Sababu za Bunge kushindwa kumng'oa Bashite na kaka yake

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Watu wengi wataendelea kubaki kama fisi kungoja mkono udondoke, na safari hii tutashangazwa tena! wengi mmewekeza katika Bunge, mkidhani kuwa kila kitu kitatokea automatically.
Hali hii ya kusubiri kudra au maamuzi ya mtu mmoja ndio yametufikisha hapa leo!
Bashite alipokuwa akilialia ni ukweli kabisa alishakata tamaa na kaka yake naye alisha-give up, ila kwa vile tulionesha hofu through social media, kwa vile tulishajadili kama yeye ndiye mwenye mamlaka ya mwisho na kwa vile walishatikisa hadi Dodoma ndani ya wiki hiyohiyo, level yao ya confidence ikawa inaongezeka na mwisho wakatenda waliyotenda!
sasa kuelekea Mjengoni hiyo April, hawa jamaa hawajakaa kama mamburula, naamini hadi sasa watakuwa wanajipanga jinsi ya kuumaliza mchezo mkishafika huko. maeneo nayoyaona watawekeza:-
  1. Social Media (Ze - Mutu)
    • wanazotimu zao za social media ambazo zitaanza ku-provoke watu na kupima upepo! yule jamaa sijui ze-mutu anatumika sana katika vita vyao vya social media!
  2. Wajumbe wataopinga hoja au kukatisha tamaa wengine
    • kuna safu ya wabunge watatumika kuyumbisha wenzao, sehemu kubwa ni mtazamo wa kulinda chama, ingawa kiukweli wote mnawatumikia mabwana wawili hawa. kwa jinsi ilivyo, utawala wa kimatabaka na misukumo ya hofu kwa wabunge dhaifu (wasio na uhakika wa kurejea) kunaweza kutengeneza kundi la mbayuwayu wa kutosha kuharibu hoja!
  3. Kumtumia Dada "kiranja" wao!
    • Huyu ndio tegemeo pekee katika jambo hili. hii ni mbinu yao tegemezi kuliko zote, endapo mkuu wa mjengo hatoongoza vikao ijulikane wazi kuwa hoja zote zitakuwa mfu!
  4. Kumkwepesha Bashite
    • Bashite anaweza kukwepeshwa endapo itaonekana kuna dalili mbaya. labda akabadilishwa mkoa, eneo la kazi au akapotea kama last time!
Jinsi ya team Wazalendo kukabiliana na team Bashite
  1. Huyu jamaa wa social media asiwaprovoke watu!
    • Kuna sehemu nyingi unknowingly Mange amekuwa akiuza team, si kila jambo ni la kulimwaga kwenye social media, kuna vitu lazima viendelee kuhifadhiwa kwa ajili ya mapambano ya baadae.
    • MANGE KIMAMBI: Huu ni wakati wako wa kuzungumza skendo tu, usiropoke plan yeyote ya ushindi! maana yake yule ze-mutu atakuwa anakuprovoke na wewe ukisema hata x na y nao hawakubaliani na issue hizi, unawapa side B chance ya kuwa hunt na kuwabadili misimamo kwa mbinu zozote wanazoona zinawafaa!
    • So hadi April taarifa iwe juu ya aibu zao tu na wala sio kina nani wapo team wazalendo
  2. Kuhamasisha wajumbe toka chama dola waunge mkono
    • Wapo wengi bado hawajahamua, lakini pia wapo waoga, so team wazalendo ziundwe, bila ya kusema mbinu watu wajipange na operesheni maalum ya kusambaza ujumbe zianze sasa kuwafikia undecided voters wote!
  3. Huyu dada ni kazi kumdhibiti ila this time watu wawe bold enough kupambana naye. kusimamia maadili ni just course hawezi hata yeye kuwa juu ya sheria, so kamati ya katiba na sheria, msemaji kambi ya upinzani watapaswa kuongoza katika kusimamia hoja hizi za maadili.
  4. Endapo itatokea Bashite kutumbuliwa, kuhamishwa au akijihamisha mwenyewe, watu wasiingie mtego walionaswa watu wa Lumumba, huyu bwana suala lake lijadiliwe tu na hatua zichukuliwe! watu wasibweteke na matokeo yeyote ya Bashite kwa sasa, hadi team wazalendo watakaporidhishwa na usimamizi wa maadili!
Kwanini team wazalendo tunaona umuhimu wa kumjadili Bashite, huyu amevuruga kila kitu! Amenajisi hadi sheria na taratibu ! amewafadhaisha watu wengi waliomuamini mkulu ambaye alikuwa strict kiasi cha kusema hata mama yetu akikosea asekwe ndani, leo yeye anakosea na kutetewa!

jipange kabla hujapangwa!
 
Je Wabunge wa CCM wakipigwa Charm Offensive ya kupangwa kwa Mkutano kati yao na PM au Presidaa kabla ya Mkutano wa bunge "ili kusikiliza matatizo yao" na kupima upepo, Je Wabunge hawa watahandle vipi?
 
Je Wabunge wa CCM wakipigwa Charm Offensive ya kupangwa kwa Mkutano kati yao na PM au Presidaa kabla ya Mkutano wa bunge "ili kusikiliza matatizo yao" na kupima upepo, Je Wabunge hawa watahandle vipi?
wanatakiwa kuwa na msimamo tu, huu sio wakati wa kuyumbishwa kwa ahadi hewa!
 
huyu ndo mwanangu mpendwa, niliependezwa nae. wole wake atakae_____.

in magufuli's voice.
 
Walikuwepo watu wazuri sana like Nyerere, Someone, Kawawa wakapita. Na wengine bado wapo hai wakapita but walitimiza wajibu wao kwa kufuata sheria. Sembuse huyu......
 
Back
Top Bottom