Sababu za kuongezeka kwa ujambazi

chakochetu

Senior Member
Oct 13, 2012
108
35
Bado tunaendelea kutafuta sababu za kuongezeka kwa matukio ya ujambazi siku za hivi karibuni:
Hebu tuangalie baadhi ya sababu hizi,na labda kuna zingine sijaweza kuzibaini:
[1].Kuchelewa kwa mishahara ya askari polisi hadi mwezi unaofuata
[2].Maisha kuwa juu,na bado kipato hakiongezeki kulingana na mfumuko wa bei
[3].Wanasiasa na wafanyabiashara kufanya ufisadi,na hakuna hatua yoyote inayochuliwa dhidi yao.
[4].Magenge ya wauhujumu uchumi kupatiwa kinga na viongozi wa ngazi za juu.
[5].Serikali kutojali hali zao za maisha ya kila siku.
 
Labda ni kwa sababu Sikukuu zimekaribia, na wao wamefulia....
 
Baadhi ya polisi kushirikiana na majambazi ili kujikwamua kiuchumi

Polisi kuwa busy kudhibiti na kufuatilia CHADEMA badala ya kuangalia usalama wa raia

Serikali kutojali raia wake
 
Pengo la maisha(tabaka)
Kukosa uadilifu ukichunguza wanasiasa wengi kuanzia udiwani wamefanikiwa kupitia ujambazi
Askari wasio waadilifu kupewa vyeo na kuvitumia kulinda majambazi (kashfa ya magendo kilimanjaro,kifo cha kamanda wa polisi Mwanza)
Askari kufanya kazi kisiasa wamekazania ulinzi shirikishi wakisahau kuwa wanalipwa pesa kwa kodi zetu ili kutulinda
Uteuzi mbovu wa rais kuanzia mkuu wa polisi,waziri na wengineo
Rushwa ambayo inawafanya askari wadogo kushindwa kuchukua hatua
 
Back
Top Bottom