Sababu za kutumbuliwa aliyekuwa Katibu Mkuu Nishati na Madini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Katibu Mkuu Madini abishana, atumbuliwa
www.ippmedia.com/sw/habari/katibu-mkuu-madini-abishana-atumbuliwa

Muda mfupi baadaye, taarifa ya 'kutumbuliwa' kwa Prof. Ntalikwa aliyeteuliwa Desemba mwaka 2015, ilitolewa kupitia taarifa ya Ikulu.

Taarifa hiyo ilisema nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Wawili hao walitofautiana kuhusu mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kujua kilichomo ndani ya makontena 256 ya 'mchanga' wa dhahabu (concetrates) yanayoshikiliwa na TPA kufuatia marufuku ya Rais Magufuli ya kuyasafirisha nje.

Hadi sasa kampuni za madini zinadai ndani ya makontena hayo na mengine 20 ambayo Rais Magufuli alionyeshwa katikati ya wiki iliyopita yote yakiwa kwenye hatua za mwisho za kusafirishwa kuna mchanga, lakini TPA inasema kuna madini.

Baada ya Spika na Kamati yake kuelezwa jinsi kontena hizo zilivyokamatwa, ndipo kila upande ulipotoa ushauri wa namna ya kulikabili suala hilo.

Aliyekuwa Katibu Mkuu huyo alitoa ushauri ambao ulionekana kupingana na maelezo ya Mhandisi Kakoko ambaye alidai ana uhakika wa asilimia 90 kuwa kilichomo kwenye kontena hizo ni madini na siyo mchanga.

Prof. Ntalikwa, kwa upande wake, alishauri kuunda timu ya wataalamu kutoka sekta mbalimbali kuchunguza suala hilo.

Alishauri kuchukuliwa kwa sampuli na kuzipeleka maabara na kujua ukweli.

“Mheshimiwa Spika, napendekeza tutengeneze timu ya wataalamu kuchukua sampuli na kuzipeleka maabara kupima," alisema Prof. Ntalikwa. "Timu hiyo inaweza kujumuisha taasisi nyingine, alafu taarifa iwekwe wazi kwa umma.”

Ushauri huo haukumfurahisha Kakoko ambaye moja kwa moja alisema anaandaa barua kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Wizara waeleze kwa kina juu ya suala hilo na kwamba linahitaji kujipanga sana ili kuliendea.

“Katibu Mkuu wewe labda ni mgeni, haya masuala huyajui vizuri," alisema Kakoko.

"Vipimo vinafanyika lakini humu kuna jambo la ziada, hatuwezi kuliendea hili jambo kwa ‘theory’ (nadharia) bali ‘practical’ (vitendo) zaidi.

"Twende hadi kwenye migodi tuone wanavyochukua sampuli, zinavyopimwa na kule unapopelekwa China, Ujerumani na kwingine tujue matokeo ya vipimo vyao, vinginevyo hatutafanikiwa.”

Alisema kwa sasa kila kontena linaloingia bandarini humo lazima lipite kwenye mashine maalum kujua kilichomo, na kwamba wameongeza mashine sita za 'scan' ili kuongeza ufanisi zaidi.

Baada ya ziara hiyo, Ndugai na wabunge hao walitoa majumuisho na kueleza kuwa Bunge litaunda kamati ya kuchunguza mikataba, sheria na mchakato zima wa sekta ya madini, ikiwamo kujua kilichomo kwenye makontena 256.

Ripoti ya kamati hiyo, alisema Ndugai, itaishauri serikali kama iendelee na biashara ya kusafirisha 'mchanga' huo au la.

Alipoulizwa na Nipashe, mbele ya Spika, wakati wa chakula cha mchana ana uthibitisho gani kuwa ndani ya makontena kuna madini na si 'mchanga', Mhandisi Kakoko alisema “Sisi ni watendaji wa serikali.

