Sababu za Kutopiga Kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za Kutopiga Kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Waberoya, Oct 4, 2010.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Huku watu wakiwa wehu na wamechanganyikiwa na kampein huku wale waota ndoto wakidhani slaa atashinda, najihurumia maskini mimi,ni nani atakayetuokoa na akili hizi za aibu si kwa kizazi cha sasa na hata kijacho.

  Nchi hii sio ya CCM wala sio ya chadema wala cuf wala TLP n.k, nchi hii ni ya watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama, makabila, dini na makundi yoyote yale!

  Kama hivyo basi hata serikali ya nchi hii haitakiwi kuwa ya chama kimoja, bali ya mseto!!! Ili kufikia hapa tukubaliane kuwa tunahitaji mambo yafuatayo!
  1. Mabadiliko ya katiba, ya kuwa vyama vyote viunde serikali kulingana na kura watakazopata
  2. Tume ya uchaguzi iwe huru na ya kujumuisha vyama vyote
  3. Mabadiliko juu ya katiba juu ya nguvu ya rais. Jaji mkuu achaguliwe na majaji na aripoti kwa majaji,kadhalika kamisha mkuu wa polisi, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, na kitengo cha rushwa kiwe chini ya usalama wa taifa!(proposal)

  Tukishamaliza hayo, ambayo kwa makusudi hayakufanywa mawaka 1992!, ndio ukombozi utakapoanzia hapo, na faida yake ni kuwa
  1. Vyama vitafanya kampeni kamilifu, hali vikijua kwa kura zozote zile watapata ushiriki ndani ya serikali ya mseto. Hii itawapa motisha vyama vyote kujitoa na kufanya kila namna kukubalika kwa wananchi
  2. Itawapa ari wananchi kujitokeza kupiga kura, hali haitabadilika mwaka huu, idadi ya kura wanazopata wapinzani inapungua kila baada ya miaka mitano kutoka 1995, ila hali maendeleo ya science na teknolojia yanaongezeka na kufanya hali nzima kuwa haieleweki
  3. Upinzani halisi ni kubadilisha mambo ya msingi kwanza!!! Hii haihitaji degree au karama Fulani, Mh.Slaa nilimuuliza kwa nini wasijali katiba kwanza akasema ni ‘kazi ngumu' ili hali leo anavuja jasho, na akikosa urais atakaa bench bila kulisaidia taifa lake kwa sera zake nzuri
  4. Watanzania wanaweza na wataweza , kama mwaka 1995 tuliona nini kilitokea je, tumeona Zanzibar, je ni kitu gani cha ajabu kinategemewa mwaka huu?? Wakati watu wanawaza kura, vyama tawala huwa vinadeal zaidi na watangaza matokeo tu!!!, na wakitangaza CCM mshindi, ndio washindi hao, na jeshi wanasema msipinge matokeo
  Naumia kila ninapoona mtu anasema kupiga kura, kura is an ultimate solution, yes but must be on sound foundation, sio kila kupiga kura ni kufanya mapinduzi, tumeishawahi kupiga kura huku kivuli na huku mtu, kitu kinachojionyesha wazi hata leo hii!

  Tukutane baada ya uchaguzi, kama tunaamini kwa namna hii ndio kuleta mabadiliko, basi we are truly accepting evolution, by which will come only through CCM!!! Otherwise we have to throw one party-governing system of which we will be employing revolution! Whats happening now is evolution, yes we will see changes but may be million years to come, you don't believe? ask Kiranga.

  Tuache mteremko!

  After Election:

  I will be visiting this and my other posts regarding politics and politician in our beautiful country of Tanzania. I will repost this for the next five years if God wishes to remind ourselves.

  Bila mabadiliko ya NEC na katiba hakuna kinachowezekana, Nilipropose kutopiga kura si kwa sababu sitaki mabadiliko, CCM wangekuwa kwenye shinikizo kubwa la kubadili NEC na katiba endapo upinzani ungesema na kutaka hivyo prior to election. Ndiyo tungesubiri hata miaka 2 tena ya kipindi cha mpito huku CCM wangekuwa bado madarakani but at least after that baaada ya kura unajua kabisa kura yangu haijapotea, siyo imeenda hewani tu!!!! every vote must do something!!!!

  Ninavishutumu vyama vya siasa na Slaa mmoja wapo maana tulijibishana humu ndani na alikiri kuwa mabadiliko ya katiba ni ngumu!! huyu mtu anataka kwenda ikulu for what? hakuna tunayemuamini pale IKULU SI SLAA WALA BABA YANGU, IKULU PALINDWE NA SHERIA TIMILIFU AMBAZO ZIMEPITISHWA NA SIO ETI NITABADILI KATIBA NIKIINGIA IKULU!

