Sababu ya Siasa: Biashara Kariakoo zinakufa kisa kuwapenda na kuwakumbatia machinga

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Tangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Kwa sasa wamachinga wameachiwa huru kufanya lolote watakalo kiasi kwamba wanafanya bishara zao mpaka milangoni mwa Maduka makubwa, mfano mbele ya duka moja machinga wanakaanga chips, moshi wa mafuta huishia kwenye Maduka.

Sidhani kama wafanyabishara kutoka nchi za nje kama CONGO, ZAMBIA, BURUNDI, ZIMBABWE, BURUNDI NA NK wanapendezwa na hali hii, kwa sababu hata kufunga mizigo mkubwa haiwezekani, kushusha mzigo mkubwa mchana haiwezekani.

Machinga hawalipi kodi za pango la bishara, hawalipi leseni za biashara. Swali, hivi serikali inapoteza pesa kiasi gani kutokana na madhara ya wamachinga?

Tunaomba Serikali ilianglie suala kwa jicho la kipekee ikiwa ni pamoja na kuwawekea wamachinga utaratibu mzuri wa kufanya biashara. Serikali imekuwa inakusanya mapato mengi kutoka Kariakoo lakini kwa sasa hali ni mbaya sana kiasi kwamba biashara nyingi zinafungwa.

Je, wafanyabiashara tunaolipa kodi, tukiacha kulipa leseni ya biashara na kodi ya mapato TRA tutakuwa tumefanya makosa?

Ushauri wangu kwa Serikali: Iwatafutie maeneo ya kufanyia biashara, si kwa Kariakoo tu hata maeneo mengine. Maeneo mengi ya watembea kwa miguu machinga wamechiwa kujenga mpaka vibanda vya kudumu kwa kuezekwa na bati. Mfano ni pale standi ya mabasi ya Makonde njia za watembea kwa miguu zimefungwa kwa kujengwa mabanda.

Kwanini wasielekezwe walau waache njia zilizojengwa kwa gharama kubwa? Kariakoo siyo Dubai ya Bongo tena bali imekuwa ni gulio.
 
Mimi mwenyewe ningekuwa na duka kariakoo nisingelipa kodi. Sasa machinga anauza suruali cadet elfu 10 mpaka elfu 12 wakati mwenye duka ili apate faida yakuweza kulipa malindiko ya makodi anatakiwa auze elfu 25 mpaka 30 wateja wenyewe wanaenda kwa machinga kwa sababu ya unafuu wa bei.
 
Mi mwenyewe ningekuwa na duka kariakoo nisingelipa kodi.
Sasa machinga anauza suruali cadet elfu 10 mpaka elfu 12 wakati mwenye duka ili apate faida yakuweza kulipa malindiko ya makodi anatakiwa auze elfu 25 mpaka 30 wateja wenyewe wanaenda kwa machinga kwa sababu ya unafuu wa bei

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Kinasho shangaza sehemu ya watembea kwa miguu wanaweka biashara ina maana tupite barabarani ili tupate ajali
 
Wewe utakua mpinzani. Huitakii mema serekali yako. Machinga wanalipa mbona elfu 20 ya kitambulisho?
Mitano tena
Hakuna nchi inayokusanya kodi bila kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara. kwa sasa kwenda Kariakoo unafikiri mara mbili hakuna hata sehemu ya kupitisha mzigo ikishaununua. Wafanyabishara kutoka nchi jirani km Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi na Comoro wanategemea Kariakoo lkn sasa kumeharibika hakufai.

Sijui viongozi wetu kama wanatembelea maeneo haya. Sina uhakika km Rais au waziri mkuu anajua mazingira ya Kariakoo ya sasa. Lkn kwa kuwa kuna wasaidizi wake kuanzia mkuu wa mkoa, wizara km TAMISEMI na biashara, zifanye kazi yao la sivyo serikali inalea mtoto isiyoweza kumtunza.
 
Mi mwenyewe ningekuwa na duka kariakoo nisingelipa kodi.
Sasa machinga anauza suruali cadet elfu 10 mpaka elfu 12 wakati mwenye duka ili apate faida yakuweza kulipa malindiko ya makodi anatakiwa auze elfu 25 mpaka 30 wateja wenyewe wanaenda kwa machinga kwa sababu ya unafuu wa bei

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Ni tatizo kubwa, machinga hata akipata faida ya elfu moja kwa suruali inamtisha, kwa sababu akikusanya faida ya 10,000/= kwa siku inamtosha. serikali ilisema kila mfanyabiashara awe na mashine za EFD wafanyabiashara wakatii na kununua mashine za EFD, kama ni kodi wanalipa, serikali ifanye kazi yake.
 
Hakuna nchi inayokusanya kodi bila kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara. kwa sasa kwenda Kariakoo unafikiri mara mbili hakuna hata sehemu ya kupitisha mzigo ikishaununua..
Yeah I read you mkuu. Mwenyewe nilikua huko juzi. Keeeroo kerooo. Full vikumbo yaani nakuambia. Hamna kwa kupita.

Watendaji nadhani wanaona sema anasubiriwa mkulu mwenyewe atoe maamuzi. Kitu ambacho sidhani kama kitatokea maana marching guys ni mtaji wa watu walio madarakani
 
Hakuna nchi inayokusanya kodi bila kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara. kwa sasa kwenda Kariakoo unafikiri mara mbili hakuna hata sehemu ya kupitisha mzigo ikishaununua...
Hata TRA wanawasumbua wafanyabiashara wenye maduka mno wakati wanajua wanapata hasara kubwa kwa kuudha bidhaa chini ya bei halisi angalau wapate chochote kwani machinga wameharibu bei
 
Back
Top Bottom