Sababu za afisa wa TISS kumtambulisha mama mzazi wake kwa rais magufuli

Wakuu sina mambo ya kikuda ila ajabu nilitafakari kidogo sababu haswa ni nin Kwani mbona twafahamu ya kuwa idara hyo ni nyeti na pengine hata staff ya idara hyo hawafahamiani kipindi hiki MBNA kumekuwa tofauti ... Nawasilisha
Ulitaka atambulishe mkeoo??
 
Ni
........Nilipenda sana namba moja kwenda kumsalimia mama ake na yule jamaa.

Mengine hata sijui.
Ni mlinzi yupi Kati ya wale tunaowaona je Ni yule wa jw au Yale mabonge mawili meusi au yule mwenye sigida au yule mrefu nanavaa miwani
 
Mkuu kuna kitu nataka nikuweke sawa, Walinzi Wa Rais na Familia yake ni watu ambao wanapaswa sana kuaminiwa kwa kuwa na wao wanakuwa sehemu ya Familia, kwa nchi zilizoendelea kama US Walinzi Wa Familia ya Rais hubaki na Familia hata baada ya Rais kustaafu,kwa hiyo hawa ni sehemu ya Familia. Mfano Walinzi wa JFK waliokuwa wanalinda Familia walibaki nayo hata baada ya JFK kuuawa.

Nayaheshimu Mawazo Ndugu ila sina muda wa ' Kubishana ' nawe lakini nakuomba sana Kitafute Kitabu chenye ' Title ' ya ' CIA and KGB Intelligence and Counter Intelligence Operations ' kilichoandikwa na Watu wawili Mwanadada Celina Bledowska na Mkaka Jonathan Bloch kisha naamini utajifunza mengi na hata Kujiongezea Maarifa kem kem. Na ukikisoma naomba ujikite sana katika Chapters 2,3,6,8 na 9 kisha utakachokipata huko nakuomba usiache pia kuja nacho hapa Jamvini JamiiForums uje ' Uwaelimishe ' na hawa Watu ninaowaonea sana huruma kwa Mwenyezi Mungu kutowabariki ' Vichwani ' mwao akina Mina cute, MACHONDELA na wa kupuliza ili Siku zingine wakiona Watu tunaopenda Kutafuta Maarifa mengi tunajadili hapa mambo muhimu na mazito kama haya basi Wao ' Wachovu ' wawe wanakaa Kimya. Ni Kitabu chenye Kurasa 172 ila Kimeelezea mambo mengi sana mengineyo yakiwepo haya tunayojadili hapa hasa ukizingatia kuwa tokea Miaka ya nyuma huko haya Mashirika Mawili ' Hasimu ' ya Kijasusi yameweza kuwa ni Mifano kwa mengineyo na hata kuna baadhi ya Vyuo vinavyotoa hii ' Tasnia ' vimeiga Utaratibu ' wao wa ' Kiutendaji ' hasa.

Kila la Kheri Ndugu.
 
Ni

Ni mlinzi yupi Kati ya wale tunaowaona je Ni yule wa jw au Yale mabonge mawili meusi au yule mwenye sigida au yule mrefu nanavaa miwani

Yule jamaa ndio nilimuona jana.

.........Huwa simwoni akiwa mbelembele kule.
 
Kwamba katika safari ya mh Rais alifika kijiji fulani huko rukwa,ni kijiji anachotoka mmoja wa walinzi wake,SASA mama wa huyo mlinzi alikuwepo eneo magufuli alpokuwa anazungumza na wananchi,mh rais kwa kutambua hilo akashuka kwenda kusalimiana na mama wa mlinzi wake.( sijajua utaratibu gani ulitumika). Ni hayo tu.
Sasa mlinzi wa rais hawi exposed, eh!?
 
KUwaona kwenye tv si kuwajua, ndio maana wanaishi zao kijitonyama pale na wengine wanakaa ikulu,

Inawezekanaje wasiwepo watu wanaomfahamu kinagaubaga mlinzi wa Rais aliyezaliwa TZ, kukulia TZ na kufanyia kila kitu TZ, ikiwemo kuonekana kila siku kwenye TV akiwa na protectee wake?
 
Walinzi au watumishi wa idara ya usalama wasiofahamika au ambao hawatakiwi kufahamika ni wale informers na wale wa covert operations ila walinzi wa rais wanawezaje wasijulikane wakati unawaona kwenye tv kila siku? Soma hii mada uone jinsi watu wanavyowajua na hadi nyumbani kwao.

Hizi akili zetu nazo....
 
Inawezekanaje wasiwepo watu wanaomfahamu kinagaubaga mlinzi wa Rais aliyezaliwa TZ, kukulia TZ na kufanyia kila kitu TZ, ikiwemo kuonekana kila siku kwenye TV akiwa na protectee wake?
wengi wao huwa ni watoto wa mitaaani, wanapewa mafunzo nk, mambo ya usalama msifikiri ni mepesi kam mnavyoona,
 
Wakuu sina mambo ya kikuda ila ajabu nilitafakari kidogo sababu haswa ni nin Kwani mbona twafahamu ya kuwa idara hyo ni nyeti na pengine hata staff ya idara hyo hawafahamiani kipindi hiki MBNA kumekuwa tofauti ... Nawasilisha
Mkuu, yule jamaa ni mlinzi wa rais na yupo exposed kwenye macho ya watu kila siku. Hivyo kutokana na majukumu aliyonayo sasa hivi, suala la usiri halipo tena. Hata hivyo hao walinzi hutoka kitengo cha PSU (Presidential Service Unit) ambacho si lazima uwe usalama wa taifa. Ukisoma majukumu ya usalama wa taifa utaona kabisa hayahusu kumlinda rais physically. Ni watu tumezoea kuwaita walinzi wa rais kuwa ni usalama wa taifa ila kiuhalisia si hivyo, wale ni kitengo tofauti.
 
Kuhakikisha usalama wa mkuu wa Nchi ndo usalama namba moja...sasa inakuaje hao wanaotekeleza hayo majukumu wasiwe wana usalama wa Taifa...???
 
hizi post za TISS zinachosha sasa. kwani wao siyo watu, hawana ndugu wala jamaa, hawana hisia, rais si mtu mwenye hisia. acha wivu wa kijinga.

rais kusalimiana na mama wa mlinzi wake ambaye hata kwenye tv anaonekana kila siku iwe nongwa? acha wivu wa kijinga.
 
Back
Top Bottom