  For the nex half decades I will open Tanzanian eyes regarding this na jinsi gani vyama hivi vinafanya biashara kwa kisingizio cha mabadiliko. Sasa mnataka kusema Rungwe na Mziray nao walijua watashinda . Hivi kutoksema ukweli ni kupona kweli??

  Mnaingiaje kwenye uchaguzi mkijua kabisa NEC wataipendela CCM?? baada ya uchaguzi unalalamika! Idd Simba akisema watanzania wengi wanamtindio wa akili nikiwepo mimi msomi anatuonea??

  SABABU KUBWA YA WATU KUTOPIGA KURA NI KUJUA WAZI JK ATASHINDA, investigate it!
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuona majina mengine hayafui dafu umeona utumie jina lako la zamani huna jipya.
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Huna vision wala hujijui kama we ni binadamu!
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Nitakuona wewe mwenye vision baada ya uchaguzi!

  Je hujaona hoja hapo juu? au umeona aibu kutolewa tongotongo ambazo haukuwahi kufikiria?

  be free thinker ebo! hatuna upinzani na hatujataka wawepo, tunajipa moyo tu, CCM itashinda hilo halina upinzani, je ukienda kwenye ushindani unaojua unashindwa nani mwenye akili? anayesema tubadili mbinu au yule anayesema twende hivyohivyo?

  chukulia DSM tunaowaona wajanja wabunge karibu wote walikuwa CCM! hujaona tatizo hapo,

  anyway uchaguzi huo, this month, I will accept this method, if and only if kura za Slaa zitakuwa angalau asilimia 20! nazo hazitafika, believe me

  naamini hapa ni kuelezana ukweli na kuamsha uhuru wa mawazo, kujipa moyo na kufuata mkumbo wa wale asilimia 70 sio vyema! wanaoshindwa hoja ndio wanakuja na kusema unatumia jina jipya! kuna rollcall humu? SIJAONA ujibuji wa hooja hiyo hapo juu, kurusha vijembe is a waste of time, jibuni hoja!! watoto wa juzi, kuna vitu huwa havijibiki kirahisi, ukiona kweli ulikosea piga U-turn, lets think of 2015, lakini baada ya kubadili yale ya msingi, viini macho hivi vya kutupumbaza jamani tumechoka, kuanzia 1961 mpaka leo, hatuchoki tu!!

  Lets go to the basics, nchi imeuzwa na wapinzani ni viini macho! bila mabadiliko ya katiba hakuna maendeleo nchi hii!! na mabadiliko haya si rahisi yanahitaji kukakamaa na wanaoweza kubadili ndio wapinzani kweli na kwa sasa hawapo, narudia tena HAWAPO, read it and loud HAWAPO, again HAWAPO!!
   
 5. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mi naona sababu yako kubwa ya kutopiga kura, unataka kupoteza haki yako ya msingi, fullstop!
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Beauty dada, tuko pamoja, wala hii hoja yangu haina lengo lolote baya, just imagine now, nguvu zote hizi anazitumia Slaa. halafu let say akipata asilimia 20, then hana input yoyote kwenye serikali ijayo! hivi utaratibu wa serikali ya mseto ungekuwepo, huoni ingefikia muda tunatangaza kifo ca CCM mapema kabla ya mechi kuanza? kama wapinzani wnapata 40% mwaka huu na wanapata wala wizara fulani kuongoza, miaka ijayo si tunahakika wanaweza kupata hata asilimia 60?

  Kweli kupiga kura ni haki ya msingi, lakini katika hali huru na misingi huru, inyoeleweka na una hakika na kura yako itafanya kazi fulani, LEO WAPIGA KURA wa wapinzani hatakama watafika asilimia 40, still hawana nafasi (i mean kura yao haina nafasi katika serikali yao inayowaongoza siku zote) kuna haki hapo? hii kauli mbiu siyo sahihi, mpiga kura tanzania hana haki, maana anaweza kupoteza muda wake na kura yake, any vote must have input in government!

  yaani post hizi zote za kutaka wapinzani waende magogoni zipotee hivi hivi bila wala impact, kumbuka tukishindwa tunaanza moja 2015!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Gooosh!

  Huyu member alikuwa amepotea sana...Nadhani ni ile kipindi alileteana za kuleta na mapolisi wa mtandao huu, akaamu kuposti stori moja mara 50 hapa na kuboa watu, baada ya kuona haifai akaamua kuja kivyengine!
  It should be this guy!

  Sasa suala la kubadili katiba ndiyo Agenda kuu katika sera za WAPINZANI wengi...mi sielewi anataka nini cha ziada!

  Mseto ni process, na si rahisi ukaibuka leo ghafla...ni maelewano na maongezi yatakayopata baraka na muafaka, na si kuridhishana kwa vyeo!

