Sababu ya Saudi Arabia kufungua uhusiano na Israel hizi hapa

Saudia katika njia ya kuimarisha uhusiano wake na utawala dhalimu wa Israel

Oct 30, 2021 02:44 UTC

[https://media]

Gazeti la Kizayuni la Globes linalochapishwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mbavu - ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel - limeandika kuwa, kumefikiwa makubaliano mengi baina ya utawala wa Kizayuni na Saudi Arabia kwa mashinikizo ya nchi mbili za Kiarabu za Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).

Mkumbo wa baadhi ya nchi za Kiarabu wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Kizayuni ulianza mwaka 2020 wakati wa urais wa Donald Trump huko Marekani. Nchi nne za Kiarabu za Bahrain, Imarati, Morocco na Sudan ziliingia kwenye mkubo huo mwaka jana na kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel licha ya kulaaniwa na fikra za walio wengi katika ulimwengu mzima wa Kiislamu. Katika miezi ya mwishoni mwa urais wa Donald Trump huko Marekani, kulienea habari kwamba, Saudi Arabia nayo imeingia katika mkumbo na ilikuwa mbioni kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Hata hivyo inaonesha kwamba mfalme wa Saudia, Salman bin Abdulaziz alipinga kutangazwa uhusiano wa kawaida baina ya nchi hiyo na Israel kwa kuhofia Saudi Arabia isipoteze itibari yake kwenye ulimwengu wa Kiislamu. Katika upande mwingine, mazungumzo baina ya Saudia na Jamhuri ya Kisilamu ya Iran yalitia nguvu dhana kwamba, Riyadh haina nia tena ya kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel. Hata hivyo matukio ya takriban wiki moja iliyopita yanaonesha kuwa, Saudi Arabia si tu haijaachana na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, lakini hata imechukua hatua mpya za kufanikisha nia yake hiyo.

[https://media]

Jumatatu wiki hii, ndege ya kwanza kabisa ilianza safari rasmi kutoka mjini Riyadh, Saudi Arabia hadi Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Siku iliyofuata yaani Jumanne, ndege ya kwanza ilifunga safari kutoka ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kuelekea nchini Saudi Arabia. Gazeti la Kizayuni la Globes limeandika kuwa, milango ya soko la Saudi Arabia iko wazi hivi sasa kwa ajili ya bidhaa za Israel na ni wazi kuwa, kuruhusiwa bidhaa za utawala wa Kizayuni kumiminika katika soko la Saudia kuna manufaa makubwa kwa mashirika ya uzalishaji bidhaa ya Wazayuni. Si hayo tu, lakini pia hivi sasa mchakato wa kufunguliwa hekalu la kwanza la Mayahudi katika mji wa Riyadh, Saudi Arabia unaendelea. Eneo hilo litakuwa kituo kikuu cha Mayahudi walioko Saudia na kitatumika kufanyika shughuli zote za kidini za Mayahudi.

Amma swali linalojitokeza ni kwamba, ni jambo gani lililopelekea Saudi Arabia iamue hivi sasa kuendelea kwa kasi na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel?

Kujibu swali hilo, inabidi tuangalie kwanza nafasi ya Marekani katika jambo hilo. Kama ilivyokuwa wakati wa urais wa Donald Trump ambaye aliziamrisha nchi nne za Kiarabu za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, ni vivyo hivyo hivi sasa, Washington ndiyo yenye nafasi kuu katika hatua hizo mpya za Saudia. Mtandao wa Kizayuni wa "Walla" hivi karibuni uliandika kuwa, Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani, tarehe 27 Septemba mwaka huu alionana na Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme za Saudi Arabia mjini Riyadh na walizungumzia suala la Saudia kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni. Feisal bin Farhan, waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia naye alidai hivi karibuni kwamba, (eti) Israel imesaidia kupatikana amani na utulivu katika eneo hili.

[https://media]Mfalme wa Saudia akicheza ngoma na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Sababu nyingine ni mashinikizo ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain katika msimamo huo mpya wa Saudia. Mwaka jana nchi hizo mbili za Kiarabu zilikuwa za kwanza kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel kwa idhini ya Saudi Arabia. Ijapokuwa uhusiano wa siri baina ya Saudia na utawala wa Kizayuni umekuwepo kwa muda mrefu, lakini nchi mbili za Bahrain na Imarati zinaishinikiza Riyadh ifanye haraka kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni kwa tamaa kuwa malalamiko ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi yao yatapungua.

Sababu ya tatu ya uamuzi wa Saudi Arabia wa kuendelea kwa kasi na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel, ni kupenda madaraka Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia. Tangu alipoingia madarakani huko Marekani, Joe Biden hajafanya mazungumzo yoyote na Bin Salman na hakuna hata tetesi za kufanyika mazungumzo kama hayo. Hivyo inaonekana kuwa, Bin Salman ameamua kutia kasi mpango wa Saudia wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala pandikizi wa Israel ili kuyafurahisha makundi ya Kizayuni huko Marekani na kunyanyua itibari yake mbele ya wazayuni walaanifu.

