Sababu za "kufutwa" kwa Upadre wa Karugendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za "kufutwa" kwa Upadre wa Karugendo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Che Kalizozele, Jan 8, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Deusdedit Jovin​
  Januari 7, 2009[​IMG]
  NIMESOMA taarifa ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine NiweMugizi, iliyotolewa “kwa maelekezo ya Mamlaka Kuu ya Kanisa Katoliki” iliyoko Roma, na kuchapishwa katika gazeti la Kiongozi, toleo namba moja la mwaka 2009, kuwa hivi sasa “Privatus Karugendo ni mwamini mlei asiye na daraja la upadre kuanzia tarehe 14 Septemba 2008 ilipotolewa Hati ya Baba Mtakatifu yenye namba ya protokali 4182/08.

  Hata hivyo, kwa mujibu wa Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki: “Ni kweli, aliyepewa Daraja (la upadre) halali aweza, kwa sababu kubwa, kuruhusiwa kuacha wajibu na kazi zinazohusiana na Daraja; au anaweza kuzuiliwa asitekeleze. Lakini hawezi kurudia katika hali ya mlei kwa maana halisi, kwa sababu alama iliyochapwa kwa kupewa daraja ya dumu daima. Wito na utume unaopokewa siku ya kupewa Daraja (la upadre) humtia alama ya kudumu.”

  Hivyo basi, kwa kuzingatia nukuu hiyo ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki kifungu cha 1583, wito na utume unaopokewa siku ya kupewa Daraja (la upadre) humtia alama ya kudumu mhusika hadi kifo chake.

  Na kwa sababu ya dosari hii ya kimantiki kama inavyojionyesha kwenye hukumu ya Papa Benedikto wa XVI, mtu yeyote anaweza kushawishika na akaamini kwamba huenda hata sababu zilizotolewa kama msingi wa kumwondoa Padre Privatus Karugendo kutoka katika “hali ya utumishi wa kipadre” zinayo dosari kama hii.

  Hivyo, kwa lengo la kuweka kumbukumbu za kihistoria sawasawa kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo, bila kupinga uhalali wa hukumu ya Baba Mtakatifu na Mahakama ya Kanisa iliyochunguza kesi hii, nakusudia kudodosa muundo wa kimantiki wa hoja zake, kuzifafanua hoja hizo, na hatimaye kuzihakiki kwa lengo la kubaini iwapo zinakidhi “viwango” vya kitaaluma na kiimani au kinyume chake.

  Kutokana na sababu zilizotolewa katika gazeti ka Kiongozi, ni wazi kwamba, upotofu wa imani anaohusishwa nao Padre Karugendo unahusu maadili katoliki ya kijinsia (catholic sexual ethics).

  Hivyo, ni muhimu sana hapa kuyafupisha maadili hayo ili ufupisho huo uweze kuwa msingi wetu hapo baadaye wakati wa kuzinyumbulisha na kuzifafanua sababu zilizotumiwa ‘kumtimua’ Padre Karugendo.5
  Kimsingi, maadili Katoliki ya Kijinsia yanaweza kufupishwa mara moja katika kanuni tatu pekee kama ifuatavyo:

  Kanuni ya kwanza kuhusu maadili katoliki ya kijinsia inasema kwamba, tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili lazima lifanyike ndani ya ndoa ya mwanamume na mwanamke pekee.

  Kanuni hii maana yake ni kwamba, ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke.

  Kanuni ya pili kuhusu maadili katoliki ya kijinsia inasema kwamba, mara zote tendo la kupeana zawadi ya mwili kati ya mwanamume na mwanamke lazima lifanyike katika namna ambayo itaruhusu kutungwa kwa mimba iwapo yai la kike ni pevu.

  Kanuni hii maana yake ni kwamba, ni mwiko kwa tendo la kupeana zawadi ya mwili kati ya mwanamume na mwanamke kufanyika katika namna ambayo haitaruhusu kutungwa kwa mimba wakati yai la kike ni pevu.