  Mi naona kama umekurupuka sana broda, na ni ajabu wazo kama hili kutoka kwako WABEROYA...rudi uanze upya!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Tangu mwaka 2008, sikuwahi kuona jina lako kaka, kama unayajua hayo mengine , si ungeyataja mkuu, kwa sasa napima uwezo wako wa akili kwa kujibu hoja, dogo jibu mawe hayo hapo juu, mstari umechachorwa, otherwise you will prove, kuwa ni mvivu wa kufikiri.JF ina weyewe wewe! kuna wengine hawajarusha post wana miaka, siku wakija, usiseme ni wageni au wailikuwa na majina mengine, angalia hoja!! na jibu, ikikugusa, kaa kimya, unafikiri wengine hawajaziona,

  umefika muda wa kuita vitu kwa majina yake halisia, kama hatujafikiri na kukaa chini swala la kuikomboa nchi yetu, nani afanye? tukijidanganya na kugundua kuwa tunakoenda siko, nani asee, wakisema kati yetu watageuka ni wabaya wetu, hasha! kama tunataja jina la ukombozi wa taifa hili siko kinyume chako, ni ubadili wa mawazo yetu! tukishindwa uchaguzi, then 2015, tutafanya hivi tena?

  kibaya nilichosema mimi ni kipi, au fimbo niliyotumia kuamsha watu, tulisema haya mkuu, kabla haujajiunga rasmi!, tulibishana na kila study za org. mbalimbali zinaonyesha Kikwete atashinda, yaani ufisadi wote tuliouanika,post tulizotuma, maendeleo ya mawasiliano, still kuna watu wanasema JK atashinda? kama kweli atashinda, tubishe wakati matokeo yatakuwa hivyo? kama mmoja wetu akisema tumekosea hapa, then anakuwa traitor? God forbid, what is forums for then?
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,085
  Trophy Points: 280
  Shindwa na ushindike wewe sio Mtanzania!
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Nani asiyekujua wewe, eti hupigi kura at the sametime unataka kiongozi bora, kama akili yako ndiyo inakutuma hivyo basi ni ujuha.
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hatutaki KURA yako
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Hata JK alituambia hivyo hivyo hataki kura zetu huna haja ya kunikumbusha kura yangu never to wabeba mafisadi soma signature yangu.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  So far sijaona hoja yangu ikijibiwa, simtaki JK mkuu kama wewe! sijui ile kamati ya kuwafunda watu iko wapi, JF imevamiwa, mtu anatoa hoja, watu wote waliojibu hamna aliyejibu hoja intelectually, hizi taarabu haziondoi ukweli, na kwa taarifa yako namchukia JK kuliko wewe, mi sitaki hata kuisikia CCM, lakini ukikasirika ndio unazuia panya au inzi? huwa hatuwazuii kwa kukasirika, strategy ndio zinazotakiwa, na zilitakiwa kufanyika kabla ya kura!

  rudi kwenye hoja, kua hata leo tu!

  cheers,
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Kumekucha uwanja wa nyamagana, hoja yangu imejibiwa kwa ' shindwa na ushindike'

  These are people they call themselves 'educated'

  Huyo mnayetaka awe rais kwa mazingaombwe, hii hoja ilishamtoa nishai na nyie mnaivamia kichwa kichwa, ebu tuanze kuyapekua majibu yake ya miaka hiyo, ndiyo tuone usanii wa akina Mtei, Mbowe na sasa Slaa juu ya taifa hili1
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida yako ya kujiona wewe bora kuliko wenzako..... mambo ya kuweka quotes kwenye educated yanamaanisha nini?

  Chuki yako dhidi ya Dr Slaa, Mbowe na Mtei inazidi kudhihirika hapa kadri siku zinavyokwenda. Mafisadi wanafiki mwaka huu mtajinyonga
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mpenzi mkubwa wa chama la kifisadi - ccm. Utajaribu sana kukimbilia kwenye trivials lakini maandishi yako yanakufunua jinsi ulivyo.
   
 17. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Waberoya anasimamia nini? huyu ni nani eti hataki kupiga kura na hampendi kikwete na mafisadi? kama hamtaki Kikwete arudi ikulu na bado anasema hatapiga ikulu ana maana gani?
  Nadhani huyu jamaa amechanganyikiwa na anataka wana wa nchi hii, wachanganyikiwe kama yeye na wasiende kupiga kura ili tuendelee kutawaliwa na mafisadi. Kila kura ya kila Mtanzania ni muhimu sana kuleta mabadiliko kwa hiyo tusidanganyike.

  Huyu chui anajitahidi kuvaa ngozi ya kondoo ili atumalize. nafikiri sitakuwa nimekosea nikisema kuwa huyu Waberoya ni jini jike lililotumwa na Sheikh Yahya likijifanya mwanamke mrembo ili tulitongoze.
  Mi Nimeshituka nitapiga kura yangu.
   