View attachment 1992249
Utawala uliochaguliwa na wananchi wa nchi yao wawezaje kuuita dharim? Ni sawa na.wewe umezaliwa ndani ya ndoa alafu mtu akuite mtoto haramu ? Hizo ni akili? Kama ni swala Israel na palestina, kuna swala la.moroco na shahara je ya Morocco nayo ni dharim? Kuna huko Nigeria na biafla nao ni dharim?
 
saudia pia kuna mashoga pamoja na kuvaa uchungi. dunia nzima inajua waarabu wanaolewa wakiwa na bikra moja tu. israel kuna mashoga kama kulivyo kokote duniani, ni dhambi kama dhambi zingine tu, cha muhimu ni kwamba serikali ya israel hairuhusu hizo ndoa kama walivyofanya waafrica wenzio wa "South Africa, wamarekani na nchi zingine.
Mashoga mbona hata Tanzania wapo? Wale aliokuwa akiwatishia Makonda ni wa wapi. Hili ni janga linalo likabili dunia nzima kwa sasa. Hao waache unafiki.
 
Saudi anamuhitaji Israel kwa sababu zifuatazo.

1. Mabadiliko ya kizazi. Kizazi cha Kina Salman ndio kilikuwa na misimamo mikali dhidi ya Waisrael, hiki cha sasa cha kina MBS hakina time na mambo hayo.

2. Vita yake dhidi ya Iran. Kimkakati, Israel ni rafiki muhimu kwa Saudi ili aweze kumdhibiti Iran (ambaye naye ni adui wa Iran).

3. Mbadala wa Marekani. Kimkakati, kadri uhitaji wa mafuta unavyozidi kupungua kwa Marekani, ndivyo umuhimu wa Saudi kwa Marekani unazidi kupungua, hivyo Israel anaweza kuwa replacement nzuri kama card ya kupata ushawishi kwa Marekani—ambaye kwa Israel, hapindui.

4. Ulinzi. Israel ana teknolojia bora za kiusalama kama Iron dome, ambazo kimsingi kwa vitisho vya Iran, ni teknolojia ambayo anaihitaji.

Screenshot_20211031-124341.jpg
 
sio wanaamini, kuna hadi matofali yapo hadi leo, na hekalu lilibomolewa sio muda mrefu sana, ni wakati wa vita vya crussades ambapo waislam waliitwaa hata Uturuki ambayo ilikuwa ni nchi ya Kikristo (Asia ndogo). Hispania pia ilitwaliwa na kuwa nchi ya kiislam lakini baadaye walipata kipigo ikarudi kwa wakristo. hujui historia, vyote vinavyosema pale Israel ni vya kweli ndani ya Biblia na ndani ya historia ambayo imeandikwa hata kidunia tu.
Hekalu original lilibomolewa na Nebuchadnezzar baada ya mfalme wa jedea sedekia kuwa mtenda dhambi kwa Mungu na Lile sanduky la agano ambalo lina- amri kumi alizopewa Musa halikuonekana Tena mpaka leo,
Baada ya hapo lilijengwa hekalu ambalo ni photocopy na ilipita miaka 1400+ ndo akazaliwa Yesu, na uislamu umekuja baada ya miaka 600+ ya kifo Cha yesu
 
Hekalu original lilibomolewa na Nebuchadnezzar baada ya mfalme wa Israel sedekia kupinduliwa na Nebuchadnezzar, baada ya hapo ilipita miaka 1400+ ndo akazaliwa Yesu, na uislamu umekuja baada ya miaka 600+ ya kifo Cha yesu
kwahiyo unazidi kuprove kwamba eneo lile lilikaliwa na wayahudi zamani kama Biblia inavyosema na kwa maana hiyo ile ilikuwa mali ya wayahudi walipewa urithi na Mungu walipochukuliwa utumwani waarabu wakaingia bila haki wanakaa pale wayahudi wakarudi kuchukua chao, kwanin mnalalalamika sasa? kumbe ushahidi mnao?
 
