Sababu za waandishi kushindwa kuandamana nchi nzima: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za waandishi kushindwa kuandamana nchi nzima:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Don, Sep 12, 2012.

 1. The Don

  The Don JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 3,455
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Yale maandamano ya waandishi wa habari yaliyofanyika janakupinga mauaji ya mwandishi mwangosi na ukiukwaji wa haki za raia yanayofanywa na polisi yameshindwa kufikia malengo kwa baadhi ya mikoa na vyombo kutoshiriki,mf. Arusha,singida,moro na vituo kama TBC na Clouds Media,hii imetokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na polisi kukwamisha,vyama na waandishi wenyewe kutokuwa na mshikamano huku vingine vikiwa na ushabiki wa kisiasa na ukasuku wa kutetea ulaji na kibarua kisiote nyasi,mf. Mzuri waandishi wa arusha wameingia ktk mgogoro na chama chao kuonyesha kutokuwa na imani na chama husika.

  Note:waandishi acheni ukasuku kuweni na umoja kwani nyie ni mhimili wa nne wa serikali mnaweza kujenga na pia kubomoa
   
 2. K

  KINUKAMORI Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, waandishi ni sawa na jeshi, halina chama, hawatakiwi kuangalia mambo ya vyama kazi yao watoe habari kwa wananchi bila kujali wako katika itikadi za vyama gani na gani
   
 3. M

  Miruko Senior Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu mleta mada nadhani alitaka kuzungumzia vilabu vyao. lakini ninachojua mimi si mgawanyiko, kilichotokea ni polisi kuzuia kwa sababu mbalimbali. Arusha polisi wamesema ni ziara ya Kikwete, Rukwa, Mara wanasema maombi ya kibali yalichelewa, saa 48 hazikutosha na nyingine zinazofanana na hizo. Hata Dar, awali walizuia, lakini baadaye wakarudi into their senses, Kova akaoverrule RPC wa Ilala na kutoa Kibali. Huenda katika baadhi ya sehemu, mambo yalichelewa kutokana na mawasiliano, maaba si waandishi wote ni wajumbe wa Jukwaa la Wahariri lililoandaa maandamano. Klabu za mikoani zinaratibiwa na Muungano wa Vilabu Vya waandishi wa Habari (UTPC) ambalo pia si Mshirika wa Jukwaa. Hapo utaoana kwamba hakuna chombo kimoja, kinachoratibu waandishi wa habari, Kuna vyama tofauti, Jukwaa, MCT, UTPC, Tamwa, AJM, TAJA na vingine.
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sehemu yao kubwa ni tawi la chadema, ndo maana hata kwenye maandamano wilimkataa nchimbi-ccm wakamkumbatia na kumpa jukwaa lwaitama-chadema
  so biased and I hate them.
   
 5. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waandishi wa habari, walimu, askari polisi..
   
Loading...