Sababu za kung'atuka uenyekiti jimbo la ubungo.

Mikael P. Aweda, you're a person to emulate, you really have cheered my heart.
Hausubiri kuambiwa kuwa sehemu fulani kunalegea, ila ww umepaona na kuchukua action.
Take your time, introduce yourself to the soldiers and field force boys (amini hawa wana mengi ya kukueleza).
Slowly Dar is ideologically changing with Peple's Power!
 
Aweda Ongera sana, ila mimi nina swali moja nje ya hoja mama; Ulisoma UDSM? na Kama ni ndio ulisoma Idara gani na mwaka gani? Samahani sana Mkuu kwa hilo swali.
 
Kuna watu wameandika thead ihusuyo kujiuzulu kwangu, ndani yake kuna ukweli lakini pia kuna upotoshaji wa baadhi ya mambo. Naomba nitoe maelezo sahihi.Mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chadema ubungo na mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni mwanachama ni nayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote. Nilipoingia Ubungo baadhi ya viogozi waliokuwepo walikuwa wanakaimu nafasi zao ktk baadhi ya ngzi, nikamilisha chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba. Shahidi wa Yote haya Mbunge mwenyewe. Nilifanya naye kazi kwa karibu sana. Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu. MCHAKATO WA KUNG’ATUKA.Nimewashirikisha wazee wa ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu wa Jimbo la Ubungo. Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wamenielewa. Kuhusu kujiuzulu ubungo.Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo. Kwanini nimjizulu? A)Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily. On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, wakanielewa.B)Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo ambayo ni imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo (wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao. Busara ni mimi kuongeza nguvu ktk jimbo kama hilo.C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana – around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo unaweza kujenga chama Ubungo wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung’ang’ania ubungo tena imara.D) Viongozi na wanachama wa ukonga wameniomba nigombee ukonga, Viongozi wengi na wanachama wa ukonga, baada ya kuona utendaji wangu walioniomba nigombee nafasi mojawapo ktk uchaguzi unaokuja hivi karibuni. Nikawakubalia. Hiyo nayo ni sababu mojawapo. Mwisho;Ni matumaini yangu kwamba yale mazuri tuliyoyafanya pamoja mimi na viongozi wenzangu watayaendeleza wenzangu wanaobaki. ALUTA CONITINUA.MIKAEL P AWEDA
Nimeyapenda sana maelezo yako. Mungu akutangulie ktk nia njema yako
 
Hongera sana chama hujengwa na wanachama wenye moyo. Pigania maendeleo ya wananchi wote huo ni mwanzo tu, mmeshinda ubungo ukombozi umehamia ukonga, naamini Dar es Salaam yote itakombolewa na Tanzania nzima itakuwa huru. CHADEMA Tunawakubali, Tunawaamini.
 
Michael P. Aweda namfahamu sana, ni rafiki yangu, nimesoma naye sekondari moja (o-level), na nikamkuta chuo kikuu (akiwa amenitangulia). Ningeshangaa, kwa jinsi ninavyomfahamu, na thread niliyoiona asubuhi ya leo hapa jukwaani, kama angefanya upupu ulioelezwa kwenye ile thread. Binafsi nakupongeza sana kaka yangu, nadhani yule jamaa alyeleta ile thread ni wa magamba bila shaka alikuwa anatingisha kiberiti cha CHADEMA akadhani ni kama wao wanavyonyukana huko kwao chama (CCM) kimegawanyika.
 
Sababu zako ni za msingi kabisa! Haihitaji kuwa na elimu hata ya shule ya kata kuelewa hili. Kwavile huko unakoenda bado utaendelea kukijenga chama, basi tunakuhakikishia kuwa tutakuwa pamoja daima, na hakuna kulala hadi kieleweke!
 
songa mbele, kumng'oa Mnyika ubungo ni kazi sana, nenda kajaribu bahati yako huko tuongeze majimbo, umesoma vizuri alama za nyakati
Sijaona sehemu aliyosema alitaka kumng'owa Mnyika wala hakuna sehemu aliyosema ana nia ya kugombea Ubunge, alichosema anagombea Uongozi wa chama katika jimbo la ukonga. Full stop.
Hapa ndipo utakapowajuwa wasomi wa shule za kata walivyo janga kwa Taifa. statement iko very clear lakini wewe hujalizika mpaka uweke na maneno yako ya kubuni!
 
Hongera sana,sasa nimekuolewa adhma yako tofauti na ilivyolipotiwa awali.kazana kujenga nchi.
 
Kuna watu wameandika thead ihusuyo kujiuzulu kwangu, ndani yake kuna ukweli lakini pia kuna upotoshaji wa baadhi ya mambo. Naomba nitoe maelezo sahihi.Mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chadema ubungo na mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni mwanachama ni nayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote. Nilipoingia Ubungo baadhi ya viogozi waliokuwepo walikuwa wanakaimu nafasi zao ktk baadhi ya ngzi, nikamilisha chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba. Shahidi wa Yote haya Mbunge mwenyewe. Nilifanya naye kazi kwa karibu sana. Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu. MCHAKATO WA KUNG’ATUKA.Nimewashirikisha wazee wa ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu wa Jimbo la Ubungo. Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wamenielewa. Kuhusu kujiuzulu ubungo.Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo. Kwanini nimjizulu? A)Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily. On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, wakanielewa.B)Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo ambayo ni imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo (wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao. Busara ni mimi kuongeza nguvu ktk jimbo kama hilo.C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana – around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo unaweza kujenga chama Ubungo wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung’ang’ania ubungo tena imara.D) Viongozi na wanachama wa ukonga wameniomba nigombee ukonga, Viongozi wengi na wanachama wa ukonga, baada ya kuona utendaji wangu walioniomba nigombee nafasi mojawapo ktk uchaguzi unaokuja hivi karibuni. Nikawakubalia. Hiyo nayo ni sababu mojawapo. Mwisho;Ni matumaini yangu kwamba yale mazuri tuliyoyafanya pamoja mimi na viongozi wenzangu watayaendeleza wenzangu wanaobaki. ALUTA CONITINUA.MIKAEL P AWEDA
je huyu ni Mikael P Aweda wa kweli au feki?kuna mtu alishawahi kuja na waraka mreeeefu halafu akajiita Edward Lowasa.tuwe makini wakuu!
 
All the best mkuu,hawa ndio vijana wa Chadema bwana,kijana mwenzangu huo ni uamuzi mzuri sana na endeleza mapambano hivyohivyo najua nchi itakomboka hivi karibuni kupitia sisi vijana kua na uwezo wa kuthubutu waziwazi,all the best Kamanda.
 
Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung’ang’ania ubungo tena imara.

Uamuzi wa busara. Chama kinahitaji vijana wengi wenye mtazamo kama wako kipindi hiki tunachoelekea kukamata dola.
 
Back
Top Bottom