"Tumeshafanya uchunguzi wetu na kubaini kuwa ndani ya makontena yale kuna madini ya dhahabu kwa asilimia 90.”
Ziara ya Spika na wabunge imetokana na matokeo ya ziara ya kushtukiza bandarini hapo ya Rais Magufuli ambapo alionyeshwa makontena 20 ya kampuni ya Acacia ya 'mchanga' wa dhahabu, yakisubiri kusafirishwa nje ya nchi kinyume na maelekezo ya yake Machi 2.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMA), Gilay Shaonika, alieleza wabunge hao kuwa uchukuaji wa vipima ufanyika mgodini na ripoti kutumwa bandarini na baadaye hulinganishwa na itakayotoka nje ambako 'mchanga' huo umepelekwa.

Alisema kila kontena la mchanga huo huwa na asilimia 0.02 ya madini yoyote, jambo ambalo lilipingwa na Spika na kueleza hakuna mwekezaji atakayefanya biashara ya faida hiyo ikiwamo gharama kubwa za kusafirisha mchanga huo.

“Hakuna mwekezaji anaweza kufanya bishara kama hii kwa faida ya 0.02," alisema Spika Ndugai.

"Lipo tatizo; ndiyo maana tunataka tufanye uchunguzi nasi tuweze kuishauri serikali iendelee na biashara hii au la.
"Nani analinda maslahi yetu mchanga unapofika Ulaya na kupimwa, au tunasubiri ripoti zao?”

Kauli ya TMA ilipingwa na Mhandisi Kakoko pia, ambaye alisisitiza kuwa na uhakika asilimia 90 ya kilichomo kwenye kontena hizo ni madini na siyo asilimia 0.02 ya madini kama inavyoelezwa.

Baada ya kauli hiyo, Spika alimhoji mwakilishi wa TMAA “kwa kufikiri kwako unadhani kuna mwekezaji anaweza kufanya biashara kwa faida ya 0.02? Atoe gharama za meli, usafiri na bandari.”
Alijibu haiwezekani.

“Ni lazima tufanye uchunguzi kujua hii biashara inaendeshwaje na ni nani ananufaika nayo," alisema zaidi Ndugai.
 
Jamani hata kama huna akili kiasi gani huwezi fikia hitimisho la huyo anayejiita mhandisi. 90% iwe madini? Au hesabu za % hazipandi. Hata kama hao wawekezaji wakijaza dhahabu walizochimba kwenye makontena na kuchanganya na mchanga kidogo huwezi jaza makontena 256!!! Ni wazo la kipumbavu kabisa.
 
Kakoko (DG Bandari) anasema yale Makontena zaid ya Miambili yamejaa madini wakat Prof anamwambia yamejaa Mchanga wenye madini.

Kontena lijae Dhahabu halafu Kaburu aruhusu likae kizembe Zembe Bandarini! Imagine Gram moja tu gram sio kg ya Dhahabu ni zaid ya laki moja halafu Kontena Miambili ziwe zimejaa Bandarini

DG wa Bandari hataki Yale Makontena yafunguliwe Kuona kilichomo kwa kuwa anajua Rais ataumbuka ukikutwa Mchanga wenye Madini badala ya Madini kwa kuwa Rais alishasema Ikifunguliwa Watanzania hatutaamini

Katibu Mkuu yeye alitaka Kontena zifunguliwe Wataalam waone kilichomo na vipimo vipelekwe Maabara na Spika Ndugai akakubaliana na wazo Hilo na akaahidi kuunda hiyo Tume.

Huenda Rais hajapenda Bunge kuingilia hili Sakata sasa hasira zake kupeleka kwa Katibu Mkuu na kumfukuza. Hata akiteuliwa Katibu Mpya naamini hatotoa ushirikiano kwa Bunge na Kamati teule!

Yale Yale ya Nape, Chagua kuwa Upande wa Ukweli au wa Rais!
 
“Ni lazima tufanye uchunguzi kujua hii biashara inaendeshwaje na ni nani ananufaika nayo," alisema zaidi Ndugai.[/QUOTe

Wafungue container zote mbele ya wenye mali kuhakiki kilichomo ili kumaliza ubishi.
 
Kakoko (DG Bandari) anasema yale Makontena zaid ya Miambili yamejaa madini wakat Prof anamwambia yamejaa Mchanga wenye madini.

