Bunge letu, kikatiba ni chombo muhimu sana, na ni miongoni mwa mihimili mitatu ya Taifa. Bunge siyo club ya mpira. Bahati mbaya, wabunge wengi wa Bunge letu la sasa, inaonekana hawatambui hadhi ya Bunge, nguvu ya Bunge na majukumu muhimu ya Bunge.
Hivi sasa tunashuhudia Bunge ambalo kwa vigezo vya chombo cha uwakilishi, kukosa umaana. Bunge limekuwa likitumia muda mwingi kujadili mambo yasiyo na tija kwa Taifa na wananchi.
Bunge kwa sasa, kwa mtazamo wa baadhi ya wananchi walio wengi, imekuwa ni chombo cha kutafuna pesa za umma bila ya umma kunufaika na chombo hicho. Bunge limekuwa kama club ya mabishano, mahali pa kupigana vijembe, kutoleana masimango, mahali pa kufanyiana kejeli, kuumbuana, na mahali pa kufanyia ushabiki.
Kutokana na mwenendo usio na tija wa Bunge la sasa, hata Mh. Rais amevumilia lakini baadaye ameshindwa, akalazimika kutoa neno. Ni aibu kubwa kwa wabunge wenyewe, ni aibu kwa Spika na aibu kubwa zaidi kwa Bunge zima kama mhimili.
Mara nyingi, uimara au udhaifu wa kitu hutokana na uanzishwaji wake na upatikanaji wake. Kama ulikuwa unapita jirani na bar, ukamwona msichana mrembo pale bar, ukavutiwa naye, na baadaye ukamchumbia na kumwoa, usishangae kuwa na mke mlevi.
Maana ulitakiwa kujiuliza pale bar alikuwa anatafuta nini, kabla unamchumbia.
Bunge letu ni matokeo ya sheria, kanuni na taratibu zetu mbaya zinazotuongoza namna ya kumpata Mbunge, na sifa za yule anayeutaka ubunge.
Karne hii, bado tuna sheria zinazosema elimu ya Mbunge ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), wakati dereva wa gari la serikali, sifa yake mojawapo ni kwamba angalao awe amemaliza kidato cha nne. Ndiyo maana haishangazi kuona watu ambao walitakiwa kwenda kwenye taasisi za kufuta ujinga, kwa Tanzania, wapo Bungeni tukitarajia watunge sheria za kuendeleza elimu wakati wao wenyewe hawana elimu.
Upatikanaji wa wabunge wa Bunge la sasa, ilikuwa ni mchakato mchafu kuliko mchakato wowote uliowahi kuwepo katika Taifa hili. Bunge hili, ni bunge la chama kimoja, CCM.
Huko CCM, mchakato wa kuwapitisha wagombea ulikuwa magumashi na uchafu wa hali ya juu. Maeneo mengine, mtu aliyepata kura za mapendekezo zaidi ya 300 aliachwa, alipewa mtu aliyepata kura 3.
Kwenye uchaguzi mkuu, wagombea wa vyama vingine walifutwa bila sababu yoyote ya msingi. Waliobakizwa, ushiriki wao uliofanywa kuwa wasindikizaji katika mchakato ambao Tume ya Uchaguzi walikuwa na maelekezo ya kutomtangaza mgombea asiye wa CCM.
Tunaweza kupinga kwa sababu ya ushabiki, lakini ni ukweli usiopingika kuwa Bunge hili ni Bunge ambalo wabunge wake waliteuliwa na kupitishwa na mtu mmoja, na zaidi kwa kuangalia watu hao wana uwezo wa kumsifu kwa kiwango gani. Na siku zote watu wanaopenda kusifu sana, ni wanafiki na watu wenye uwezo mdogo kifikra. Mwenye akili kabisa na uwezo unaojitegemea, hawezi kukubali kufanywa mtu asiye na mawazo ambaye kazi yake ni kusifia tu.
Kutarajia kupata tija yoyote kutoka kwenye Bunge hili, ni kusubiria embe chini ya mchongoma.
USHAURI
Turudi kwenye mchakato wa katiba mpya. Na kwenye kipengere cha Bunge, mapendekezo yangu:
Kwanza kwa aina ya wabunge hawa tulio nao, hata kama tusingekuwa na Bunge kabisa, hakuna kitakachobadilika.
Tuwe na Bunge ambalo lina wabunge wanaotokana na mikoa. Kila mkoa wabunge wawili. Hivyo, Bunge zima lisizidi wabunge 100. Sifa za hao wabunge zifafanuliwe vizuri ili kuepuka wabunge wanaojua KKK tu, wa aina za akina Kibajaji, Musukuma, Japipo, n.k.
Na Spika naye sifa zake zifafanuliwe, na sifa mojawapo ni kuwa aliwahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au mwenye sifa zinazomwezesha kuwa jaji wa Mahakama Kuu.
Baraza la Mawaziri litokane na watu wasiokuwa wabunge ili Rais awe na uwanja mpana wa kuwapata watu wenye uwezo wa kumsaidia katika kuendesha Serikali.
Rais apeleke majina mawili Bungeni ya watu wasiokuwa wabunge kwaajili ya kumpata Waziri mkuu. Waziri Mkuu ni yule ambaye atapata zaidi ya theluthi 2 za kura za wabunge. Akikosekana aliyepata zaidi ya theluthi 2, Rais apeleke jina la tatu, na wote watatu wapigiwe kura na wabunge. Waziri mkuu awe yule aliyepata zaidi ya 50% ya kura.