MSHINO
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,067
- 709
Tangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Kwa sasa wamachinga wameachiwa huru kufanya lolote watakalo kiasi kwamba wanafanya bishara zao mpaka milangoni mwa Maduka makubwa, mfano mbele ya duka moja machinga wanakaanga chips, moshi wa mafuta huishia kwenye Maduka.
Sidhani kama wafanyabishara kutoka nchi za nje kama CONGO, ZAMBIA, BURUNDI, ZIMBABWE, BURUNDI NA NK wanapendezwa na hali hii, kwa sababu hata kufunga mizigo mkubwa haiwezekani, kushusha mzigo mkubwa mchana haiwezekani.
Machinga hawalipi kodi za pango la bishara, hawalipi leseni za biashara. Swali, hivi serikali inapoteza pesa kiasi gani kutokana na madhara ya wamachinga?
Tunaomba Serikali ilianglie suala kwa jicho la kipekee ikiwa ni pamoja na kuwawekea wamachinga utaratibu mzuri wa kufanya biashara. Serikali imekuwa inakusanya mapato mengi kutoka Kariakoo lakini kwa sasa hali ni mbaya sana kiasi kwamba biashara nyingi zinafungwa.
Je, wafanyabiashara tunaolipa kodi, tukiacha kulipa leseni ya biashara na kodi ya mapato TRA tutakuwa tumefanya makosa?
Ushauri wangu kwa Serikali: Iwatafutie maeneo ya kufanyia biashara, si kwa Kariakoo tu hata maeneo mengine. Maeneo mengi ya watembea kwa miguu machinga wamechiwa kujenga mpaka vibanda vya kudumu kwa kuezekwa na bati. Mfano ni pale standi ya mabasi ya Makonde njia za watembea kwa miguu zimefungwa kwa kujengwa mabanda.
Kwanini wasielekezwe walau waache njia zilizojengwa kwa gharama kubwa? Kariakoo siyo Dubai ya Bongo tena bali imekuwa ni gulio.