Sababu za rais Magufuli kuogopa mikutano ya vyama vya Siasa isipokuwa ya CCM

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Heshima kwenu wakuu,

Mimi najitahidi kumuelewa Rais Magufuli hasa Mambo yake ya kiuongozi.

Rais Magufuli naomba nikukumbushe, upende usipende vyama vya siasa vimepewa Uhuru wa kikatiba kufanya siasa. Nakushauri Ubadikishe katiba ili uonekane unatenda haki. Unawatumia Polepole na Bulembo kupokea wanachama wa vyama vingine lakini unakata wale wa Vyama vingine kupoea wnachama wa CCM ambacho ni chama chako.

Rais anajisifu kuwashughulikia watu sio kuwatumikia watu. Wa kushughulikia watu ni Mahakama sio rais. Subiri uone watu watakavyo shinda kesi.

Ila nimetafakari nikagundua kinachokufanya utetemeke na kuamua kuzua mikutano ya siasa.

i) Unaogopa vyama vya siasa vunaweza kutoa Elimu ya Uraia na Elimu ya Uchaguzi kwa Wananchi kwani itasababisha usichaguliwe tena kwani hata huo Ushindi wako Lowassa anaupinga kwamba umeiba kura.

ii) Unajua kabisa kama watatoa Maoni ya kisiasa kadri watakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zao, kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na Zanzibar, basi utaweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza kuongoza kipindi kimoja.

iii) Unajua kama utaruhusu vyama vya Upinzani kujadili na kushindanisha sera zao na zile za CCM, basi CCM hawana chao sababu unajua ndani ya miaka zaidi ya 50 CCM imeshindwa kuwahudumia wananchi wake japo maji ya kunywa japo wamezungukwa na vyanzo vya Maji. Hadi leo wanakunywa maji kuchangia na Mifugo. Hivyo kama rais ukiwaza unatetemeka.

iv) Unajua kabisa kama utaruhusu vyama vya upinzani kutafuta wanachama wapya, basi wote wa CCM watahamia vyama vya Upinzani. Japo unatumia nguvu kuongea huku ukikazia maneno, kusema kweli watu hawakuelewi nawe unalijua ndo maana hukubali hilo litokee. Juzi kulifanyika chaguzi ndogo hadi leo CCM pamoja na kusaidiwa na Polisi kwa baadhi ya maeneo kudhibiti viongozi wa kitaifa wa Upinzani kwenda kwenye kampeni bado imeangukia pua. Hivyo ilikutia hofu.

v) Unajua Kama utaruhusu vyama vya upinzani kufanya mikutano ya hadhara na maandamano kwa Mjibu wa Sheria na Katiba, basi CCM bye bye.

Mimi najaribu kukuelewa, tatizo unavunja SHERIA NA KATIBA. Nashauri Ubadilishe Katiba ili uwe na Uhuru.

Unaweza ukatenda Mema elfu moja lakini kosa moja linafuta mema yote.

Umeanza Vizuri, lakini watendaji wako bado wanatenda kazi ili uwasifie, kwa kuwa hawana fedha ya kufanya mambo ya maendeleo, wanaamua kuwakamata na kuwanyanyasa wapinzani ili wasikike na waonekane wachapakazi na wamesahau kabisa kwamba hukuwateua wakapambane na Upinzani.

Najaribu kukuelewa unaposema tukuombee, lakini nashindwa kuomba kwa sababu nashindwa kujua nani wa kwanza kumuombea:

1. Kati yako uliye huru Ikulu au Ben Saanane aliyoko kusipojulikana.

2. Kati yako au Alfonce Mawazo aliyeuawa pasipo hatia na hatua hazijachukuliwa nawe unasema ni rais wa wote.

i) Rais wa wote kivipi wakati Wapinzani wanaishi kama wanyama? Sione aibu kusema ni Rais wa CCM.

ii) Rais wa wote wakati wakati hela unanunua Ndege huku wafanyakazi ukishindwa kuwaongezea Mshahara kwa Miaka Miwili?

Naomba uruhusu Wapinzani wakupe Mawazo mbadala ya kuongoza Nchi, usisikilize mawazo ya CCM tu, watakupoteza.

SIASA SIO UHASAMA WALA UADUI KWETU TANZANIA.

Nashukuru kwa jinsi unavyowashughulikia wanaotumia kigezo cha upinzani kufanya vurugu na kutukana. Endelea kuwashughulikia lakini ruhusu siasa. Siasa ni Maisha na siasa ni maendeleo. Huwezi kuendelea wakati wenzio umewaacha Nyuma. Tanzania ni ya CCM wasio na Vyama pamoja na Wanachama wa vyama vingine.
925e14ba886cab603a5679bbaef10554.jpg


Asante
 

mwayena

JF-Expert Member
Apr 21, 2016
2,888
2,000
yani huyu mzee?kuna vitu anaongea unajiuliza mara mbili mbili hivi nafsi haimsuti?
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Wamejisahau wanadhani Tanzania ya sasa ndio ile ile ya miaka ya nyuma!
Mbona kuna ubaguzi wa wazi wazi kabisa
 

Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,411
2,000
Ukweli mtupu hawa ma rc na ma dc wameona kunyanyasa wapinzani ndio maendeleo
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,235
2,000
Mwanaume ukiwa hujiamini ni hatari sana, mbaya zaidi ukiwa na wivu.. Unaweza gombana na ndugu na majirani kwa kuhisi kuwa wanamtongoza au wanakula mkeo, kumbe walaa, wao wapo busy na maisha yao na kuwajenga watoto wao na wako pia wawe na tabia njema na heshima kwa watu wa rika zote..
Baba una wivu, mikwara, roho mbaya, mchoyo, mbabe, mshamba, mwongo, tapta, na tabia zote mbaya... Lazima uwe unajihami sana!!!!!!!!!!!
 

mwita_zakayo

Member
Jun 17, 2017
18
45
Wewe ni mchanga kwenye siasa huwezi kusema kwamba Rais akiruhusu mikutano ya kisiasa eti mtapeleka Sera zenu kwa wananchi wasikubali CCM ni uongo mtupu mbona Sera zenu mlizinadi wakaziona hazifai
 

Denis denny

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
5,787
2,000
Yani hata ile mijinga imeanza kumkataa mana bei ya sukari na chumvi ni somo tosha kwao kuwa wanatawaliwa na manyonya damu siyo viongozi kama wanavyojinadi
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom