KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,589
- 4,600
Tukirudi nyuma kuanzia mwaka 2008-2015, upinzani Tanzania ulikuwa na mvuto kutoka kwa wananchi na wananchi walivutiwa sana na agenda za ufisadi na rushwa ambazo zilitamalaki kipindi hiko. Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo( CHADEMA) kikajizolea umaarufu na mvuto mkubwa kiasi kwamba kilikuwa kinatazamiwa kuwa tishio kwa CCM kwa chaguzi zijzo.
Kuanzia mwaka 2015 hasa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, CHADEMA waliua agenda zote za ufisadi na rushwa nchini kwa kipindi chote cha miezi mitatu ya kampeni. CHADEMA haikusikika hata mara moja ikizungumzia ufisadi na rushwa kuanzia timu ya kampeni ya CHADEMA taifa mpaka kwenye kata. Kitendo cha kuua agenda za ufisadi na rushwa, kwa sababu wanazozijua wao ndio ulikuwa ni mwanzo la kukosa mvuto kwa CHADEMA.
Hali ya kukosa mvuto ikaendelea kuleta matokeo hasi kwa CHADEMA na upinzani kwa ujumla hasa kushindwa kila uchaguzi pale unaposhiriki. Watanzania walihitaji kujua vyama vya siasa vitashiriki vipi katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Kitendo cha upinzani kuzunguka nchi nzima bila kuyazungumzia mambo hayo kiliwastaajabisha na kuwashangaza watanzania na watanzania kuanzia hapo wanakistaajabisha na kukishangaza Chama hiko kila uchaguzi.
Wote ni mashahidi, katika mapambano dhidi ya Rushwa na Ufisadi Rais Magufuli alipambana sana hata kabla ya kuwa Rais, kwenye kampeni zake 2015 alishiriki kwa namna kubwa na ya kutia moyo angalau kuonyesha hisia zake ni jinsi gani atashughulika nayo. Hii ikamuongezea mvuto sana na CCM ikazidi kuvutia kwa wananchi kiasi kwamba kila uchaguzi toka 2015 imekuwa ikiibuka kidedea.
Katika kuhahakisha CCM inapata mvuto na inashinda kila uchaguzi, Mwenyekiti wa CCM taifa Ndg. Dkt John Magufuli alihahakisha anaifanya CCM inakuwa mpya na huo ndio ukawa mwanzo wa CCM mpya. Hakika CCM mpya ni tishio la upinzani nchini. CCM mpya ndio sababu ya kukosa mvuto na kushindwa kwa upinzani kila uchaguzi. CCM mpya ndio chimbuko la vita mpya dhidi ya ufisadi na rushwa nchini, agenda zilizoipa mvuto upinzani. CCM mpya ndio kinara wa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa nchini. CCM mpya imeweka msingi mzuri wa hali ya kisiasa nchini. CCM mpya ndio zao la fikra mpya. CCM mpya ndio sababu ya Tanzania mpya.
CCM mpya imefanya upinzani kupoteza dira na mvuto kwa wananchi na kusababisha kushindwa kila uchaguzi. Watanzania wanaona matunda ya CCM mpya na wanashiriki uchaguzi wakiwa na matumaini na matarajio makubwa ya ushindi kwa CCM. Wapinzani wanapokuja na habari za kuonewa na wakurugenzi au tume ya uchaguzi, wanafanya watanzania wacheke tu. Watanzania wanaamini kuwa kwa CCM mpya hata Mbowe angekuwa ni mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC angesikia aibu kutomtangaza mwanaCCM kashinda.