  Na kanuni ya tatu ambayo ni kanuni ya maadili katoliki katika ujumla wake inasema kwamba, waumini wanawajibika kuutii uamuzi unaofanywa na maaskofu wao katika jina la Kristo, kuhusu masuala yote ya imani na maadili, na kisha kuushika uamuzi huo kwa moyo mmoja.

  Kanuni hii maana yake ni kwamba, ni mwiko kwa waumini wanaowajibika kuutii uamuzi uliofanywa na maaskofu wao katika jina la Kristo, kuhusu masuala yote ya imani na maadili, kuukaidi uamuzi huo katika namna ambayo inaonyesha utovu wa nidhamu kwa maaskofu hao.

  Kinachoruhusiwa na kanuni hii ni kwamba muumini anaweza kujizuia kutii uamuzi wa maaskofu pale anapokuwa na shaka juu yake, lakini bila kuyapinga waziwazi, na wakati huo akaendelea kufanya uchunguzi zaidi, huku akiwa na utayari wa kukubali uamuzi wa mwisho wa maaskofu kuhusu suala husika.

  Kutokana na kanuni hizo tatu hapo juu, inafuata kimantiki kwamba matendo yafuatayo ni haramu kwa mujibu wa maadili katoliki:

  Tendo la kupeana zawadi ya mwili nje ya ndoa kwa ajili ya kuingiza tupu ya kiume kwenye tupu ya kike (adultery); tendo la kupeana zawadi ya mwili kabla ya ndoa kwa ajili ya kuingiza tupu ya kiume kwenye tupu ya kike (fornication); tendo la kupeana zawadi ya mwili kwa ajili ya kuingiza tupu ya kiume kwenye tupu ya nyuma ya binadamu (sodomy);

  Aidha, matendo yafuatayo ni haramu kwa mujibu wa maadili katoliki: tendo la kupeana zawadi ya mwili kwa ajili ya kusisimua tupu za mbele kwa kutumia vidole (masturbation); tendo la kupeana zawadi ya mwili kwa ajili ya kusisimua tupu ya mbele ya mwanamume kwa kutumia mdomo (fellatio); tendo la kupeana zawadi ya mwili ambapo angalau mmojawapo amekula kiapo cha useja; tendo la kupeana zawadi ya mwili ambapo angalau mmojawapo amevaa kondomu kwenye tupu yake ya mbele (condomised intercourse).

  Kadhalika, tendo la kuunga mkono matendo haya yanayoitwa haramu kimaadili kwa mujibu wa imani katoliki au matendo yanayofanana nayo (theological and doctrinal dissent) ni haramu kimaadili.

  Na sasa basi, kutokana na hitimisho hili kuhusu maadili katoliki ya kijinsia, tunaweza kuzielewa zaidi sababu zilizotoloewa na Papa Benedikto wa XVI kama chanzo cha ‘kutimuliwa’ kwa Padre Privatus Karugendo.

  Na katika muktadha huu, uchanganuzi unaonyesha kwamba Baba Mtakatifu ‘amemtimua’ Padre Karugendo, angalau, kwa sababu kuu sita:

  Kwanza, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki ya kijinsia yanasema kwamba “ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke,” Padre Privatus Karugendo anawahimiza vijana ambao hawajaoana kutumia kondomu kama kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kila wanapoamua kwa hiari yao wenyewe kujinufaisha na haki yao ya kupeana zawadi ya mwili, na hivyo kupotosha maadili katoliki.

  Pili, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki ya kijinsia yanasema kwamba “ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke,” Padre Privatus Karugendo anawahimiza wanandoa kutumia kondomu kama kinga dhidi ya maambukizi ya VVU kila wanapoamua kwa hiari yao wenyewe kuchepuka nje ya ndoa kwa lengo la kuhemea zawadi ya mwili, na hivyo kupotosha maadili katoliki.

  Tatu, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki ya kijinsia yanasema kwamba ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke, Padre Privatus Karugendo anawahimiza watawa waliokula kiapo cha useja kutumia kondomu kama kinga dhidi ya maambukizi ya VVU na mimba zisizotarajiwa kila wanapoamua kwa hiari yao wenyewe kuchepuka nje ya kiapo chao kwa lengo la kuhemea zawadi ya mwili kwa muda, na hivyo kupotosha maadili katoliki.

