Sababu za ndoa nyingi kuvunjiika

Sep 4, 2022
87
148
Ndoa na Jamii

Je, mbona kuna talaka nyingi siku hizi? Sababu ndio hizi, na kuna nyingi zaidi ambazo hazimo katika orodha hii.
Wakati huo watu wengi huwa na chaguo la kujiondoa mapema kutoka ndoa hiyo, kuliko kungoja hadi watakapoachwa.

Siku hizi kuingia na kuondoka katika ndoa ni kama mchezo wa "Cha baba na cha mama". Hakuna wanaoipa ndoa heshima na hadhi yake kama ilivyokuwa hapo awali. Ndoa thabiti ndiyo msingi wa jamii endelevu na ishara ya ustawi wa kizazi kijacho.

Msukosuko katika ndoa ni ishara ya ukosefu wa msingi katika hatua ya kwanza ya kujenga taifa au jamii yenye mtazamo wa kujenga kikubwa cha kudumu. Je, mbona kuna talaka nyingi siku hizi?

Hizi ndizo sababu zinazopelekea ndoa nyingi kuvunjika

Kutojitolea/kukosa kuaminiana

Ingawa nguzo muhimu ya ndoa ni mtu kujitolea kuwa na mwenzake kwa mbivu na mbichi, idadi kubwa ya watu hawajajituma katika ndoa zao, na baada ya miaka miwili utepetevu unaanza kuingia katika uhusiano wenu, na kila mtu anakosa kumjali mwenzake. Hatua hii hufanya ndoa kukosa mvuto na baadaye kusababisha watu kutaka kutalakiana.

Uzinzi /mahusiano ya nje ya ndoa
"Mipango ya kando" ni mojawapo ya sababu kuu ambazo huwafanya watu kutalakiana. Endapo mwenzako atagundua kwamba unakula tunda jingine na siyo lake tu basi ole wako! Safari ya talaka imeanza. Unapoanza kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa mwenzako huhisi kutengwa, na pia kupatwa na hofu ya uwezekano wa kuachwa. Wakati huo watu wengi huwa na chaguo la kujiondoa mapema kutoka ndoa hiyo kuliko kungoja hadi watakapoachwa.

Migogoro na malumbano ya mara kwa mara
Kuna haja ya wanandoa kutafuta jinsi ya kusuluhisha mizozo yao na pia kupunguza malumbano ambayo yana hatari ya kuvuruga uhusiano wao. Ishara za mwanzo kwamba chuma kitaingia moto ni ugomvi na kelele kati yenu, mmoja wenu baadaye huchoka na kelele hizo na baadaye kuamua kwamba anataka kuondoka.

Kuolewa au kuoa ukiwa na umri mdogo
Wengi wa wanandoa ambao wana jumla ya umri wa miaka 23.3 wapo katika uwezekano wa juu kutalakiana. ingawaje kumekuwa na ongezeko la umri wa mtu kuoa au kuolewa hadi miaka 50. Ndoa za watu walio na umri mdogo zimepatikana kuwa na matatizo si haba. Mnapooana mkiwa wadogo ndivyo ilivyo hatari ya ndoa yenu kuvunjika haraka ikilinganishwa na wale waliofunga pingu za maisha wakiwa na umri wa juu kidogo.

Matatizo ya Kifedha
Utafiti umeonyesha kwamba ukosefu wa fedha za kuendesha mipango yenu kama wanandoa ni hatua inayoweza kusababisha talaka. Wakati pesa zinapokosekana kuna uwezekano wa kuwepo hali ya taharuki ambayo pia huvuruga uhusiano wenu.

Kila mmoja wenu ana mawazo kuhusu mtakavyogharamia hiki na kile na hivyo basi hamna muda wa kuzungumza mambo yanayohusiana nanyi. Kwa kinaya, pesa nyingi nazo zina uwezo wa kusababisha matatizo katika ndoa pia. Iwapo hamtajua au hamna mpango wa kuzitumia pesa zenu hasa katika hali ambapo hamukua na pesa hapo awali –basi kuna mmoja au nyote mtabadilika kwa njia mbaya itakayovuruga ndoa yenu.

Kutumia dawa za kulevya/mihadarati
Takriban asilimia 30 ya wana ndoa wa zamani wametaja utumizi wa mihadarati kama sababu iliyowafanya kutalakiana. Ulevi kupindukia, sigara, bangi na dawa za kulevya kama vile cocaine na mandrax husababisha msukosuko katika uhusiano wowote na ndoa haijasazwa katika patashika za matumizi ya mihadarati. Kama siyo pesa za kununua dawa hizo basi ni matokeo ya kuzitumia kama vile kuvurugana au kusahau kufanya jambo au kulifanya kwa njia isiofaa.

Dhulma za kupigwa/kuvurugwa kiakili
Takriban robo ya ndoa zote zinazovunjika hutokana na dhulma za mmoja dhidi ya mwenzake. Dhulma hizo siyo lazima ziwe za mtu kushambuliwa bali pia kukukwazwa kimawazo au hata kukufanya uwe na mawazo kupindukia. Kuwa katika hali tete ya kifikra ni jambo linaloweza kukufanya ujichukie na uamue hata kujiua. watu wengi huvumilia kwa muda lakini dhulma katika ndoa zina hatari na hivyo basi wengi huamua kupata talaka kabla ya mambo hayajachacha.

Muingilio wa kifamilia na marafiki
Kuna ndoa ambazo huvunjika kwa sababu ya muingilio wa jamaa kutoka pande zote. Tofauti kati ya mmoja wenu katika ndoa na jamaa za mwingine huweza kukomaa na kuwa kidonda kikubwa katika ndoa yenu. Hatimaye mwenzake huhisi kana kwamba hufanyi chochote kumkinga dhidi ya jamaa zako na kuamua kupata talaka.

Unafiki wa marafiki na jamaa zenu pia ni jambo mnalofaa kuwa makini nalo. Kuamini kila unachoambiwa na huyu na yule bila ithibati ni mambo hatari katika ndoa. Wakati wote hakikisha unaikinga imani ya mwenzako katika kila unalosema na kufanya.

Ongezea zingine unazoona zinapelekea ndoa nyingi kuvunjika.
 
Uhuru uliopitiliza unaochagizwa na matamanio ya kifedha na mwili.

Mfano sisi tumekua miaka yote unamuona baba au mama baada ya shamba wakiwa nyumbani. Jioni wakitoka ni baba kwenda senta basi.

Siku hizi mume yuko kikaoni dodoma. Mke yuko semina ya wanawake arusha ni vurugu.

Matamanio ya kingono yanayochagizwa na kidigitali. Mfano njia rahisi za mawasiliano, ushawishi toka kwa watu wa karibu kupitia mitandao. Mfano ata humu jf kuna uzi za kusifia michepuko.
 
Sasa kama sababu za kuvunjika ndoa zinafahamika bila shaka na suluhu yake ipo!! Ila watu wanakiburi tu .
 
Back
Top Bottom