Sababu za Sabaya kukifunga kiwanda cha Daren Fabrics Industries Ltd

ONGEEENI YOOOTEE ILA KUMBUKENI KUNA WATU FULANI WALIAMBIWAGA MAENDELEO YAO YAMETOSHA WASUBIRI WENGINE,WAKAPELEKEWA WATU KAMA KINA SABAYA,GAMBO,MNYETI,MURRO
KWA KIFUPI K NJARO N ARUSHA YALIYOKUWA YANAFANYWA NA SABAY NDIYO YALIVYOTAKIWA KU FRUSTRATE WATU WA KULE NA KUKIMBIZA HELA KABISA AND HE DID IT WELL
KULE KWA KIPPI WARIOBA VUNJO WALICHANGA BILIONI 2 YA KUJENGA KILOMITA TATU ZA LAMI,MKUU WA WILAYA ANAKAZANIA HELA APEWE YEYE WAKAKAZA ULIZA VIONGOZI WA HUO MCHAMGO MOTO WA TRA ULIOWAKUTA HADI HUKU DSM
ILIKUWA BALAA KUBWA SANA
Sasa wachaga mnafeli wapi nanyi
 
Sasa wachaga mnafeli wapi nanyi
watu wana uwezo wa kuchanga bilioni 2 kwa group la whatsapp kujenga kilomita 3 za lami unawaita wanafeli? bado kippi warioba akawa anawakataza wasijenge lami ? unajua kilichowakuta viongozi wa huo mchango?ila mwisho wa siku lami ilijengwa
 
watu wana uwezo wa kuchanga bilioni 2 kwa group la whatsapp kujenga kilomita 3 za lami unawaita wanafeli? bado kippi warioba akawa anawakataza wasijenge lami ? unajua kilichowakuta viongozi wa huo mchango?ila mwisho wa siku lami ilijengwa
Mnafeli wapi kuwashughulikia hao wahalifu mbona Mara Hakuna ujinga huo
 
Mnafeli wapi kuwashughulikia hao wahalifu mbona Mara Hakuna ujinga huo
watu walikimbizia hela zao nairobi kaka ila nasikia wameanza kurudisha hela, ni balaa huko kwa jerry muro ana hadi madeni ya flat screen inchi 52 kachukua dukani hataki malizia hela....yaani mwendazake alikuwa anapenda wahuni na vibaka sana
Halafu huko mara si ndo baba yake sabaya alikuwaga mkuu wailaya serengeti akachoma nyumba za kutosha? na kuna huyo wa Rorya odongo anawacharaza viboko?
 
Huyu wamtoe gerezani kisha wampeleke sokoni Wilayani Hai ili wananchi wenye hasira kali wadili naye.
Bure Wanapoteza raslimali za nchi kwenye mifumo ya kisheria
Hapana, Hao wananchi wataonyesha hasira kwa muda mfupi na hatopata majuto ya muda mrefu. Acha sheria ichukue mkondo wake, atapata mateso na majuto ya muda mrefu. Unajua kwa mfano ukumuua jambazi haraka, hakuna mateso anayopata ili akisota mahabusu miaka kadhaa na baadae akahukumiwa say kunyongwa (na hanyongwi) ni mateso sana
 
Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John.

Mwezi February mwaka huu, aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alimpigia Jeff na kumwambia kuwa CCM itafanya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuanzishwa, na yeye ni miongoni mwa wanakamati wanaoandaa maadhimisho hayo.

Akataka kiwanda hicho kichangie TZS 10M kufanikisha maadhimisho hayo. Jeff akamwambia hana uwezo wa kuchangia 10M, lakini akaahidi kuchangia 1M. Sabaya akamnanga kwamba serikali ya CCM ndiyo iliyomuwekea mazingira mazuri ya kibiashara hadi akaweza kufungua kiwanda, kwahiyo kuchangia 1M ni dharau kwa chama, anatakiwa achangie kiasi kisichopungua 10M.

Jeff akamwambia hana pesa hiyo. Sabaya akamwambia nimepitia transaction zako TRA najua unafanya mauzo ya mamilioni ya shilingi. Jeff akamwambia bado kiwanda ni kichanga na hakijaanza kujiendesha kwa faida kiasi cha kumpa Sabaya 10M.

Mwezi May mwaka huu Sabaya akavamia kiwanda hicho akiwa na mabaunsa wake. Wakawa-harass sana wafanyakazi waliokuwepo. Sabaya akiongozana na waandishi wa vyombo 11 vya habari akatangaza kukifunga kiwanda hicho kwa madai kinajiendesha bila vibali.

Vyombo vya habari vikaripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa kwa kufanya uzalishaji wa vinywaji vikali bila kuwa na kibali. Jeff akashangaa kwa sababu alikua na vibali vyote.