Kontena lijae Dhahabu halafu Kaburu aruhusu likae kizembe Zembe Bandarini! Imagine Gram moja tu gram sio kg ya Dhahabu ni zaid ya laki moja halafu Kontena Miambili ziwe zimejaa Bandarini

DG wa Bandari hataki Yale Makontena yafunguliwe Kuona kilichomo kwa kuwa anajua Rais ataumbuka ukikutwa Mchanga wenye Madini badala ya Madini kwa kuwa Rais alishasema Ikifunguliwa Watanzania hatutaamini

Katibu Mkuu yeye alitaka Kontena zifunguliwe Wataalam waone kilichomo na vipimo vipelekwe Maabara na Spika Ndugai akakubaliana na wazo Hilo na akaahidi kuunda hiyo Tume.

Huenda Rais hajapenda Bunge kuingilia hili Sakata sasa hasira zake kupeleka kwa Katibu Mkuu na kumfukuza. Hata akiteuliwa Katibu Mpya naamini hatotoa ushirikiano kwa Bunge na Kamati teule!

Yale Yale ya Nape, Chagua kuwa Upande wa Ukweli au wa Rais!

Prof. Ana uhakika kabisa kua huo mchanga hauna madini, isipokua ni wa madini. Kakoko naye anadai huo si mchanga bali ni madini.

Tz ya vi-wonder
 
Jamani hata kama huna akili kiasi gani huwezi fikia hitimisho la huyo anayejiita mhandisi. 90% iwe madini? Au hesabu za % hazipandi. Hata kama hao wawekezaji wakijaza dhahabu walizochimba kwenye makontena na kuchanganya na mchanga kidogo huwezi jaza makontena 256!!! Ni wazo la kipumbavu kabisa.

Prof kakataa kuwa Mpumbavu kukubali hili kafukuzwa kazi!

Nadhani atapunguza
Kuteua Ma Prof alidhani atawaburuza kizembe zembe
 
Jamani hata kama huna akili kiasi gani huwezi fikia hitimisho la huyo anayejiita mhandisi. 90% iwe madini? Au hesabu za % hazipandi. Hata kama hao wawekezaji wakijaza dhahabu walizochimba kwenye makontena na kuchanganya na mchanga kidogo huwezi jaza makontena 256!!! Ni wazo la kipumbavu kabisa.
Kama 90% ni dhahabu basi barabara zetu zitakuwa zinaharibika kwa uzito uliokithiri, mizani watakuwa walipwa fedha kibao .... watch it ,..not to that extent ...
 
Prof. Ana uhakika kabisa kua huo mchanga hauna madini, isipokua ni wa madini. Kakoko naye anadai huo si mchanga bali ni madini.

Tz ya vi-wonder

Kakoko na Bosi wake hawajui tofauti ya Madini na Mchanga wenye Madini wao wanajua ni kitu kimoja!
Ukiwafundisha Tofauti wanakufukuza kazi !

CAG nae akikabidhi report ya CAG Leo Ikulu kapewa kazi ya kufuatilia Hilo Skendo la Madini na akampiga biti kuwa akimaliza CAG ataunda Timu ya siri isiyojulikana ichunguze.

Analazimisha Majibu
 
Jamani hata kama huna akili kiasi gani huwezi fikia hitimisho la huyo anayejiita mhandisi. 90% iwe madini? Au hesabu za % hazipandi. Hata kama hao wawekezaji wakijaza dhahabu walizochimba kwenye makontena na kuchanganya na mchanga kidogo huwezi jaza makontena 256!!! Ni wazo la kipumbavu kabisa.

Bwana Eli 91 wewe ndo hujaelewa ana maana asilimia tisini ya dhahabu iliopaswa kuwa extracted
 
Jamani hata kama huna akili kiasi gani huwezi fikia hitimisho la huyo anayejiita mhandisi. 90% iwe madini? Au hesabu za % hazipandi. Hata kama hao wawekezaji wakijaza dhahabu walizochimba kwenye makontena na kuchanganya na mchanga kidogo huwezi jaza makontena 256!!! Ni wazo la kipumbavu kabisa.

Mkuu hujaelewa....rudia kusoma kauli ya mhadisi ...anahuhakika wa 90%...anaaamini kabisakabisa. hajasema kilichomo 90% ni madini. He has 90% confidence what is inside mostly gold....He believe highly.

Back
Top Bottom