang'ang'ania kukutongoza. Badilikeni acheni hizo tabia mnakera sana.
We nahisi hujakereka vizuri..Nwei Ukitaka usisumbuliwa we kaa kimya tu kwa kila unachoongeleshwa..that is the best way..Mtu hawezi kuongea peke yake..
 
We nahisi hujakereka vizuri..Nwei Ukitaka usisumbuliwa we kaa kimya tu kwa kila unachoongeleshwa..that is the best way..Mtu hawezi kuongea peke yake..

Hataki huku namba katoa na kila sms anaijinu fasta...
 
Ni njia ya kipumbavu ya kuonesha manhood yao. Kwamba asipokutongoza utamdharau
 
kwani kutongozwa dhambi cha msingi response yako ni nini baada ya mtongozo,kutongozwa uatatongozwa tuu mpaka pale itakapo onekana hufai kutongozeka sababu ya umri.kwani mimi nikukuona mara ya kwanza ukanivutia nitaota kama wewe ni mke wa mtu! na ukiona umemwabia kuwa wewe ni mke wa mtu bado anakufuata jua fika wewe mwenyewe utakuwa bado hujajiweka mzingira mbele yake ya kuonyesha kuwa wewe ni mke wa mtu kweli. nasema hivyo sababu wanaume wengi wana psychology kali sana juu ya mwanake
 
Back
Top Bottom