Sababu za vijana kushindwa kujitegemea

suwifred

Member
Jul 13, 2021
6
3
(Nyumbani kwa mzee Jingo sebuleni)
Mzee Jingo : Hivi Chuma utakaa nyumbani mpaka lini, kijana mwenye nguvu huna kazi unashinda vijiweni
Chuma : Mzee unatambua wazi kazi hamna nikipata kazi nitafanya
Mzee Jingo :Vijana siku hizi hamtaki kuwajibika unashindwa ata kulima !
Chuma : Sasa nilime nini? Siku hizi kilimo hakieleweki unapoteza nguvu bure.
Mzee Jingo :Hayo makaratasi yako ya kubashiri na kulima kipi bora
Chuma :Kubeti ajira mzee tena watu wanajenga kwa kubeti
Mzee Jingo : Huo ujinga ndio unakufanya hutaki vibarua, nani kafanikiwa kwa kubashiri?
Chuma :Wapo wengi
Mzee Jingo : Mimi niliondoka nyumbani nikiwa na miaka 16, sasa wewe miaka 30 unakaa kwangu!
Chuma : Lakini mzee muda umetoka kwenu ulikuwa unafanya nini.
Mzee Jingo : Vibarua vidogo vidogo.
Chuma : Leo hii mimi namaliza chuo na umri wa miaka 25 ndo nianze sifuri tunalingana kweli?
Mzee Jingo
: Mara ngap nakwambia twende shamba hutaki?
Chuma :Mzee mimi siwezi lima, muda nilioutumia shule leo niwe mkulima!
Mzee Jingo
:Kwa akili hizo vijana hamtajikwamua kiuchumi kabisa, fanya kazi bila kujali umri wa elimu yako Ilimradi ni halali ,maisha yamebadilika msibweteke na michezo ya kubashiri haitawasaidia kwa lolote utapoteza muda na pesa zako kuna siku wazazi wako hatutakuwepo iyabidi uwe mzazi ni nani atawajibika kwa ajili yako?
 
Makundi ya kudanganyana pia huchangiwa na elimu yetu haimuandai kijana kuwa mjasiriamali,ambao huenda sambamba pia na kilimo,ufugaji,biashara mbalimbali na kufanya kile wazazi wetu wanafanya nyumbani kabla au baada ya kustaafu.
 
Hata ukilima utauza wapi? Madalali na serikali ndio wanaamua bei. Hakuna watu maskini kama wakulima. Na mwaka huu bei ya mbolea na pembejeo imepanda mara mbili.
Yajayo yanahuzunisha sana.
 
Hata ukilima utauza wapi? Madalali na serikali ndio wanaamua bei. Hakuna watu maskini kama wakulima. Na mwaka huu bei ya mbolea na pembejeo imepanda mara mbili.
Yajayo yanahuzunisha sana.
Chuma umemaliza maongezi na mzee jingo sahiv umeshika smartphone yako eti ukilima utauza wapi
 
Back
Top Bottom