Sababu za mwanaume kushindwa kurudia tendo!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Huo ni ukweli, lakini kama nilivyosema katika mada yangu ya awali kuwa kinachotakiwa ni kuthibiti nguvu hiyo katika hatua za mwanzoni na hasa kama ukiwa katika hatua za mwanzo za kujizoeza kufanya hivyo.

Inafurahisha tu kwamba kuna watu wengi wamenipigia simu na kuniambia kuwa wamefanikiwa kwa kiwango cha kushangaza.

Jambo jingine ambalo wiki jana sikulizungumzia ni la wanawake kutajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wanaume wafike kileleni mapema, hiyo inatokana na kutojua vipindi vya mapumziko ambavyo wanaume huwa wanavipanga katika kujipa nguvu na kujipunguzia mihemko mikali inayowafanya wafikie kilele mapema.

Inashauri kwa mwanawake kusitisha kwa muda purukushani za huba pindi atakapobaini kuwa mwenza wake anavuta kasi ya kuongeza gia. Isitoshe dondoo za mazungumzo zinashauriwa sana kuchukua nafasi, isiwe ni kasi kwa kwenda mbele kana kwamba mapenzi ni mchezo wa kukomoana au ni pambano la kumpata mshindi.

Mapenzi hayako hivyo na sio lazima yafanyike kwa mhemko mkali kwa kipindi chote kana kwamba ni mbio za mita mia.

Pamoja na hayo wanawake wanashauriwa kutoa angalizo la umbali wa wao kufika kileleni, ili kumpa fursa mwanaume naye kupata kipimo cha wakati wa kumaliza. Angalizo hilo litamsaidia kumfanya apoteze mawazo kwa hofu ya kuonekana hafai kwa kitendo cha kumwacha mwenzake njia panda.

Hizi ni kanuni ndogo, lakini nawashauri sana watu wenye tatizo hili kuwasiliana nami ili tuelemishane kwa kina kwani mara nyingine huchukua muda kwa mtu kupata matokeo sahihi ya zoezi hili la kujizuia. Baada ya kusema hivyo sasa tutazame mada ya wiki hii!
Miongoni mwa tatizo sugu la upungufu wa nguvu za kiume ni kwa wanaume kushindwa kurudia tendo au kuwa na idadi chache za awamu.

Kusema kweli hili sio tatizo kubwa linalohitaji tiba ya matatibu kwa kiasi hiki, isipokuwa ni kupata elimu ya kutambua uwezo wa miili yetu. Kwa maana hiyo maelezo ya dondoo zifuatazo yanaweza kumsaidia mwenye tatizo hili.

MAZOEA YA MWILI: Watu wengi wenye mjukumu hujikuta wakiizoeza miili yao kufanya mapenzi kwa tendo moja kutokana na kukosa nafasi, kwao kukutana na mwanamke ni short time.

Kwa maana hiyo miili yao hukosa hamasa ya kurudia kutokana na mazoea. Hivyo mhusika anapotaka kwenda raundi nne lazima aanze kuuzoeza mwili kidogo kidogo asifikiri atakurupuka mara moja na kwenda mara tano.

Huo ni upofu wa kielimu. Kwa maana hiyo mwanaume kabla hajalalamikia kushindwa kurudia aangalie historia yake kwamba amekuwa anashiriki mara ngapi!
UMRI WA MTU: Kuna watu wengine wa ajabu sana wanajikuta wakihangaika kutafuta dawa za nguvu za kiume eti kwa sababu hawaendi kama zamani, ilhali wanajua fika nguvu za mwili hupungua kutokana na umri unavyokwenda.

Maana itakuwa ni ujinga kumwabia Firbat Bayi atimue mbio kama zamani! Kumbe kinachotakiwa ni kukubaliana na hali na kutulia na kuachana na hofu ya kupungukiwa nguvu za kiume!
HAMASA KUSHUKA: Upofu mwingine wa kimawazo ni kwa wanaume na wanawake kutotambua kuwa hamasa ya kimapenzi hushuka kulingana na muda wa wapendanao kuwa pamoja. Kuna wengine wanadhani kuwa watadumu kwenda mara sita au saba kama walivyokuwa wakati wa uchaga wa penzi lao.

Na wakiona dosari wanaanza kulaumiana, "mbona zamani mume wangu ulikuwa unakwenda mara saba!" Ukweli ni kwamba kakuchoka miaka kumi, kunakipi kipya kitakachoamsha hamasa ya penzi na endapo mitindo ni ile ile na migogoro kibao?
Kwa maana hiyo ukichunguza kwa makini utaweza kubaini kuwa watu wengi wanawake na wanaume wanajitesa na mawazo ya kupungukiwa nguvu za kufanya mapenzi bila sababu. Kama wangekuwa na ufahamu juu ya mabadiliko ya miili yao wangekubaliana na ukweli wa mambo na kuacha kujisumbua kulilia ujana ambao umeshawapita.

Mwisho kama nilivyosema katika mfululizo huu wa mada za upungufu wa nguvu za kiume ni kwamba siku zote mwili wa mwanadamu una desturi ya kuzoea kile ambacho kinafanyika kila siku. Kwa mfano kama wewe huna desturi ya kunywa chai asubuhi, mwili wako hauwezi kudai chakula hicho kamwe kutokana na kwamba sivyo ulivyozoezwa.

