sababu za kuvunjika kwa EAST COAST TEAM (upanga)

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Jamani wana jf wenzangu. Mwenye kujua kisa cha kuvunjika kwa hili kundi la EAST COAST lililokuwa na makazi yake pale upanga ambalo liliundwa na CRAZY GK, AY, MWANA FA, OTEN, BUF G, SNARE ......... na wengineo . Tafadhari naomba mnijuze sababu za kufa kwa kundi hili.
 
"Chanzo cha Mabaya ni pesa na wasichana chunga sana alishasema SALU T"-Fid Q

N.B Mabaya-Mitafaruku,Mikanganyano,Kuvurugika kwa makundi etc
 
Wezi tu ndio sababu mwana fa anjipendekeza kwa ruge ili aimbe fiesta, ay na JK hawajipendekezi wana pesa
 
Jamani wana jf wenzangu. Mwenye kujua kisa cha kuvunjika kwa hili kundi la EAST COAST lililokuwa na makazi yake pale upanga ambalo liliundwa na CRAZY GK, AY, MWANA FA, OTEN, BUF G, SNARE ......... na wengineo . Tafadhari naomba mnijuze sababu za kufa kwa kundi hili.

Hebu nikuambie japo kwa kifupi, kundi hili lilikuwa la kwanza nchini kuwa kampuni na kuanza kufanya kazi zake lenyewe, ukiwemo uzinduzi wa albamu ya mwisho ya GK kwa udhamini wa Konyagi na TBL.
Hii ikafanya wasanii wote walio chini ya ECT kutotumiwa kwa kupunjwa malipo yao, hali hii ikafanya mahusiano ya ECT na akina Ruge yawe mabaya kwani walizoea kuwatumia wasanii kwa kuwalipa laki mbili mbili katika show za Fiesta.
Alichofanya Ruge ni kuivuruga ECT kwa kuwachukua FA na AY na kuwapeleka kwa Mamu yule wa GMC na kuwaombea mkataba wa kutengeneza albamu ya pamoja, na kwa kuwa Mamu hapindui kwa Ruge, akatoa mkataba!
Sasa kutokana na mkataba huo AY na FA wakalazimika kujitoa ECT ili wawe huru kufanya kazi bila kusimamiwa na ECT Company, na moja kwa moja wakajitoa. Hivyo wakatengeneza ile albamu yao, bila kujua malengo ya Ruge.
Maana wenyewe wasanii walishazoea kupelekwa kwa Mamu na Ruge ili kupata mkataba wa albamu kisha albamu ikitoka Ruge anachukua cha juu chake, hivyo haikuwa rahisi kwao kujua lengo lililo nyuma ya pazia.
Lakini lengo la Ruge lilikuwa ni kuwaondoa wanamuziki walio juu wa ECT Company ili kuiua ECT ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa na uelekeo wa kuwafumbua macho wanamuziki wa Kitanzania kwa kuwa na utaratibu maalum kwa kuzuia kupunjwa malipo yao na wajanja.

Nadhani nimeeleweka!
 
ngoja aje 'o ten' anaweza kutupa full stori ambayo nafikiri haitatofautiana sana na ya mdakuzi,hawa majamaa yalikuwa majembe mno basi tu
 
oooh hapo nimekusoma mkuu . kwahiyo njaa yao na upeo wao duni mwana fa na ay hawakuweza kugundua mbinu ya muhaya yule ruge . dah kumbe ndio maana hata mr 2 alimpaka sana yule jamaa. kumbe ndio anavyoisha kwa kulaghai wasanii . ok ndio maana hata tht kawaweka mfukoni . lakini sijui why mr 2 alimsamehe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom