Sababu ya Umasikini wetu kwa mujibu wa Mh. Benard Membe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu ya Umasikini wetu kwa mujibu wa Mh. Benard Membe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by consigliori, Apr 9, 2010.

 1. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jana nimeona kwenye taatrifa ya habari ya ITV, Balozi wa US nchini alitushauri watanzania kutafakari sababu zinazotufanya kuendelea kuwa masikini pamoja na ukweli kuwa Wahisani wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa Tanzania.

  Kilichonishangaza ni majibu kwa swali hilo yaliyotolewa na Waziri wetu wa mambo ya nje Mheshimiwa B.Membe. Yeye alizitaja sababu kuu kuwa ni Tanzania kujihusisha sana na harakati za ukombozi wa nchi za kiafrika. Akiendelea kufafanua, Mheshimiwa Membe alisema, TZ ilikuwa kituo cha vikundi mbalimbali vya kupigania uhuru na wakati mwinging askari wetu walitumika katika harakati hizi.

  Ninachojiuliza mimi ni je;

  tangu harakati hizi za ukombozi ziishe, ni miaka mingapi imepita sasa? Kwa haraka haraka, haipungui miaka 25! 1985 - 2010) Je bado tusingizie kujitolea kwetu kwa nchi nyingine kuwa sababu ya umasikini wetu mpaka leo?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Huyu Bwana membe wala hata hakutoa majibu ya kuelewa ..ni sahihi hakuwa na majibu kwani anajua wanachokifanya
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Poor Membe!

  Hivi huyu jamaa nyie huwa mnamwelewa?

  Alijitapa sana kwamba lazima "AU" ingemwondoa Rojeilina kule Malagasy na akadiriki kumwita "kijana" lakini so far "kijana" andunda!

  ukifuatilia sana hata uwezo wake wa kuongea ni kama mtoto wa Darasa la sita hivi!
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Membe hajui wanachokifanya - "he is not part of them" . Anachofanya ni kujaribu kukaa mlangoni "kwao" angalau apate yale makombo! Imefikia hatua hata yeye anajiweka kwenye list ya "next president" 2015! Nashangaa kabisa
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  oooh my basi namuhurumia maana katika pumba alizotoa jana ..nilibaki nashangaa mie
   
 6. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Halafu kwa kulalamika kabisa akasema..."watu hawajui tu jinsi Tanzania tulivyopoteza fedha nyingi kuwasaidia wengine kwenye ukombozi"! To me it was like anaona Watz wanalalamika sana bila kuangalia historia. Ikanijia kichwani huku tunakoelekea ni kule kule tulikowasaidia wenzetu kujitoa...Ukoloni si ndio huu? Kwani hii ni nchi yetu? Tupo huru?Nani anatusaidia? Na hata hivyo watu wataachaje kulalamika ikiwa hawaelezwi? nani aliwahi kutoa hayo maelezo ni kiasi gani kilitumika kusaidia nchi za jirani kujikomboa? Na nia halisi ilikuwa ipi? Je tumefanikiwa kufikia hilo lengo? Why Tz? tuna huruma saaaaana! Au?
   
 7. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #7
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK Haelewi kwanini Tanzania bado maskini
  Mheshimiwa njoo JF upate sababu:

  * Asema anajiuliza swali hilo kila siku bila jibu
  * Apinga fikra za siasa za ujamaa kuwa tatizo
  * Aeleza mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo
  *Akiri kuna kipengele katika madini hakimfurahishi  Na Waandishi Wetu (Mwananchi)

  RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.

  Rais Kikwete aliyasema hayo Oktoba 4, mwaka huu mjini Paris Ufaransa katika mahojiano na Mhariri wa masuala ya Afrika wa gazeti la Financial Times, William Wallis na Mwandishi wa gazeti hilo,Tom Burgis.

  "Hata mimi sielewi. Hili ni swali ambalo hata mimi huwa najiuliza kila siku, ni nini ambacho hatujafanya? Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini."

  Alisema hata yeye haelewi ni kipi ambacho bado hakijafanywa ili kuifanya Tanzania kuwa katika nchi zenye maendeleo mazuri katika bara la Afrika.

  "Lakini bado tunaendelea kuvutia uwekezaji katika sekta nyingine. Labda ujumbe bado haujafika vilivyo," alijibu Rais Kikwete alipoulizwa kwanini Tanzania bado ni masikini.

  Alipoulizwa iwapo tatizo pengine bado ni kutawaliwa na mawazo ya kijamaa, Rais Kikwete alisema:

  "Sidhani hilo kama bado ni tatizo. Uwekezaji mara nyingi unatoka sehemu moja kwenda nyingine. Labda wakati wetu utafika katika muda mfupi ujao."