  Nne, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki ya kijinsia yanasema kwamba ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke na kwamba ni mwiko kwa tendo la kupeana zawadi ya mwili kati ya mwanamume na mwanamke kufanyika katika namna ambayo haitaruhusu kutungwa kwa mimba wakati yai la kike ni pevu, Padre Privatus Karugendo anawahimiza vijana ambao hawajaoana kutumia kondomu kama kinga dhidi ya mimba zisizotarajiwa kila wanapoamua kwa hiari yao wenyewe kujinufaisha na haki yao ya kupeana zawadi ya mwili, na hivyo kupotosha maadili katoliki.


  Tano, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki ya kijinsia yanasema kwamba ni mwiko kwa tendo la kupeana zawadi ya mwili kati ya mwanamume na mwanamke kufanyika katika namna ambayo haitaruhusu kutungwa kwa mimba wakati yai la kike ni pevu, Padre Privatus Karugendo anawahimiza wanandoa kutumia kondomu kama kinga dhidi ya mimba zisizotarajiwa kila wanapoamua kwa hiari yao wenyewe kujinufaisha na haki yao ya kupeana zawadi ya mwili, na hivyo kupotosha maadili katoliki.

  Na sita, Baba Mtakatifu anasema kwamba, wakati maadili katoliki yanasema kwamba, waumini wanawajibika kuutii uamuzi unaofanywa na maaskofu wao katika jina la Kristo, kuhusu masuala yote ya imani na maadili, na kisha kuushika uamuzi huo kwa moyo mmoja, Padre Karugendo ameandika makala nyingi kwenye magazeti akiwajulisha waumini wenzake na viongozi wa Kanisa Katoliki maoni yake juu ya kile kinachohusu Kanisa lakini bila kuzingatia ukamilifu wa maadili na imani ya Kanisa wala heshima kwa viongozi wake na waamini kwa ujumla, jambo ambalo linamaanisha kwamba amekiuka mafundisho ya imani katoliki yanayokataza uasi wa wazi dhidi ya mamlaka halali.

  Hatimaye, kutokana na sababu hizi sita, Baba Mtakatifu anasema kwamba, kwa mujibu wa sheria za Kanisa Katoliki, kila kosa lililotendwa na Padre Privatus Karugendo adhabu yake ni ‘kutimuliwa’ kutoka katika huduma ya upadre. Hivyo, amehitimisha kwamba ni halali kwake ‘kumtimua’ Padre Privatusi Karugendo, uamuzi ambao hauna rufaa dhidi yake.

  Hata hivyo, sisi waumini wa kanuni ya kuona, kuhukumu na kutenda yatupasayo, kanuni ambayo inatukuzwa sana na Baba Mtakatifu, hatuwezi kuishia hapo. Kuna maswali mawili muhimu lazima yajibiwe kitafiti.

  Swali la kwanza ni hili: je, utaratibu uliotumika ‘kumtimua’ Padre Privatus Karugendo ni halali kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki? Na swali la pili ni hili: je, sababu zilizotolewa kama msingi wa kutimuliwa kwa padre Privatus Karugendo ni sahihi?

  Katika ajira yoyote, mwajiri anapomtimua kazi mwajiriwa, na mwajiriwa akakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mwajiri, wasuluhishi (mediators, arbitrators and adjudicators) hutafuta kujibu maswali haya mawili. Na kwa kweli taarifa kwamba hakuna rufaa dhidi ya uamuzi wa Papa zinatuhimiza kuchunguza jambo hili kwa kina.

  Hili ni lazima kwa mtu yeyote anayemwabudu Mungu wa haki za binadamu. Na kwa kuwa Kanisa Katoliki linajinadi kama taasisi inayokuza na kuhami haki hizo tunatarajia itaharakisha kuweka bayana mambo haya. Vinginevyo, uamuzi wa Papa Benedikto wa kumi na sita unaweza kuwa ni pigo kubwa sana kwa Kanisa Katoliki.

