Sababu ya Tanzania kujitoa katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

(African Court on Human and Peoples' Rights) ni Mahakama ya Kibara iliyoanzishwa na nchi za Afrika ili kulindaHaki za Binadamu na za mataifa barani humo.

Uamuzi huo ulichukuliwa naOAU huko Burkina Faso, mnamo Juni 1998 ukapata nguvu ya kisheria tarehe 25 Januari 2004 baada ya nchi 15 kuupitisha kwa saini. Mahakama inaundwa na mahakimu 11, wote raia wa nchi za Umoja wa Afrika. Wale wa kwanza walianza kazi yao mwaka 2006 huko Addis Ababa, Ethiopia lakini mnamo Agusti 2007 mahakama ilihamia Arusha, Tanzania.

MAHAKAMA KUITAKA TANZANIA KUREKEBISHA VIPENGELE VYA KATIBA JUU YA MATOKEO YA URAIS
Mahakama ya haki za binadamu ya Afrika imeitaka serikali ya Tanzania kurekebisha baadhi ya vipengele vya katiba ya taifa hilo vinavyozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani, kufuatia kesi iliofunguliwa na mwanasheria. Baada ya uamuzi wa mahakama hiyo, baadhi ya wachambuzi wa haki za binadamu wanasema kuna mashaka ya utekelezwaji wa agizo hilo kwa kuwa Tanzania ilishatangaza kujitoa katika mahakama hiyo inayoshughulika na haki za binadamu.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 41 kifungu kidogo cha saba kinaeleza kuwa baada ya matokea ya rais yaliyotokana na uchaguzi mkuu kutangazwa na tume ya uchaguzi, matokeo hayo hayawezi kuhojiwa mahakamani. Msimamohuo unakiuka ibara ya pili na ya saba kifungu kidogo cha kwanza cha mahakama ya haki ya Afrika, ambacho kinaeleza kuwa endapo mtu hataridhika na matokeo hayo ya urais, anahaki ya kukata rufaa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na wakili Jebra Kambole wa Tanzania akitaka vifungu hivyo vilivyopo katika katiba vibadilishwe kwani vinakiuka haki za kisheria za binadamu.

Utekelezwaji wa hukumu ya mahakama
Tanzania ni miongoni mwa nchi nne zilizotangaza kujitoa katika mahakama hiyo, nchi zingine ni Rwanda, Benin na Cote d'lvoire iliyotoa maamuzi hayo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.Hata hivyo mahakama hiyo inasema kujiondoa kwa nchi hizo katika mahakama ya Afrika hakuzuii nchi hizo kutekeleza na kulinda haki za binadamu.

Dr. Robert Eno, msajili wa mahakama ya Afrika na haki za binadamu, anasema nchi zote nne zilizojitoa zimeeleza wajibu wa kulinda hakiza binadamun kuendelea kutekeleza mkataba wa haki za binadamu. Kenya na Malawi ni nchi ambazo hivi karibuni zilipinga matokeo ya urais waliyotangazwa katika nchi zao jambo ambalo watetezi wa haki za binadamu wanasema ni ukuaji wa demokrasia na ulinzi wa haki za binadamu.
 
Hatutaki mwanya uwepo kwa wale wanataka kuingilia uhuru wa nchi yetu. Siku tukiona kuna haja kuruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani tutabadili sheria wenyewe bila amri kutoka nje. Katiba yetu ni kazi yetu wenyewe hatuhitaji mamlaka ya nje kutuamrisha.
 
Hatutaki mwanya uwepo kwa wale wanataka kuingilia uhuru wa nchi yetu. Siku tukiona kuna haja kuruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani tutabadili sheria wenyewe bila amri kutoka nje. Katiba yetu ni kazi yetu wenyewe hatuhitaji mamlaka ya nje kutuamrisha.
Na wewe ni mmoja wapo wa wale maprofesa waliookotwa majalalani?
 
Back
Top Bottom