  Alipoulizwa juu ya utata wa vivutio vinavyotolewa katika sekta ya madini katika miaka ya nyuma, Rais Kikwete alisema hajui kama kuna utata wowote katika sekta hiyo.

  Hata hivyo alikiri kuwa kulikuwa na kipengele kilichowaruhusu wawekezaji katika sekta hiyo kuendelea kudai kuwa wanapata hasara hivyo kila wanachozalisha wawekezaji katika sekta hiyo walitumia kipengele hicho kufidia 'hasara' hiyo.

  Alisema kutokana na kipengele hicho wawekezaji walikuwa wakichukua chote walichozalisha bila kulipa kodi kwa madai ya kupata hasara na kwamba wenye mali (wananchi) hawakulindwa, na suala hivi sasa linajadiliwa kwa lengo la kurekebisha.

  Alisema makampuni yote ya madini yamekubaliana na suala hilo kwa kuwa wameona kuna hoja ya msingi katika kumlinda mwenye mali inapotokea hasara.

  Alipoulizwa iwapo anaridhika na malipo ya dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka kama kodi kwa halmashauri migodi ilipo, Rais Kikwete alisema anakubaliana ingawa angependa malipo hayo kuongezwa ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa maeneo husika.

  Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema pamoja na kukua kwa michango ya sekta ya madini na utalii katika uchumi, msisitizo wa serikali ni kuibadilisha sekta ya kilimo ili itoe mchango mkubwa zaidi.

  Alisema katika mkakati huo mabadiliko makubwa yatafanyika katika sekta hiyo kwa kuongeza kilimo cha umwagiliaji, kuongeza matumizi ya mbegu bora na utumiaji zaidi wa mbolea.

  "Matumizi ya kawaida ya mbolea katika kilimo chetu kwa sasa ni ya chini mno ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano, sisi tunatumia kilo nane za mbolea kwa ekari moja ukilinganisha na kilo 577 kwa ekari zinzotumiwa nchini Uholanzi," alisisitiza Rais Kikwete.

   
 8. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #8
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hata Presidaa hajui sababu ya umasikini wa nchi yake, unategemea MAEMBE akujibu nini?...nchi ishauzwa


   
 9. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanasiasa hawaachi sababu wakiulizwa maswali magumu. Watajibu chochote tu
  wakati mwengine hata bila ya kuwa na takwimu kuweza kubeba hoja wanayoulizwa.
   
 10. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,749
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  i watched Membe on TV and i couldnt believe my ears!!! sasa sijui ni vingapi anavyosema hatuvioni wala kuvisikia

  he is our public and international image but and i was really dissapointed with him kwa jinsi alivyokwepa point za muhimu za umsikini wetu na kurushia watu mambo yao
   
 11. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama tuliowapa madaraka hawajui kwa nini nchi inakuwa masikini kunahaja gani ya kuendelea kuwachagua....waache blabla wanainajisi mno nchi yetu....ipo siku watanzania wataamka usingizini na sanduku la kura litawaadhibu.
   
 12. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ikiwa Membe hawezi hata kuyaona haya kuwa ni kati ya sababu zinazotukwamisha maendeleo yetu, basi kazi ipo Watanzania wenzangu

  • Ufisadi ( Yaanani viongizi wa kisiasa ndo matajiri na wafanya biashara wakubwa, sasa sijui kama serikari inakusanya kodi kisawasawa toka kwa wafanyabiashara hawa, Na je inakuwaje viongozi ndo wanakuwa matajiri wakati mishahara na marupurupu yanaeleweka – kuna namna hapa )
  • Uongozi usiojua vipaumbele vya taifa letu na namna ya kuvisimamia ( Mkapa anaposema wakati wa awamu yake kilimo kilisahaulika!Very strange, but this is TZ)
  • Mikataba mibovu ya madini na mali asili nyingine za taifa hili
  • Matumizi ya kifahari ya serikali yetu ( tazama aina ya magari ya serikali, seminar na safari zisizokuwa na tija)
  • Kutojali elimu na kilimo ( kwa mfano, Rais anaposema wanafunzi wapende masomo ya sayansi wakati huo anasifia maelfu ya shule za kata sizizokuwa na waalimu, vitabu wala Maabara, sijui sayansi gain wanatufundisha kwenye hizi shule!)
  Watanzania tutafika tu, ila hofu yangu jua litakuwa limezama.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Jawabu lililotakiwa kutolewa hapao ni refu sana zaidi yahilo, na lingewauma baadhi ya watu, ndo maana aliamua kujibu kisiasa zaidi!...Vita za ukombozi za miaka ya 1975-80 haziwezi kuwa sababu za umasikini waleo....Atalaaniwa huyu mtu, na wazungu wale nadhani walikuwa wanacheka kimoyomoyo!
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyo balozi ameweka challenge nzuri sana..kwa mtu mwenye akili atakuwa ameshaelewa kwamba alikuwa ana-refer kwamba uongozi uliopo ni BOGUS, ndo maana ya hiyo homework, lakini pia ni KIJEMBE. Yaani maana ya swali ni kuwa HUEZI ukaondokana na umaskini kama hujui MBINU SAHIHI ya kwamba utajikwamua vipi. Hilo ndo swali.
   
 15. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi tutaendelea kutoa visingizio mpaka lini? Mwanzoni nchii hii ikiwa changa wanasiasa walisingizia ukoloni. Leo wamekuja na mpya ya kusaidia Ukombozi tena? Swali hili ama kweli limeulizwa wakati mwafaka, mahali pake na kwa makusudi kabisaa!. Hawa wageni wanaouliza maswali haya tunatakiwa Watanzania tuwashukuru sana maana wanasaidia kuwaelimisha wananchi kupitia Magazeti, TV na Redio jinsi ambavyo viongozi hawajihusishi kabisa kama siyo kikamilifu na nchi waliyokabidhiwa dhamana ya kuiongoza.

  Waziri Membe alikuwa anajua kabisa alitakiwa agusie vitu gani vinavyoathiri maendeleo ya nchi lakini akajifanya mjinga kujibu hovyo hovyo tu. Nina hakika kabisa kwamba alikuwa anajua fika kuwa hiyo si kweli akafanya makusudi kupotosha mwelekeo wa mazungumzo yale.

  Sasa cha kujiuliza ni je siasa za kupotoshana na haswa na viongozi wa juu zinamanufaa gani kwa nchi? na wananchi kwa jumla?
  Matokeo yake ni kama tunavyoona wananchi wanachoka, kinachofuata ni migomo ya TUCTA nk. na mengine yako njiani.

  Lakini ukiangalia sana utaona vitu vya kufanana sana katika viongozi wetu. Membe asingeweza kuwa tofauti hata kidogo na viongozi wenzie wa CCM maana ili ufikie ngazi ile ya uongozi inatakiwa uwe umepenyeza kwenye vichujio vya CCM huku ukulishwa mma wa chama chenyewe. Ni chama kinachoongoza kibabe, kwa kupotosha wananchi wake hata pale ambapo haistahili wala kuwepo haja, ni chama kinachoogopa na kuponda utaalam, hakipendi kukosolewa, ni chama kisichopenda hata ushauri wa bure.

  Ingekuwa bora kama badala ya kujibu hovyo hovyo angeji- "commit" kwa kusema atalifanyia kazi na angeomba Balozi na mashirika ya kimataifa yachangie kwani wakati mwingine ni vyema mtu baki akachangia katika mambo muhimu kama haya ili kuyafanyia kazi kwa ushirikiano. Lakini hata hivyo alistahili kukiri mapungufu yaliyo wazi mbele ya Taifa letu.

  Majibu aliyotoa yamemuweka mahali pabaya sana kisiasa, maana anaweza kueleweka kuwa labda wala haoni kuwa nchi ni maskini. Hawaoni watanzania wanavyotatizwa na umaskini. Yaani ni kwamba Watanzania tumekubali tuendelee kubakia maskini hivyo kwa sababu tulisaidia ukombozi wa Afrika miaka takribani 25 iliyopita? Hii ni aibu kubwa sana haswa tukitambua kuwa huyu ni Waziri wa ushirikiano wa kimataifa, anayesafiri na anayeona jinsi nchi nyingine zinavyosonga mbele kimaendeleo. Wanapomkaribisha kwenye majumba ya kifahari waliyoyajenga kwa kuchapa kazi huku akifaidi huduma nyingine zitokanazo yeye huuchapa usingizi tuuuu! Aibu, tena aibu. sana kwa kweli! Hivi angeongezewa swali kuwa "Waziri mligundua lini kuwa uchumi wenu uliathiriwa na kuchangia Ukombozi wa Afrika na mmeweka mikakati gani kurekebisha hayo?" angejibu nini? Nina hakika hawakuuliza swali hilo siyo kwa kuwa walishindwa kuwaza hivyo ila hawakuwa tayari kusikia tena ziada pumba.
   
 16. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Well said Mpenda TZ
   
 17. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mleteni IDI AMIN No. 2 asawazishe mambo.
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2014
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kwanza idea ya Membe kugombea urais alipewa na nani?
   
Loading...