Ana leseni ya BRELA nambari 142255766 iliyotolewa July mwaka 2020. Ana leseni ya TRA nambari 142255766 iliyolewa July 2020. Ana leseni ya biashara nambari 03356294 iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Hai tarehe 25 September 2020.

Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.

Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.

Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.

Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.

Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.

Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.

Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.

Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?

Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa!
Bora sabaya alivyokifunga hicho kiwanda. Eti faru john..nyie wamangi biashara yenu pombe tu ngoja kama wote hamjakua kama warombo. Tutahamia kukamata something zenu kuokoa zisihamie kenya. 😂😂😂😂
 
ONGEEENI YOOOTEE ILA KUMBUKENI KUNA WATU FULANI WALIAMBIWAGA MAENDELEO YAO YAMETOSHA WASUBIRI WENGINE,WAKAPELEKEWA WATU KAMA KINA SABAYA,GAMBO,MNYETI,MURRO
KWA KIFUPI K NJARO Na ARUSHA YALIYOKUWA YANAFANYWA NA SABAY NDIYO YALIVYOTAKIWA KU FRUSTRATE WATU WA KULE NA KUKIMBIZA HELA KABISA AND HE DID IT WELL
KULE KWA KIPPI WARIOBA VUNJO WALICHANGA BILIONI 2 YA KUJENGA KILOMITA TATU ZA LAMI,MKUU WA WILAYA ANAKAZANIA HELA APEWE YEYE WAKAKAZA ULIZA KILICHOWAKUTA VIONGOZI WA HUO MCHANGO.... MOTO WA TRA ULIOWAKUTA HADI HUKU DSM
ILIKUWA BALAA KUBWA SANA
mwendaZake alikuwa hatari Sana.
 
Bora sabaya alivyokifunga hicho kiwanda. Eti faru john..nyie wamangi biashara yenu pombe tu ngoja kama wote hamjakua kama warombo. Tutahamia kukamata something zenu kuokoa zisihamie kenya. 😂😂😂😂
Mwenye kiwanda ni mpare
 
Halafu mkikaa hapa mnamsifia jiwe eti alikuwa mzalendo.

Do yoy think haya hakuyaona au kusikia?
Halafu Jiwe mwenyewe eti anaenda Kanisani anahutubia eti "tumtangulize Mungu mbereee, tusibaguane kwa ukabila, ukanda, dini na vyama vyetu, tuwe wazarendo- jinga kweli, kiswahili kibovu. Mungu akaona Jiwe ndo litangulie mbele, Sabaya na wenzao wafuatie. Kwa kina Sabaya ingekubaliwa lile ombi la tatu la kibaka (kama alivyoelekeza Chalamila).
 
Hakuna haja, hivyo Vyeo vifutwe kabisa...
Ni kweli vyeo vya RC, DC vifutwe, then viondoke pia vya RAS na DAS. Hivi vyote ni vyeo vya kuilinda CCM na pia kuwatafutia ulaji wana CCM wanaokosa vyeo vingine vya kitaalam na kisiasa.

TAMISEMI iwe Wizara inayosimamia Serikali za Mitaa kwa ngazi ya Halmashauri chini ya DED. Kila kinachofanywa kwenye Halmashauri kwa sehemu kubwa kina Wizara mama inayosimamia. Mfano Maji, Elimu, Afya, Umeme, Barabara, Kilimo na Mifugo, Ulinzi na Usalama kuna Polisi - OCD ambaye yuko chini ya Polisi HQ na Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwa hiyo TAMISEMI ikiwasimamia vizuri DEDs wakiwa na wataalam wao inatosha kabisa. Hao watasimamiwa na Wabunge na Madiwani kwa ngazi za kisiasa, basi mchezo umeisha. Wananchi wanataka huduma na maendeleo yao, siyo administrative structures zinazoongeza gharama za uendeshaji ambazo mwisho wa siku zinabebwa na walipa kodi.
 
Sabaya hakuwahi kukifungia kiwanda cha Daren fabrics kama inavyopotoshwa na Malisa Godlisten, hapa chini naambatanisha video yenye ushahidi wa kilichotokea siku ya tukio, ambapo ndugu Speshoz mmiliki wa kiwanda hicho alikubali kosa la kutofuata utaratibu halali wa serikali na kukiri kuufuata upya utaratibu huo.

Rai Yangu, Sabaya akiwa Clouds Tv alikiri uwepo wa Project ya kumchafua inayofadhiliwa na Wahalifu aliowadhibiti kule Hai, Miongoni mwa Vijana wanaolipwa kufanya propaganda ni Malisa, Kumbusho Dawson na Twaha Mwaipaya. Acheni huu mchezo nyie vijana wadogo sana.View attachment 1811645
Tumekusikia miss sabaya
 
Back
Top Bottom