Sababu za vyama vya upinzani kufanya vibaya kagera 2010 hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za vyama vya upinzani kufanya vibaya kagera 2010 hizi hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sembuli, Jun 26, 2012.

 1. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nimesoma post iliyotumwa jana na mwana jamii forum aitwae “omutwale”. akihimiza wana kagera kuamka na kuiga moto wa mabadiliko wa mageuzi na kuachana na ccm kama mikoa mingine ya kanda ya ziwa,na kutoa mfano wa matokeo ya uchaguzi uliofanyika majuzi shinyanga ambapo kati ya viti 11, CDM kimenyakua viti 7 na 'magamba' viti 4 tu. zifuatazo ni sababu zilizofanya ccm kushinda viti vingi kagera mwaka 2010.
  1. Kauli ya askofu KIRAINI kuwa 'JK ni chaguo la mungu. kutokana na wakazi wengi wa kagera kumuamini sana kiraini, waliweka hisia na utashi wao pembeni na kuamini unabii wa kiraini hivyo kuamua kuchagua 'UTATU' Yaani rais ccm, diwani ccm na mbunge gamba.
  2. njaa na ukame uliukumba mkoa wa kagera hasa kutokana na ugonjwa wa migomba, , palipo na njaa hata kushinda kishawishi cha kuuza shahada ya kuchagua mgombea kwa kupewa pesa si kazi rahisi. ikizingatiwa kuwa kushuka kwa bei ya kahawa kumefanya mkoa huo kuwa masikini kwa kukosa zao la biashara.
  3.vijana wengi kukimbilia mijini hivyo sehemu kubwa ya wapiga kura kuwa ni wazee
  ambao wengi wao wamekuwa wakichagua kwa kufuata CV kama prof, dr, engeneer nk badala ya utendaji.
  USHAURI:
  ' solve kiraini syndrome' ondoa njaa, peleka elimu ya uraia kwa wapiga kura kijijini, kukutana kwenu dar wakati wapiga kura mmewaacha kijijini haisaidii HATA MBEYA,SHINYANGA,MWANZA, ARUSHA ,KILIMANJARO NA kwingineko kwenye mageuzi hawakukaa vikao dar es salaam, ni moyo wa dhati na uthubutu ndio silaha. mliwahi kuthubutu mwanzoni kabisa ktk mageuzi enzi za kina wilfred lwakatare. mkiondoa hayo matatizo mageuzi yanawezekana!
   
 2. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu, naunga mkono!
   
 3. T

  Twigwe Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanahitaji elimu ya uraia na kusaidiwa kujua mwelekeo wa siasa za sasa za TZ.
   
 4. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Inawezekana unasema ukweli lakini sababu ulizotoa sio sahii kwa asilimia mia moja.Kauli ya Kilaini haikuwa na effect namna hiyo sababu kwa upande wa uraisi kama sikosei Dr Silaa alipata kura nyingi zaidi ya JK katika mkoa wa kagera.Kwa upeo wangu mdogo nadhani sababu ni kama ifuatavyo
  1.Kwa upande wa BK mjini mgombea wa CCM Balozi Kagasheki alipata kwa vile heti aliuletea mkoa heshima kwa mtoto wake kuoa mtoto wa raisi Mwinyi,pia title ya ubalozi na fact kwamba ukoo wake ni mkubwa sana vilichangia sana katika kumpa kura,pia anamiliki kiwanda cha kukoboa Kahawa hivyo kupata ushawishi wa wafanya biashara wakubwa wa Kahawa.Mgombea wa CHADEMA alijitahidi sana japo alizushiwa tuhuma kuwa katika matamshi yake aliwahi kutukana wapiga kura,tuhuma hiyo ilitumiwa vilivyo kama kete ya kisiasa.Pia kwa vile hapo awali alikuwa mbunge kwa kupitia CUF suala la udini ilitumiwa sana kummaliza na hivyo waislamu wengi kumpa kura mgombea wa CCM.Hongo ikiwemo screen kubwa waliyowekewa wakazi wa Bukoba mjini eneo la Uswahilini na mgombea wa CCM vilisaidia kumuongezea kura.
  2.CHADEMA kusimamisha wagombea ilimradi,hii ilichangia sana kukosa kura ,mfano mzuri ni Nkenge ambapo walimsimamisha DJ ambaye baadae alipewa vijisenti akampisha mgombea wa CCM.
  3.Ukweli kwamba wasomi wengi wa mkoa wa Kagera wanaishi uhamishoni na wachache waliobaki mkoani hawana exposure nzuri,ni wabinafsi na wakabila.Wengi wanachagua mtu kwa historia ya ukoo wake,mfano baba yake alikuwa mlangila,babu aliwahi kuserve kwa chief,baba yake mdogo ni diwani,au ukoo wao uliwahi kutoa ubunge etc.mbaya zaidi kwa watu wa mkoa huu wanaangalia vitu trivial kama nyumba yake inafananaje,je ni ya kujenga au kurithi,kwanini hajajenga etc ni vigumu sana kwa mgombea anayetoka familia ya kimaskini kupata nafasi katika mkoa huu.Pia makosa binafsi ambayo yaliwahi kufanywa na mwana ukoo wa mgombea pia nayo wakati mwingine yanaangaliwa.Kwa kifupi hakuna elimu ya uraia kabisa na watu wengi waliovijijini ni miyopic.
  3.Mgombea kama wa Bukoba vijijini alitumia shule yake ya binafsi ya sekondari iliyokuwa karibu kufunguliwa eneo la Kyetema kama mtaji wa kisiasa,ali take advantage ya kiu ya watu kupata elimu na umaskini na kuunda kauli mbiu ya ''OMWANA ASHOME'' maana yake acha watoto wasome,watu walikuwa na matumaini kuwa kama akichaguliwa basi watoto wao watasoma bure kwenye shule ya mgombea ama kwa ada nafuu sana kitu ambacho kilikuja kuonekana uongo baada ya mgombea kupita.
  4.Wilaya ya Ngara inaongoza kwa ignorance,kwao wana amini kuwa kuchagua upinzani ni kosa la jinai,wengi ni waoga na kwa wale walio wahi kuishi kwa karibu na watu wa wilaya hii mnaelewa ninachokisema ,wale wachache waliobahatika kusoma hawataki kabisa kurudi nyumbani.
  5.Kulikuwa na uchakachuaji wa hali ya juu wa matokeo ya wilaya ya Karagwe,huku watu ni waelewa sana,wanafanya biashara na wana safiri sana,exposure yao ni kubwa,hivyo nguvu ya ziada ilitumika kuhakikisha CCM wanashinda,ndio sababu hadi leo baadhi ya wabunge wa wilaya hii hawajawahi kukanyaga jimboni tangu uchaguzi umalizike,na kama wakija inabidi wawe na bodyguards.
  3.
   
 5. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red the vice versa is true. Ingawa sina uhakika sana na sababu zako ulizotoa.
   
 6. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,259
  Likes Received: 1,195
  Trophy Points: 280
  Yap,wenzetu wahaya,c ndo wajivunia kwa elim ss inakuwaje?get like
   
 7. 1

  19don JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  sisi wa kwetu tunaye 1 tu wale wanaotusingizia tuna mlinzi tukutane ipogolo au kihesa tuanze mchakato wa kuchukua majimbo yote ya kukaye
   
 8. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ni vizur lakin hujaonyesha hizo sababu so jipange vizuri katika headline.
   
Loading...