Sababu za CHADEMA kushangilia kurudi kwa mafisadi CCM ni zipi?

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,701
15,149
Kwa akili zao wanajua hapo Chadema ipo madarakani sasa na watashitukia 2025 hii hapa wanapokea kipigo kikali tena.
CCM mpya ya awamu ya tano haikuishia kuongoza kwenye kuwaletea maendeleo watanzania tu mbali iliongoza pia kwenye kutoa misamaha ya dhati kwa wanachama wake waliofanya makosa mbalimbali kwenye chama kipindi hicho.
Miongoni mwa misururu ya wanufaika wa misamaha hiyo ni pamoja na makamu mwenyekiti mpya bwana KINANA, wengine ni Nape, Makamba, Ngeleja, Sofia Simba etc.

Kwa hiyo porojo zinazoenezwa na wanasiasa uchwara waliofilisika kichwani wa CHADEMA kwamba CCM ya Dk Bashiru, Dk Magufuli na Polepole iliongoza kwa ukatili wa kufukuza watu siyo kweli na ushahidi upo hadharani

Hivi ulishawahi kukaa na kujiuliza taifa la Tanzania lingelekea wapi bila ujio wa hayati Magufuli kama rais?

Hivi ulishawahi kujiuliza kama Magufuli angefariki kwenye mwaka wake wa kwanza wa urais kingetokea nini?

Kama leo baada ya hayati Magufuli kukaa madarakani kwa miaka 6 kuna watu wanakuja kuponda miradi ya ndege, SGR, Bwawa la mwl Nyerere je vipi kama angeisaini tu na kufariki dunia hao wapondaji wangesema nini?

Vipi kama Magufuli angefariki kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020 si Chadema wangezusha kwamba Magufuli amekimbia kipigo cha Tundu Lisu kwenye sanduku la kura?

Leo Corona imepuuzwa duniani kote na sasa wananchi wote wanafuata falsafa za hayati Magufuli lakini bado kuna baadhi ya Chadema wanashupaza shingo na kupuuza misimamo ya Magufuli, je ulishawahi kujiuliza ingekuwaje kama Corona ingeingia Tanzania tukiwa hatuna Magufuli?

Mungu alimtuma Magufuli kutuvusha kisha akamchukua na kwenda zake


 
Acha kukufuru mkuu. Kwani Magufuli ndiye aliyeifanya corona isiwe tishio Tanzania? Mungu anaipenda Tanzania ndiyo maana corona haijatusumbua sana.

Jiwe alichofanya ni kutunyima data halisi za athari ya corona tanzania. Watu waliendelea kufa ila ashukuriwe Mungu vifo havikuwa vingi sana Tanzania ukilinganisha na majirani zetu.
 
IMG-20220331-WA0670.jpg
IMG-20220331-WA0661.jpg
 
Ingawa ulichokiandika hakina uhusiano na kichwa chako cha habari,ila nikijibu kutokana na heading yako ni kuwa,inawezekana kabisa uongozi wa kina Kinana na kina Nape chini ya Mwenyekiti Kikwete haukuwa mwiba sana kwa CHADEMA kama ulivyokuwa kwa akina Polepole na Bashiru chini ya Magufuli.
 
Acha kukufuru mkuu. Kwani Magufuli ndiye aliyeifanya corona isiwe tishio Tanzania? Mungu anaipenda Tanzania ndiyo maana corona haijatusumbua sana.

Jiwe alichofanya ni kutunyima data halisi za athari ya corona tanzania. Watu waliendelea kufa ila ashuriwe Mungu vifo havikuwa vingi sana Tanzania ukilinganisha na majirani zetu.

Jibu zuri sana
 
Ingawa ulichokiandika hakina uhusiano na kichwa chako cha habari,ila nikijibu kutokana na heading yako ni kuwa,inawezekana kabisa uongozi wa kina Kinana na kina Nape chini ya Mwenyekiti Kikwete haukuwa mwiba sana kwa CHADEMA kama ulivyokuwa kwa akina Polepole na Bashiru chini ya Magufuli.

Hapana kipindi Cha Magufuli dola iliingia nzima nzima kupambana na upinzani, kuanzia bunge, mahakama, NEC na polisi.

Ndio maana Lissu alipigwa risasi, polisi hawakuchunguza, bunge likamfukuza Lissu na mahakama ikasema haiwezi kuingilia bunge.
 
Back
Top Bottom