  Katika makala zijazo nitachunguza mambo haya kwa kina kabisa. Na kwa kuanzia nitachunguza uhalali wa kanuni mbili. Kanuni moja ni inayosema kwamba ni mwiko tendo lolote la kupeana zawadi ya mwili kufanyika nje ya ndoa ya mwanamume na mwanamke.

  Na kanuni nyingine inasema kwamba ni mwiko kwa waumini wanaowajibika kuutii uamuzi uliofanywa na maaskofu wao katika jina la Kristo, kuhusu masuala yote ya imani na maadili, kuukaidi uamuzi huo katika namna ambayo inaonyesha utovu wa nidhamu kwa maaskofu hao.

  Usahihi wa kanuni hizi mbili zikishapembuliwa vizuri uchambuzi mwingine kuhusu sababu za ‘kumtimua’ Padre Karugendo unakuwa ni rahisi.
  [​IMG]


  Simu:
  0734 800808​
   
  Last edited by a moderator: Jan 9, 2009
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...same topic inaendelea tayari lakini naona imehamishiwa kwenye imani na dini ambako wengine hatuna pass!
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Naomba hii ibaki hapa maana kule kwenye imani na dini wengine tunaogopa kuingia! Ila, naomba Mods wawe macho (sisi wengine tuwasaidie) kuwa kila panapotokea posting ambazo zinataka kutupeleka kwenye vita za mwituni za kule kwenye imani na dini, posting hizo zifutwe!

  Amandla.........
   
 4. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
   
 5. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kanisa hili linatutatiza wengi na hizo sheria zilizopitwa na wakati, naona Kuna haja ya Mapadri kama Karugendo kuanzisha kanisa katoliki lililo na focus ya kuhoji mambo yaliyopitwa na wakati kama kwenda pekupeku!
   
 6. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  "Ya Kaizari mwachieni kaizari" - If you can't beat them, join them". Kwa kweli huhitaji kuwa Padri au Mchungaji au Shekh kuwakosoa waliomo (clergies within sect). Kwa kifupi huyu Karunyendo aliapa kuzilinda hizi sheria 'mbofu", leo hii ana wageukia wale wale waliomuapisha na kuwanyea, unategemea nini. Akafanye kazi nyingine kuna gazeti la pale Mwanza linahitaji waandishi.
   
 8. Modereta

  Modereta Senior Member

  #8
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Walio Wakatoliki waliingia ukatoliki wakijua sheria zake, na wale ambao hawakujua hawajakatazwa kutoka. Jamii yeyote hata kanisa ina taratibu zake ambazo zinakuwa desturi nazo huwa sheria. Kanisa katoliki likaenda mbele zaidi likaandika Cannon Law. Haya yote yalijulikana kwa Karugendo akiwa seminari , akiwa Padre na baada ya kupumzinka akitafakari mwishowe wakaona watamngoja mpaka lini ngoja tumpe uhuru wa kufanya anchotaka, maana kabla ya hili anakuwa bado anachunguzwa maendeleo yake, sasa haonyeshi dalili za kubadilika sasa???. Ikumbukwe mwaka 1517 Martin Luther alichoshwa na tabia fulani za ukatoliki akaacha, aliandika barua yenye sababukuu saba na nyingine 10 kwa nini anaacha, akaenda akanzisha ulutheri hakuna aliyemkataza, leo ulutheri ni moja ya madhehebu makubwa duniani, sasa yeyote asiyependa sheria katika jamii anayoishi basi ni kujitenga tu unaanzisha au unajiunga na kingine ukipendacho, si unao uhuru, mbona Mwingira aliondoka leo kaanzisha Efata, naye Fernandes kaanzisha Agape, kelele za nini?????????????????
  Hii haina maana kuwa yote wayafanyayo katika ukatoliki yanampendeza kila mtu, LA HASHA, lakini kila mtu anao uhuru wa kuabudu huko au la, tusiwaamulie watu wengine. Baadhi yetu toko huko tuliko kwa vile tu tulizaliwa tukakuta wazazi wetu huko tuka baki huko, sasa walaumu hao na wewe mwenyewe kwa kun'gan'gania huko
   
 9. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hata kama wataanzisha makanisa yao, unadhani hakutakuwa na matatizo? Taja kanisa lililoanzishwa, ambalo waumini wake wanaishi raha mstarehe! Palipo na binadamu kuna mambo kwani watu wanaweza kuwa na mgogoro siyo kwa sababu sheria ni mbaya bali interpretation yao ya sheria ni mbaya.

