Sababu za kufeli sera ya ruzuku ya pembejeo za kilimo. Serikali ikune kichwa upya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za kufeli sera ya ruzuku ya pembejeo za kilimo. Serikali ikune kichwa upya...

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mwanakilimo, Oct 25, 2011.

 1. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naishi mjini, wala si mkulima kwa practice, bali kwa taaluma.

  Mwaka jana kuna mbolea ya ruzuku 'ilikuja' mtaani kwetu nami nikajipati mfuko mmoja UREA na miwili ya DPP. Nilichukua nikaweke kwenye maua yangu.

  Ukweli ni kwamba mpango wa serikali wa ruzuku ya pembejeo ni total failure. Sina uhakika kama serikali iliamua kwa makusudi kuplan na ku-implement mpango mbovu kiasi hicho, lakini nachojua ni kuwa kama objective yake ilikuwa kuongeza tija katika kilimo, then haijafanikiwa hata 20%. Kama objective ilikuwa siasa, then hapo sina comment...

  Kwa ushauri tu wa mwanzo kwa serikali, kama kweli wanataka kusaidia kilimo na kumsaidia mkulima nchi hii, then wanatakiwa wawe na majibu ya ndiyo katika maswali yafuatayo...

  1. Je, serikali ina orodha (register) ya wakulima wa mahindi, wa mtama, wa mihogo, wa kahawa, wa korosho, wa chai, wa tumbaku, wa pamba, wa kunde, wa viazi, wa ufuta, wa alizeti, wa pareto, wa vanila, wa ndizi, wa nyanya, wa vitunguu, wa mchicha, wa tikiti, wa mazao yote yanayolimwa hapa nchini?

  2. je, serikali inajua mkulima x mwaka jana alilima mahindi ekari ngapi, alivuna ekari ngapi, mwaka huu kalima ngapi na mwaka ujao atalima ngapi?

  3. Je, serikali inajua mkulima x ana ekari ngapi za ardhi ya kilimo cha mvua, na ngapi za ardhi ya kilimo cha umwagiliaji, anaweza kulima ngapi kwa mwaka, na ni kwa nini hawezi kulima ngapi?

  Lengo la maswali yangu ni kutaka kuipa serikali ujumbe kuwa inatakiwa kuratibu kwanza shughuli za kilimo nchini, ili iweze kusaidia na kukuza kilimo. Serikali inatakiwa iwe na register ya wakulima wote nchini, mahali walipo, mazao wanayolima, ukubwa wa ardhi yao na aina ya kilimo wanachofanya. Kwa utaratibu huu ina maana kama kuna mtu anayelima mahindi, anatakiwa ajiorodheshe serikalini, aseme analima akari ngapi, ni shamba lake au la kukodisha n.k...

  Serikali inatakiwa iratibu idadi ya ekari za zao fulani zilizolimwa mwaka husika, zililimwa wapi na mazao yalikuwaje... Serikali inatakiwa ifahamu mathalani mkuliwa y ana miti mingapi ya kahawa, au ya korosho na inahitaji mbolea ipi na kiasi gani, na uzalishaji wake ukoje...

  Mtu unaweza kudhani ni kazi ngumu kwa serikali kufanya mambo haya lakini wka maendeleo ya teknolojia tuliyo nayo kwa sasa ni kazi rahisi mno. Serikali inaweza kuwa na majina yote ya wakulima wake, na pale itakapoamua kugawa mbolea ya ruzuku wka mfano, then wanajua mbolea kiasi fulani imeenda kwa fulani, na wanaweza ku crosscheck kwa kuwasiliana kwa simu na wakulima kadhaa (siku hizi asilimia kubwa ya wakulima wana simu), na kama ikionekana kuna tatizo eneo fulani, then mtendaji aliyekuwa responsible eneo hilo anafuatiliwa...

  nina mengi sana na naamini wanajamvi pia mna mengi ya kuishauri serikali katika kuboresha kilimo Tanzania...
   
 2. Zurie

  Zurie JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2016
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 964
  Likes Received: 1,623
  Trophy Points: 180
  Kwakweli kilimo kwa serikali hii si kipaumbele. Sisi ni taifa la viwanda. Hoja yako ni nzuri ila utekelezaji wake sio wa muda mfupi. Inaweza kuchukua hata mwaka.

  Kingine kikubwa nilichoki'grab' kwenye hoja yako ni ubadhirifu wa wanataaluma wa kilimo. Mifuko 3 hiyo kuna mkulima angeitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na sio maua.
   
 3. Alfan issa

  Alfan issa JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2016
  Joined: Dec 26, 2015
  Messages: 2,020
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Kabisa, ye anaeka kwenye maua
   
 4. Interest

  Interest JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2016
  Joined: Apr 11, 2015
  Messages: 935
  Likes Received: 1,259
  Trophy Points: 180
  Kilimo cha maua nacho kina tija yake, usimbeze.. Maua ni biashara, ni pesa, ni pato endapo tu litafanywa kwa scale kubwa na ya kibiashara zaidi. Unajuaje yeye hafanyi hivyo?

  Anyway, nchi hii asilimia kubwa watu wanalima, lakini mambo hayaendi kwa sababu wenye dhamana hawako serious kukuza uchumi kupitia kilimo, yanapigwa maneno matamu tu na sera zisizotekelezeka.

  Rais Magufuli sasa aruhusu ziara za nje za viongozi kwa masharti ya kujifunza na kuja kufanyia kazi waliyojifunza huko (mfano China au Italia ambako ni mafundi wa kilimo).. Ole wake atakayeshindwa kuleta tija, atarejesha gharama zote za safari!

  Magufuli pita hapa please.
   
 5. miss zomboko

  miss zomboko JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2016
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 1,273
  Likes Received: 2,053
  Trophy Points: 280
  Tatizo serikali yetu ina juhudi sana katika kuanzisha vitu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo lakini utekelezaji mbovu ndio unaofanya miradi mingi ya maendeleo inakufa halafu mwisho wa siku tunaanza kutafuta nani mchawi kumbe ni sisi wenyewe. Kila mtu akiwajibika kwa nguvu zote kutekeleza majukumu aliyopewa tutafika mbali sana.
   
 6. real G

  real G JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2016
  Joined: Feb 7, 2013
  Messages: 4,796
  Likes Received: 4,449
  Trophy Points: 280
  Kilimo Tanzania kinaonekana kama ni shughuli isiyo na tija na hata mtu akiwa na mtaji anawekeza kwenye mambo mengine
  Hii ni kwa sababu masoko yake hayaomeki,
  unaweza ukalima ila ikitokea ilikuwani msimu mzuri basi imekula kwako mazao yanashuka bei na hakuna viwanda vya kuyaongezea thamani, kuhifadhi ni ngumu pia kutokana na teknolojia duni, pia kuuza nja huruhusiwi ukiwa na mazao mengi, unatakiwa uikopeshe serikali, tena bila riba!
  Njia nzuri ya kufanya kilimo kivutie kwa watu ni kuandaa soko zuri kwa mazao ya wakulima, hii itawapa moyo watu wengi kwenda kulima wakijua hakuna riski ya soko
  Pia wanatakiwa kujenga dykes na mabwawa kwa ajili ya kuhifadhia maji ya mvua kipindi cha masika ili kiangazi watu walime pia
   
 7. Chachu Ombara

  Chachu Ombara JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2016
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 5,119
  Likes Received: 5,049
  Trophy Points: 280
  Sina imani na Serikali kuhusu kuinua kilimo cha mkulima mmoja mmoja tokea tupate uhuru. Nadhani serikali suala la kilimo ambacho ni tegemezi kwa watanzania 80% + hawakipi kipaumbele, wanafanya tu basi.

  Kama wameshindwa kutatua tatizo la ugonjwa wa mnyauko Kagera unategemea nini? Wenzetu Uganda wameweza kwanini sisi tushindwe? Tanzania hii ina matatizo sana.

  Nimeshangaa wilaya ya Karagwe kukumbwa na baa la njaa!! Inachekesha sana. Wilaya ile ina udongo wenye rutuba na mvua za kutosha ila serikali imewatupa wakulima wadogo wadogo mpaka majanga kama haya yanatokea.

  Serikali inabidi iwape kipaumbele wakulima wadogo wadogo, pembejeo za kilimo zimekuwa ghali kwasababu ya walanguzi hapo kati.

  Bei ya mazao hairidhishi kabisa na wakulima wanazuiwa kuuza mazao nje ya nchi wakati wanajua wanawanyonya sana wakulima.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 8. RUCCI

  RUCCI JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2016
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,696
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Ukiamua kuingia kwenye kilimo kama unategemea Serikali ikusaidie sidhani kama utafanikiwa. Kwenye kilimo ni kujitoa mhanga kwenye nchi hii, either unawaza ukalamba mamilioni au ukabakia maskini sababu serikali ndio regulator wa bei za mazao, Kama sasahivi wakulima wa tumbaku wanalalamikia bei, wamelima lakini bei hailipi, So conclussion yangu kilimo ni kizuri but it's a very big risk in Tanzania and Africa as a whole.;)
   
 9. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2016
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,904
  Likes Received: 4,760
  Trophy Points: 280
  Kilimo kwa hapa kwetu Tanzania kiko kwenye midomo ya viongozi/ Wanasiasa lakini hakuna mikakati thabiti ya kukuza kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Mkulima na Taifa kwa ujumla.

  Serikali kila mara imekuwa ikileta kaulimbiu mbalimbali na sera lukuki lakini unapokuja upande wa utekelezaji ndiko tatizo linaanza. Mfano taifa hili limesikia na kushuhudia kaulimbiu na sera mbalimbali kama;

  1- Siasa ni Kilimo
  2- Kilimo ni uti wa mgongo
  3- Kilimo Kwanza
  4- Big Results Now (BRN)

  Na kauli mbiu nyinginezo, sasa unaleta kaulimbiu ya Kilimo Kwanza lakini wakulima wanapewa Power tiller hakuna Agrarian Revolution itakayotokea kwa kutumia Power Tillers

  Serikali hivi majuzi imeleta makakati wa Big Results Now hapa pia ilithibitika ni kwa kiasi gani serikali inavyocheza na sekta ya kilimo huwezi kusema unataka kueta matokeo makubwa sasa ikiwa hakuna mikakati ya awali ya kuleta matokeo hayo unayoyahubiri.

  Kwani maendeleo ya Kilimo ni kama unaunga chumvi kwenye mboga? kwamba ukiweka chumvi kisha ukakoroga ukaonja ndio tayari?

  Kwa mataifa yaliyoweka umakini katika Kilimo wamefanikiwa kukomesha njaa na kuwapa ajira ya uhakika wakulima sasa hapa kwetu mkulima ni mtu fukara wa kutupwa.

  Mtu akiwa hana kazi ya kufanya anaambiwa aende akalime kwani kilimo ni cha watu wasio na kazi?

  Kilimo ni sekta iliyojifia..........
   
 10. Donatila

  Donatila JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2016
  Joined: Oct 23, 2014
  Messages: 2,236
  Likes Received: 2,221
  Trophy Points: 280
  Serikali inaweza kufanikisha kwa Kilimo kama itakuwa na 'usimamizi makini', nionavyo mimi ufuatiliaji umekuwa zero, mfano mbolea na mbegu zimekuwa haziwafikii wakulima kwa wakati...hii yote ni kwasababu ya usimamizi mbovu, wakati mwingine mbolea hizo ni bure wao wanatakiwa watoe fedha, Pili wataalam wa kilimo wanakaa mijini na wakati wanatakiwa wakae karibu na wakulima ili waweze kupata elimu kuhusiana na kilimo.

  Mi naoa Serikali inafeli kwakuwa haina 'usimamizi makini'
   
 11. k

  kirerenya JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 27, 2013
  Messages: 1,332
  Likes Received: 1,745
  Trophy Points: 280
  Ishu ni kwamba vitu vimekuwa vikiendeshwa kwa maneno tuu, utekelezaji umekuwa mdogo mno.
  Nakumbuka toka enzi za mwalimu kumekuwa na kauli mbiu nyingi za kuinua kilimo kama vile; Siasa ni kilimo, Mapinduzi ya kijani, Kilimo ni uti wa Mgongo wa Taifa na hata kipindi cha Kikwete tukaja na kaulimbiu mpya ya Kilimo kwanza.

  Ukijaribu kuchunguza kaulimbiu hizi kwa makini utagundua kuwa nyingi ni za kuiga na kukurupuka, pia zimejawa na siasa ndani yake bila uhalisia. Kiongozi anatembelea nchi fulani anakuta wamepiga hatua fulani, bila kutumia wataalamu na kuelewa kwa undani kwamba wamefanyaje, yeye anakopi ile idea anakuja nayo na kuanza kuitekeleza.

  Kama tunataka mapinduzi ya Kweli ya kilimo; Ni lazima serikali itulize kichwa, ifanye utafiti kujua tulikuwa tunakosea wapi kila mara alafu tuje na mikakati mipya ya kufanya kilimo kwa matendo na siyo kwa kuongea tuu. Pia bajeti ya Kilimo iwe inatosheleza.

  Japo tunalenga kuwa na serikali ya viwanda lakini bila kilimo, malighafi itatoka wapi? hizi sekta mbili lazima zikuwe pamoja.
  Naomba tuyafanyie kwanza haya kazi
  Asanteni
   
 12. r

  rsvp JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2016
  Joined: Dec 13, 2012
  Messages: 554
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Kilimo kimeingiliwa na maagizo ya siasa.
  Mkulima anakatazwa asiuze mazao nje ya mkoa hata nje ya nchi eti atapata njaa.
  Hali hii inawavunja moyo hata wale wenye nia na mtaji wa kufanya shughuli za kilimo
   
 13. H

  Hwasha JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2016
  Joined: Aug 22, 2015
  Messages: 1,281
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  Inaelekea nina tatizo au wachangiaji wengi wa JF hawaelewi cha kuchangia na namna ya kuchangia.Mchangiaji makini hawezi kushauri watu wazalishe mazao wasi

  o na uhakika watauza wapi ila wasubiri serikali iwatafutie soko la wanachozalisha.

  Yapo maswali rahisi ,ya msingi ila ya lazima kwa kila mzalishaji.Jiulize nizalishe/nilime nini? nitauza wapi? lini nitauza? nitatunzaje/nitahifadhi namna gani? Ukijiingiza kuzalisha ukitegemea serikali au watu wengine wakushauri baada ya kuzalisha uuze wapi na biashara hiyo ikulipe unaota ndoto za alinacha.

  Lengo la ruzuku ni nini? kuongeza chakula au kuongeza kipato kwa mkulima? Marehemu mama yangu alinufaika na Sasakawa Globe 2000,aliwezeshwa kuzalisha gunia 33 za mahindi kwa ekari.Huduma za ziada alizopewa ni pembejeo kwa wakati,alikopeshwa pembejeo,alipewa huduma za ugani hatua kwa hatua.Mradi huu ulifadhiliwa na Marekani.Mradi ulipoisha mama hakuweza kumudu gharama za uzalishaji.Mbinu zote na hatua za kupita alizijua,aina ya mbegu alizijua.Alipokosa pembejeo za mkopo na kutakiwa kulipia kila pembejeo anapoihitaji vikawa vikwazo kwake.Akapunguza baadhi ya pembejeo akarudi kwenye kiwango walichomkuta nacho Sasakawa yaani gunia 20-25 kwa ekari.

  Kiwango hiki ni chini mno kulinganisha na gunia 33 kwa ekari japo bado wakulima wengi Tanzania hawajakifikia ukiondoa Mikoa ya Iringa,Ruvuma,Mbeya na Rukwa (jumlisha na mikoa mipya iliyokiwa sehemu ya big four).Ruzuku ilipoanzishwa imeleta maumivu kwa nchi badala ya tija.Watumishi wengi wameitumia kuiba.Vigezo vya kupata wanufaikaji vimekuwa na utata mkubwa,kwa asiyeelewa tafuta vigezo vya Sasakawa linganisha na vya ruzuku ya pembejeo kisha linganisha matokeo yake.

  Tija si ruzuku tu mpe mkulima maarifa ya kuchagua alime nini,mwachie uhuru wa kuuza anapotaka bila vizuizi,achana na wakuli
  ma wa mitandoni kama JF,kupanga vigezo usitumie vya wataalam wa amakaratasi tu pata ushauri wa wakulima halisi,boresha,simamia kwa ukali wa JPM. Matokeo tutakayoyapata yatatushangaza wenyewe.Tukiendekeza siasa na matakwa ya wahuni walio katika vyama vya siasa,serikalini na taasisi za fedha hadi wazungu watuambie cha kufanya tutakuwa tunaendeleza vichekesho
   
 14. real G

  real G JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2016
  Joined: Feb 7, 2013
  Messages: 4,796
  Likes Received: 4,449
  Trophy Points: 280
  Watu wengi wanalima, wengine wamelima kisha wamekimbia, kinacho katisha watu tamaa kulima ni kuwekeza nguvu nyingi kisha kuja kuuza kwa bei isiyoendana na nguvu waliyowekeza, na hili linatatuka tu endapo serikali ikiamua
  Kutoa ruzuku au msamaha wa kodi kwa vipuri vya viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ingeaidia sana, maana mazao badala ya kuuzwa bei chee kipindi cha mavuno na kukatisha watu tamaa, yangeweza kuwa processed na kuongezewa thamani na kuuzwa hapa nchini badala ya kuagiza vitu kama tomato, mafuta, vyakula vya ngano n.k kutoka nje, pia tungeweza ku export na hii ingewatia watu moyo sana
  Kma kuna mmoja aliyeweza usidhani wakulima wengi wana uwezo wa huyo mtu mmoja uliyemtolea mfano
   
 15. H

  Hwasha JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2016
  Joined: Aug 22, 2015
  Messages: 1,281
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  Hoja kubwa ya akili kuwa inaleta tija kubwa naafikiana na wewe.Wakulima nao washauriwe kabla serikali haijafika huko wapange mapema mazao ya kulima wakiwa wamesoma hali ya soko na kipindi sahihi cha kuzalisha.
   
Loading...