M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
I) POSITIVES
Tangu ameingia madarakani, tumeona mabadiliko kidogo sana yenye mwelekeo chanya. Nimetumia expression ya "kidogo sana" kwa vile si mambo yaliyohitaji kutumia effort kubwa sana kuyatekeleza bali yanahitaji self-restraint pamoja na busara ya kawaida tu ya kiuongozi.
1. Kutotumia lugha ya kijeuri, matusi, ubabe, vitisho na majigambo
2. Kukiri kuwa nchi ina hali tete kiuchumi na anahitaji kuinyanyua - of course kinyume na tambo za mtangulizi wake
3. Reconciliatory tone na private sector na investors
4. Kukiri uwepo wa COVID-19 na kuruhusu sayansi ichukue nafasi yake
II) NEGATIVES
1. Rais Samia ameendelea kuwakumbatia watendaji wakuu katika nafasi zote nyeti - hawa wote (angalia orodha hapa chini) aliwarithi kutoka kwa mtangulizi wake.
Ukiukwaji wa haki kwa baadhi ya Watanzania ulitokea right under their watch. Kuna kila dalili kuwa ukiukwaji huu umeshaanza kurejea tena (rejea dinner get together ya wamama wa Chadema hivi karibuni):
Pamoja na sasa kuamua kui tackle COVID-19 kisayansi, bado tumeshuhudia kauli zinazokinzana kutoka kwa Rais Samia. Alinukuliwa akiwataka Watanzania wajilinde na COVID-19 kwa kukwepa mikusanyiko isiyo ya lazima. Siku chache baadaye akanukuliwa akiwasifu vijana waliolundikana kwa wingi sehemu moja kwa starehe zao huku hawajachukua tahadhari yoyote ya kujikinga. Tukumbuke vijana hao waliokusanyika ndiyo wale wale waliokuwa wakitumiwa katika propaganda mbalimbali za mtangulizi wake.
III. TUTOKEJE HAPA?
Ili Rais Samia aache lasting legacy, inampasa afanye kitu kurejesha tabasamu lililopotea miongoni mwa Watanzania tangu awamu ya 5 ilivyoingia madarakani kwa kufanya yafuatayo:
1. Hatua ya kwanza ni kuwaondoa wahifidhina kwenye ranks za uongozi (serekalini na chamani)
2. Kinachofuata akutane na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ndani ya nchi - vyama vya siasa, taasisi zinazosimamia haki, jumuiya za wasomi, taasisi za dini, nk
3. Atangaze mchakato wa undikwaji wa katiba mpya. Tayari tunayo rasimu ya Warioba - tuanzie hapo. Ashirikiane na taasisi nilizozitaja hapo # 2 kuunda mfumo muafaka wa namna kuunda bunge la katiba kwa ajili ya kuipitia rasimu a Warioba
4. Aamuru mahubusu wote wa kisiasa waachiwe huru (ikiwamo kutangaza msamaha kwa waliofungwa kwa sababu hizo hizo)
5. Atamke hadharani usalama wa Watanzania waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa

- PM (huyu binafsi sitamsahau kwa kitendo chake cha kutosema ukweli - tena akiwa madhabahuni - kuhusu afya ya Magufuli. Alidai Magufuli haumwi ila yupo bize na mafaili!)
- IGP (polisi ni kama ndiyo walikuwa watendaji na wasemaji wakuu wa chama tawala)
- DGISS (tunaweza kumuita alikuwa ni pacha wake na IGP)
- Ndani ya bunge kuna wabunge ambao hawatambuliki kikatiba. Samia analijua hilo na repercussions zake kisheria, kiuchumi, kijamii na kisiasa lakini ka-mute tu
- Kisiasa, Rais Samia ameipa likizo katiba - tafsiri yake ni kwamba ameruhusu baadhi ya watu (akiwemo yeye mwenyewe kutumia fursa hiyo kufanya maamuzi yanayoweza kuwa yanakiuka sheria na watu kama IGP kama tulivyoshuhudia hivi karibuni polisi walivyokwenda kuwafanyia vurugu wamama wa Chadema kwenye dinner yao)