Mengi Ayoub
Member
- Apr 20, 2022
- 56
- 46
Asilimia kubwa ya wanafunzi nchini Tanzania hufanya vibaya SoMo la HISABATI , Jambo linalofanya wengi kuliita tatizo hili gonjwa la taifa . Kuna sababu mbalimbali zinazofanya wanafunzi wengi kushindwa SoMo la HISABATI . Sababu hizo ni Kama ifuatavyo:
1. Ni dhana potofu iliyojijenga katika vichwa vya watu wengi tangu enzi na enzi , juu ya ugumu wa Somo la hisabati . Watu wengi huamini kuwa Somo la hisabati ni gumu Sana . Jambo hili huwakatisha tamaa wanafunzi wengi na kuwafanya wapunguze jitihada za kulisoma somo Hilo.
2. Ni uvivu wa wanafunzi. Kila somo Lina namna yake ya kulisoma . Namna ya kusoma historia ni tofauti na namna ya fizikia. Somo la hisabati huhitaji kusoma kwa kufanya mazoezi ya Mara kwa Mara . Wanafunzi wengi ni wavivu wa kufanya mazoezi . Hivyo somo la hisabati linalohitaji kusomwa Mara kwa Mara hukosa wapenzi.
3. Uhaba wa walimu wa Somo Hili. Dhana potofu iliyojijenga tangu Zamani imeathiri wengi na kusababisha watu wachache tu wenye moyo wa kukazania SoMo Hilo kuendelea kulisoma katika ngazi za stashahada na shahada .
4. Ni ustadi wa walimu . Licha ya kuwa Somo la hisabati Lina walimu wachache , bado hao wachache wenyewe si stadi . Waalimu wengi hawajawa na uwezo mkubwa katika somo hili. Jambo hili huwaathiri wanafunzi na kuwafanya wafeli somo hili.
5. Kukariri. Wanafunzi wengi wamezoea kusoma kwa kukariri . Somo la hisabati halifai kukariri. Hii hulingana na sababu iliyozungumziwa hapo juu ya namna ya kusoma. Ingawa kukariri hakukubaliki , Kuna masomo ambayo mwanafunzi anaweza akakariri na akafaulu. Hii ni tofauti kwa SoMo la hisabati .
6. Ukali wa waalimu wa hisabti. Hii iko wazi , walimu wa hisabati ni wakali Sana . Kumbuka tu walimu waliowahi kukufundisha wewe ....Jambo hili huwatisha wanafunzi na kuwafanya kuogopa SoMo.
Hizo ni baadhi tu Ila zipo sababu nyingi ..
#Eliupendo mbise
#Leonard mbikilwa