  Na kuwa na kanisa lisilo na sheria ni sawa na kutokuwa na kanisa kabisa. Na sheria zikiwepo lazima ziwa'exclude' watu fulani na kuwa'include' wengine kwenye system.
   
 10. johnj

  johnj Member

  #10
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Haina maana kwa padre kusema ati anaonewa kwa kosa ambalo kalitenda. tunasisitiza kwamba padre ni lazima awe mseja. useja usiwe tu kwa nje bali kwa ndani. yapasa ujichunge mwenyewe. kama huuwezi useja na bado unataka uwe padri lazima tukushangae.
  Kwa nini asijiunge na kaniza la Anglican ambalo linafanana fanana na katoliki na aoe. la, hilo halimfai aende lutheran au aanzishe dhehebu lake kama Kakobe. Kwani ni lazima aendelee kuwa mkatoliki ? anapokuwa mkatoliki isiwe tu kwa jina ni lazima afate na ahubiri yale ambayo wakatoliki wanaamini vinginevyo yeye si mkatoliki.
  Jamani msituharibie kanisa letu. kama haziwezi sheria atoke hakuna anayemzuia. kwa heri Karugendo
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kule hakufai, mtu unaomba access ukijua utaenda pata huduma ya kiroho, LOL!!, Ni balaa na kufuru zisizo na mipaka watu utadhani hawana dini vile, ukichungulia mara moja hurudi tena wala kupata hamu ya kurudi. Nafikri 2009 MoDs wafanye reform kule kwenye ile forum wengi wanakimbia kufuru.
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  :D :D :D :eek: LOL!
   
 13. J

  Jitume Senior Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magobe T

  Umeeleza vizuri sana,na ni kama ulikuwepo.

  Wachangiaji wengi watakuwa hawajui issue nzima kuhusihana na sakata la Karugendo. Bila hata kusikiliza upande wa pili, ukipitia makala zote za Padre Karugendo tangu wakati ule wa gazeti la Rai (chini ya J.Ulimwengu) na baadaye gazeti la Raia mwema hadi makala ya wiki hii kuhusiana na uhusiano wake na viongozi wa Jimbo lake utabaini Padre Karugendo ni mtu wa namna gani.

  Binafsi sijasoma gazet la Kiongozi, lakini kama ulivyosema mengi hayakusemwa kwa ajili ya heshima ya Kanisa na Padre mwenyewe na ni jambo zuri.

  Karugendo kwenye maandiko yake hayo amewahi kueleza jinsi alivyoombwa na watu wengi, marafiki kwa ndugu kuwa mpole na kutoendeleza mafundisho yaliyo kinyume na sheria za kanisa lakini pia kuendeleza malumbano na viongozi wa kanisa. Sijui kwanini mtu mwelevu kama yeye alipuuza ushauri huu wa msingi na manufaa makubwa kwake. Ulikuwa ni ushauri si kwa ajili ya kulinda heshima yake pekee lakini na ya viongozi na mapadre wenzake!!

  Binafsi nimeishi Ngara, Jimbo la Rulenge kwenye kindi cha mwishoni cha maisha na uhaskofu wa Marehemu askofu Mwoleka ambaye aesifiwa na kuelezwa vizuri na Karugendo katika makala zake nilizotaja. Nilikutana naye wakati wa uhai wake pale Rulenge, nilimfahamu. Alikuwa mpole, mnyenyekevu,mbunifu rafiki wa kila mtu na kwa hili hakuwa na mipaka ya dhehebu. Kipindi chake cha mwishoni alikimaliza akiwa na matatizo ya afya tena kwa kipindi kirefu. Kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wenzake mapadre walikitumia kipindi hiki na upole wa Askofu huyo vibaya, vibaya sana.