Lakini kama mwili huo huo utazoezwa kinyume chake na kulishwa chai kila asubuhi basi itakuwa vigumu sana kwa mtu husika kupitisha masaa hayo kama hakutia kinywaji hicho mdomoni. Hivyo basi kabla ya kwenda hospitali au kubwia madawa ya kuongeza nguvu jiulize maswali juu ya mazoea yako.

Na kama ukitaka kubadilisha mazoea hayo kumbuka kuwa haitakuwa jambo la leo bali litachukua muda kuliwekea kumbukumbu katika mwili wako. Hivyo basi nawashauri wale wote ambao wanashindwa kurudia kufanya tendo wafanye utafiti juu ya nini kinapungua katika ushindwaji wao.

Lakini pia wasikubali kukata tamaa na kujiona hawawezi eti kwa sababu wamekutana na mwanamke fulani na wameshindwa kufanya hivyo.

Kwani mbali na hayo niliyosema kuna jambo la nguvu za mwili kutokana na siku husika. Kuna siku nyingine mtu anaweza kuwa dhaifu tu kwa namna moja au nyingine. Anaweza kuwa kachoka, ana mawazo, anaumwa, hana furaha kutokana na sababu wazi au zilizojificha na mambo kama hayo!
Hivyo isiwe jambo rahisi kwa mhusika kujilaumu na kujiona hafai, kufanya hivyo kutazalisha wasiwasi na matokeo yake mtu huyu atakuwa akitokewa na hali hiyo kila anapokutana na mwanamke na pengine akabaki na kumbukumbu kuwa mara ya kwanza kutokewa na hali hiyo alikuwa na mwanamke fulani na hivyo kuingiwa na mawazo kuwa pengine alirogwa na kusahau ukweli kuwa kajiroga mwenyewe na hofu yake! Leo tupige kambi hapa tuonane tena wiki ijayo. Nawatakia kazi njema!
 
Pia mazoea yana ongezea upungufu, Mke na Mume wakikaa pamoja miaka mingi, mwisho inakuwa kama Kaka na Dada, Hisia zinapungua, inafika asubuhi, lol kumbe nilikuwa nimelala na mke/mume. Inakuwaje Mzee anacheza kipindi kimoja hapo nyumbani lakini akipata mechi ya ugenini ana enda Extra time????
 
Pia mazoea yana ongezea upungufu, Mke na Mume wakikaa pamoja miaka mingi, mwisho inakuwa kama Kaka na Dada, Hisia zinapungua, inafika asubuhi, lol kumbe nilikuwa nimelala na mke/mume. Inakuwaje Mzee anacheza kipindi kimoja hapo nyumbani lakini akipata mechi ya ugenini ana enda Extra time????
Kweli mechi za ugenini zina utamu wake ndio maana extra taimu ya muhimu, Mazoea kama ulivyosema nayo yanasababisha kwa kiwango kikubwa.
 
Nafikiri sababu nyingine inayofanya wanaume wasiende round nyingine ni utundu wa wanawake. Wanawake wengi wa huku uzunguni upstairs wana exposure nzuri sana lakini linapokuja suala la mapenzi wengi utundu na manjonjo ni sifuri tofauti na kuku za kienyeji.

Unakuta binti mkimaliza round one, yeye kazi yake inakuwa ni kukuangalia usoni tu........hawezi lamba koni wala kufanya makeke mengine. Na kwa wanaume wengi kupata mihemuko kwenye round one sio issue, issue ipo kwenye subsequent rounds.
 
Mwisho kama nilivyosema katika mfululizo huu wa mada za upungufu wa nguvu za kiume ni kwamba siku zote mwili wa mwanadamu una desturi ya kuzoea kile ambacho kinafanyika kila siku. Kwa mfano kama wewe huna desturi ya kunywa chai asubuhi, mwili wako hauwezi kudai chakula hicho kamwe kutokana na kwamba sivyo ulivyozoezwa.

Asante Mzizimkavu kwa darsa zuri! Elimu hizi ni nzuri sana kwa wanandoa na kwa hakika zinaweza kuponya ndoa nyingi sana.
 
Na ndio maana ni vizuri kuoa mke zaidi ya mmoja, mkipeana zamu, ukirudi kwa wa kwanza unajihisi kama uko mech ya ugenini hivi. nimesema kuoa na sio nyumba ndogo, msinikoti vibaya.
 
Pia mazoea yana ongezea upungufu, Mke na Mume wakikaa pamoja miaka mingi, mwisho inakuwa kama Kaka na Dada, Hisia zinapungua, inafika asubuhi, lol kumbe nilikuwa nimelala na mke/mume. Inakuwaje Mzee anacheza kipindi kimoja hapo nyumbani lakini akipata mechi ya ugenini ana enda Extra time????

Kuwa na desturi ya kubadilisha viwanja uone.......!!!!!!! Kuchezea uwanja wa nyumbani pekee ni tatizo kubwa.
Siku moja moja unajikung`uta unampeleka wife saloon anapendeza then unampeleka viwanja vizur vizur pembezoni mwa mji au nje ya mji.
Usipokwenda extra time au ukimchoka basi inabidi utafute dawa ingine.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom