Sababu za kitaalam zinazosababisha mzazi asinyonyeshe mtoto

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,359
Hello
Kwa wataalamu wa afya ningpenda kujua ni sababu gani zinamfanya mzazi akatazwe kunyonyesha mtoto ukiacha ya HIV ambayo ndio pekee naifahamu.

Leo nimeshangazwa kuona mzazi hanyonyeshi tena mtoto sababu anasema maziwa yake ni machafu hivyo ameshauriwa ampe mwanae maziwa ya ng'ombe au kopo, na akasema ni jambo la kawaida kwa wazazi wengi.

Je ni kweli ni jambo la kawaida?

Sababu ni nini inayosababisha mzazi akatoa maziwa machafu ambayo sio afya kwa mtoto mpaka akatazwe kunyonyesha ila mtoto bado ni mchanga?
 
Maziwa machafu????
Sio ana HIV na hawezi kusema ukweli?
Nina hisi hicho ila anadai mtoto akinyonya anatapika hivyo hospitali wamemkataza kunyonyesha na anasema kaambiwa ni jambo la kawaida, ila me i doubt ndio maana nimejaribu kuuliza humu kama kuna mtu ashawahi sikia hii kitu.
 
Namie nasubiri elimu ya maziwa machafu
 
Back
Top Bottom