 18. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wee vip!! sasa wote tukiacha kupiga kura kwa kigezo cha kukubliana na mawazo yako unategemea kuwe na uchaguz TZ? Mawzo kama haya usilete huku bwana.

  Ushauri: -Ili hiyo katiba ibadilike na iwe hivyo ulivyopendekeza basi kapige kura haraka sana tarehe 31.
  -U sikipigie kura chama kingine zaidi ya (CHADEMA Dr Slaa) ili abadilishe hyo katba unayosema manke as you say since then katiba haijabadilishwa pamoja na kuwepo kwa malalamiko kibao (kiburi cha ccm na kutokua na uchungu na nchi)
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa mko upande wa negative.

  Leo gazeti la citizen lieandika wasiwasi wa chadema kuwa NEC itaipendelea CCM!, refere to my main post in this thread, nimeongelea kuhusu swala la tume ya uchaguzi. Je ni akili kuingia uwanjanai ukijua refa ataipendelea timu pinzani? nguvu zote hizi zipotee bure? guys be serious at leat to preach the truth where is necessary

  Kumbukeni, Mrema naye alikuwa na nguvu pengine zaidi ya hii! lets wait baada ya uchaguzi, tutaendelea na hii maada.

  kuna mambo ya msingi ya kufanya kabla ya so called kupiga kura, asa i said, vote ni ultimate solution katika misingi imara na bora, bila hivyo, tutakuwa tukiwehuka kwa furaja ya muda na CCM will reign if not rule forever

  Misingi ya nchi hii ni chama kimoja, hatuna msingi ya kitaifa ya vyama vingi, na hapo ndipo ninapoona tatizo, vita yangu ni kuweka msingi ya vyama vyote(vingi kwanza) sina chuki na yeyote maana hawanisaidii kitu.

  Guys, what if wakishinda wapinzani yet, NEC ikasema CCM mshindi? visiwani imeshatokea mara nyingi, achilia nchi jirani, na sheria inasema NEC wakisema mshindi fulani, then is final! jeshi ndio hao wanaonya mapema, tukikata rufaa majaji karibu wote ni CCM! MAY BE i AM JUST WORRYING! but shouldnt I speak?

  cheers once more!
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu poleni sana kwa uchungu na hali mnayopitia hivi sasa.

  Pamoja na hayo, mtoto akianguka kama alikuwa akicheza huwa anafokewa asirudie tena, hali kadhalika wakati tunaona CCM wakitapatapa lazima tuangalie tumekosea wapi au tumeanguka wapi.

  Slaa hawezi kushinda labda mitume wote wafufuke leo hii, sio kwa sababu hana uwezo kwa sababu hakuna mazingira yaliyotayarishwa ili mshindi yeyote awe kweli mshindi

  sijaona serikali iliyotayari kuachia madaraka bila kufanya mbinu zozote za kubaki HAIPO, in human nature that is impossible , hivyo basi!

  ilitakiwa kuiandaa na kupigania tume ya uchaguzi iwe huru tangu miaka 5 iliyopita, achilia mbali mabadiliko ya katiba n.k
  leo hii kusema CCM wataiba kura hata chadema wakichukua mwaka 2015 wengine watasema the very same thing

  wakati tunalialia kama wajinga fulani, lazima tujue kuwa vyama vya siasa kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi hali wakijua hata kama wakishinda mtangaza matokeo atatangaza CCM mshindi ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu ambayo historia haitaacha kutuhukumu.

  Sio kwa sababu tunalilia mabadiliko basi tuwe wajinga tusioweza kufikiri, natumia neno wajinga na wapumbavu because they are perfectly matching us I will not embelish these words ! Leo hii mbaba mzima na ndevu zake na balls zinaning'ininia anafikiri eti CCM ghafla watageuka malaika wa nuru na kutowaza kuiba kura, wakti miaka hii mitano tumeshuhudia na kuhakikisha ni wezi wa mali asili, richmond,epa, rada, iptl n.k, ila kwenye uchaguzi tunawaamini wao na tume yao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  I repeat this is good time for opposition parties to retreat!!!

  -Ishinikizwe iundwe serikali ya mpito, inayojumuisha vyama vyote
  -mabadiliko ya katiba ambayo yata accomodate vyama vyote kuunda serikali ya mseto
  -tume ya uchaguzi iwe huru
  -Ni rahisi opposition parties kupata support ya watanzania wengi na mataifa ya nje endapo watasimamia hayo hapo juu, na dhahiri tutauona ukombozi wa watanzania -LIVE, na kamwe si kwa kubahatisha wala kusubiri bahati!!!!!
   
Loading...