  Karugendo analijua hili. Kila padre na hasa waliokuwa viongozi wa Idara mbali mbali, alifanya anavyotaka!! Leo hii ukienda pale Rulenge na Bushangaro (Jimbo jipya sasa) na kudadisi maisha ya watawa kipindi hicho hata kabla ya ujio wa Askofu wa sasa, ukawadadisi waumini wa kawaida, utapata picha ya nini kilichokuwa kinamsononesha Mwoleka kwenye siku zake za mwisho,inawezekana na hayo aliyotaja Karugendo (Raia Mwema) ni mojawapo. Lakini mapungufu ya kibinadamu yaliyofikiwa na wasidizi wa Mwoleka wakati huo yalimtia simanzi kila mwumini na hakika Askofu Mwoleka mwenyewe. Kipindi hicho walishamshinda kuwatawala,walimtawala.

  Askofu wa sasa simfahamu vizuri,bila shaka naye kama binadamu wengine wote ana mapungufu yake. Lakini ukipitia maandishi ya Karugendo utaona kuna kukiri maungamo yake kwa Askofu ambayo anadai askofu aliyatumia kumwadhibu. Maandishi ya Karugendo hayana lugha ya unyenyekevu baada ya maungamo, hayana mwendelezo wa kutubu na kuungama. Ni picha ya ubabe na ushindani kama kupadirishwa wakati Askofu wake ni mwanafunzi pale Ntungamo!!!.

  Kalugendo hakuwa peke yake kwenye mapungufu hayo, ni wazi wenzake waliungama na kuendeleza maungamo na unyenyekevu. Ninafahamu kila mmoja na maisha aliyoishi, baadhi wametangulia mbele ya haki na haya yalitokea hata kabla ya kujulikana ni nani atamrithi Mwoleka. Waumini wa Rulenge na Kalugendo kama hawawi wanafiki wanafahamu ukweli huu.

  Kuna wakati jimbo lilikaribia kufirisika kwa sababu ya mapungufu ya wasaidizi wa Mwoleka.

  Kwa kuwa mimi si mwumini wa dhehebu hilo, haitakuwa vyema kutaja ni nani aliongoza kitu gani na alifanya nini cha kuwaacha midomo wazi waumini na jamii nyingine jimboni humo. Namuheshimu Karugendo timu nzima aliyokuwa nayo wakati huo.

  Hakuna Askofu yeyote angekuja na kukuta jimbo katika hali ile na akakaa kimya!!! Karugendo mwenyewe angekuwa katika nafasi ile asingekaa kimya.

  Waliomtaka Kalugedo kukaa kimya na kuacha marumbano wana uelewa mzuri wa hali ilivyokuwa wakati ule. Hawa walikuwa na busara, wana nia njema na Karugendo.

  Karugendo ni mtu mwenye kipaji, mjuzi na mwenye karama ambayo akiitumia vizuri mahala pazuri na muda muwafaka jamii itanufaika kuliko anavyofikri yeye. Akianzisha NGO,kama shule,watu wana mahitaji ya shule kila mahala,mashamba watu watanufaika na kipaji chake. Na anaweza, anafahamiana sana na ana marafiki kuliko kuwekeza kwenye malumbano ambayo yatasababisha mgawanyiko wa watawa jimboni kwake na hata kuhatarisha usalama wao au wa taifa.

  Kanisa Katoliki lina heshima ya pekee duniani, nchini na jimboni Ngara na Karagwe(Jimbo la Rulenge la wakati ule). Askofu Mwoleka ameacha miradi mingi inayowanufaisha wananchi wote (Si wakatoriki tu) hii ni pamoja na hospitali Bushangaro,Ngara, Rulenge n.k. Mashule Rulenge, Katoke, Ntungamo ndogo,Bushangaro nk. Mradi wa mshikamano aliouanzisha ulishindikana hata kabla ya ujio wa Niwemugizi. Karugendo analijua hili, si kumtendea haki askofu wa sasa kudai ameuharibu. Haukupokelewa na jamii kama alivyokusudia Mwoleka. Kumlaumu Askofu wa sasa ni sawa na Kuwalaumu Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwa kushindwa ujamaa, huu ulikufa Nyerere angalipo!!

