Sababu ya Vifo vya Wachezaji wa Kiafrika Uwanjani

Hans Miki

Member
May 30, 2017
12
28
images.jpg
Baada ya kupata taarifa za kifo cha mchezaji raia wa Ivory Coast, Cheick Ismael Tiote, kuna wazo lilinijia. Nikaamua kufuatilia zaidi ndipo nilipothibitisha kuwa ni kweli kwa takriban miaka 20 iliyopita wacheza soka kutoka Afrika ndiyo wameongoza kwa kufariki wakiwa uwanjani. Hivi ni kitu gani kinaweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa wachezaji wa Afrika?
 
...alimradi tu na wewe umeanzisha uzi,sio?
..endelea kufuatilia utuletee sababu!
 
Wataalam wanasema waafrika wengi wana matatizo ya moyo na huwa hatuna desturi ya kucheki afya zetu.
Hili sio kweli kabisa kwa asilimia 99.9 maana kule wenzetu kabla ya mchezaji kuingia mkataba huwa wanakupima afya yako kwanza endapo ukiwa na tatizo hawakupi mkataba hilo lilitokea kwa Nwanko Kanu aliyekuwa mchezaji wa Taifa la Nigeria pamoja na Klabu za Arsenal,Inter Milan walikuja kubaini ana tatizo la moyo ikabidi asisajiliwe ila wakakubali kumtibu tatizo lake na kuendelea kucheza na tatizo hili sio kwa waafrika tu hata huko Ulaya na Amerika ya kusini ni wachezaji wengi tu wamekufa kwa moyo ukiangalia kuanzia mwaka 2012 kuna wachezaji 35 walikufa kutokana na mshtuko wa moyo waafrika hawazidi 10.Cha mwisho KIFO kipo kwa ajili yetu sisi binadamu kwa hiyo nayo ni sababu sio kwamba ukifanya mazoezi sana basi hautakufa laa maana kuna wangapi wanakufa wakiwa usingizini au wakiwa wamekaa tu.
 
Tunarogana sana watu weusi
Kuna uchawi wa voodoo kutoka afrika magharibi wanakotoka wachezaji wengi wanaofariki kwa ishu za moyo. Huu uchawi mostly huwa unatarget zaidi kwenye moyo. Its the heart attack oriented juju.

Maana mpiga juju anapaswa kutengeneza doll ambalo atalipa jina la anaetaka kumroga then anaacha uwazi pale kwenye moyo na akichoma tu sindano pale kwenye moyo yule mhusika kule anafariki kwa ishu ambayo kidaktari itakuwa diagnosed kama cardiac complication.. Yaani tatizo la moyo ila ukweli inakuwa kapigwa msumari wa moyo spiritually somewhere else then inajidhihirisha physically popote pale alipo.

Tupitie google for kwa taarifa zaidi.
 
Ungekuwekea hizo statistics, ila matukio mengi ya namna hiyo huwa nayasikia nje ya africa. Labda kama ya waafrica huwa hayatangazwi
 
Kudanganya umri kunachangia. Matokeo yake mchezaji anapewa mazoezi, lishe na matibabu ambayo hayaendani na umri halisi.
 
Back
Top Bottom