  Ask.Niwemugizi mbali ya kuendeleza huduma hizi za kijamii alizozikuta, ameanzisha miradi mingine huko Karagwe, Ngara hadi Chato.

  Karugendo ni mwandishi mzuri, lakini naamini kalamu yake anaielekeza kumlida yeye kwenye swala hili. Bahati mbaya maandishi yake ni waumini wachache wa majimbo hayo wanaopata nafasi ya kuyasoma. Yanaishia kwetu tulioko mijini na kuona picha ya upande mmoja!!! Kama ulivyosema hatujapata picha ya upande wa pili kwa sababu ya taratibu za kanisa.

  Inawezekanaje Karugendo aandike barua kwa Askofu wake, Kardinali, kwa Papa ambako yeye alihakikisha imewafikia Rome na wote wasimjibu!!

  Karugendo ni binadamu kama mimi na wewe, ni vyema, haki na faida kwake, jamii, rafiki zake, akarudi nyuma na kusikikiliza ushauri wa marafiki na ndugu zake wa kuwa mpole ili tunufaike naye. Hatuwezi kunufaika naye kwa mtizamo alionao sasa. Hata yeye hatonufaika na msimamo kama huo.

  Ni mawazo yangu.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mambo yaliyofanya atolewe kanisani ata nami nayakubali ila kosa alilofanya kila institution ina misingi na kanuni zake and you need to adhere to these rule and regulations zikikushinda achana nao tena hasa mambo yanapohusisha imani.
  Ila kanisa nalo laitaji kulainisha baazi ya mambo?
  Vishawishi vingi siku izi!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Swali moja la msingi sana ambalo wengi bado hatujapata jibu ni kwamba , je ni kweli Fadher alivunja kanuni za useja kama zilivyoelezwa hapo juu? Hamna anayetoa jibu hili, kila mtu anazunguka tuu. Kama ni kweli basi hastahili kuwa kupewa kondoo achunge. kwa hili simtetei.

  Lakini je pia kanisa lilimemtendea haki kipindi chote alichokuwa amesimamishwa bila kumpa matunzo ? Askofu wangu hapa alisimamishwa uaskofu kwa sexual acts on minors lakini analipwa pension na yupo katika nyumba za walei anakula raha, hapa ninakubaliana na Padri kuwa kuna double standards kwa mapadri wa Africa na Ulaya / US, kama alivyowahi kusema katika makala zake.
   
 16. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2009
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Makanisa mengi yametoka Roman Catholic eg Lutheran,Anglican etc due to various reasons of which they believe they are right, no wonder if they will keep running way due to the fact that they are not able to comply RC's Law&regulations .
   
 17. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeongea ukweli na kweli tupu. I mean no better words could deliver what you have written.

  Kifupi tuu: Kwa wanaomjua Mwoleka (RIP) ni kwamba afya yake alianza kudorora in early 1990s na mapadre wengi wakatake advantage. Ni ukweli usiopingika hata ungekuwa Niwemugizi lazima ungetake drastic measures. Akina BOSCO, BAMBARA, HERMANI, BENEZETI, KAZAWADI (RIP) NA WENGINE WENGI..Walilitumia jimbo kama personal property. Huu siyo mda wa kuanza kulaumiana ila mkuu kwa kweli umetoa picha halisi...na umenikumbusha mbali sana....

  Anyway Karugendo kama anakuja humu..basi asome hii post. Akifuata yaliyomo humu..hakika atabadilika na atakuwa na amani kabisa.

  Masanja,
   
 18. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  shukrani mkuu Jitume kwa maelezo murua kabisa.Wakuu mamods tafadhali kama itawezekana muirudishe ile nyingine na muiunganishe na hii manake kule mlikoiweka kila mtu anapaogopa kuingia!
   
 19. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Du ntaisoma vizuri kwa uhuru zaidi ngoja kwanza nimbembeleze mtoto hapa alale
   
 20. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2014
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,217
  Likes Received: 8,292
  Trophy Points: 280
  afutwe uaskofu kilaini.
   
Loading...