Hivi waislam wa bongo wanaoishobokea Iran ni washia au???nimegundua 90% ya waislam wa bongo hata hawajui wako dhehebu gani ukiwauliza Uislam una madhehebu Gani utasikia "Uislam wa kawaida Na wa bakwata"
 
ni kitu kisichowezekana kwa dunia nzima kuishambulia israel kwasababu sio dunia nzima ni adui za israel kama ulivyo wewe. pia, Mungu hajalala hata dunia nzima imshambulie. kama umesoma mstari wangu wa mwisho, itafika kipindi mpinga kristo atakapotawala dunia nzima itaishambulia israel, na hapo ndipo Mfalme wa wafalme atakaposhuka kwa nguvu zake kuitetea Israel kwa mikono yake, na hapo ndipo 3/4 ya majeshi yote ya adui wa Israel watakapoteketezwa kwa mvua za mawe radi na kila aina ya silaha za Mungu. wakati huo waisrael watakuwa walianza kudhoofu wakakimbilia milimani hadi pale Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme Mungu mwenyewe atakaposhuka kutoa kipigo kwenu nyie adui za israel.. wakati huo haupo mbali, kwasababu dalili moja wapo ni kuvunjwa kwa ule msikiti wa temple mount ambapo itazusha vita ya dunia nzima, na tayari hilo lipo kwenye schedule ya Israel, walishapanga just a matter of time kuna siku ule msikiti utavunjwa na vita kubwa sana itatokea. tupo nyakati za mwisho kabisa, turudi kwa Mungu (kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ndiye pekee njia kweli na uzima). dini zingine hizo mnapoteza muda na zinawapeleka moja kwa moja jehanamu walikopelekwa waanzilishi wake.
Hao wayahudi wenyewe mnaojikomba kwao hawamtambui huyo yesu wenu tena kwa myahudi anaona anakaribiana na muislam zaidi kiimani kuliko hata mkristo
 
Kivipi nawakati biblia ya wayahudi ndo hii wanatumia wakristo, agano la kale na biblia ya kiyahudi ziko identical 💯
 
Uislam ,ukristo zote ni Abrahamic religions zote zimetoa baadhi ya mambo kwa wayahudi
........manabii waliokua wayahudi unakuta wanatambulika pia kwa waislam na wakristo
Screenshot_20211031-204836_Samsung Internet.jpg
 
Kivipi nawakati biblia ya wayahudi ndo hii wanatumia wakristo, agano la kale na biblia ya kiyahudi ziko identical 💯
Kuna vitu ambavyo wayahudi wanaendelea ku practise ila wakristo wamevitoa .....wayahudi hawali kitimoto kama waislam ila wakristo wanakula
 
Tatizo la wengi hasa waislamu ni kutotaka kusoma na kujua hii inchi ni mali ya nani tangu enzi hizo.
Ni vyema wakasoma ili kujua historia na maandiko ndio pekee yatawatoa ktk kujua ukweli kuliko kulalama.
 
Akili yako inatakiwa ipanuke iende mbali zaidi unavyosema utawala dhalimu unamaana gani udini wako peleka kwenye vijiwe vya wenye msimamo sawa na Abdu rogo au makabuli Jihadi km unachuki na Israel itakutafuna sans
Saudia katika njia ya kuimarisha uhusiano wake na utawala dhalimu wa Israel

Gazeti la Kizayuni la Globes linalochapishwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mbavu - ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel - limeandika kuwa, kumefikiwa makubaliano mengi baina ya utawala wa Kizayuni na Saudi Arabia kwa mashinikizo ya nchi mbili za Kiarabu za Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).

Mkumbo wa baadhi ya nchi za Kiarabu wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Kizayuni ulianza mwaka 2020 wakati wa urais wa Donald Trump huko Marekani. Nchi nne za Kiarabu za Bahrain, Imarati, Morocco na Sudan ziliingia kwenye mkubo huo mwaka jana na kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel licha ya kulaaniwa na fikra za walio wengi katika ulimwengu mzima wa Kiislamu. Katika miezi ya mwishoni mwa urais wa Donald Trump huko Marekani, kulienea habari kwamba, Saudi Arabia nayo imeingia katika mkumbo na ilikuwa mbioni kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Hata hivyo inaonesha kwamba mfalme wa Saudia, Salman bin Abdulaziz alipinga kutangazwa uhusiano wa kawaida baina ya nchi hiyo na Israel kwa kuhofia Saudi Arabia isipoteze itibari yake kwenye ulimwengu wa Kiislamu. Katika upande mwingine, mazungumzo baina ya Saudia na Jamhuri ya Kisilamu ya Iran yalitia nguvu dhana kwamba, Riyadh haina nia tena ya kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel. Hata hivyo matukio ya takriban wiki moja iliyopita yanaonesha kuwa, Saudi Arabia si tu haijaachana na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, lakini hata imechukua hatua mpya za kufanikisha nia yake hiyo.

Jumatatu wiki hii, ndege ya kwanza kabisa ilianza safari rasmi kutoka mjini Riyadh, Saudi Arabia hadi Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Siku iliyofuata yaani Jumanne, ndege ya kwanza ilifunga safari kutoka ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kuelekea nchini Saudi Arabia. Gazeti la Kizayuni la Globes limeandika kuwa, milango ya soko la Saudi Arabia iko wazi hivi sasa kwa ajili ya bidhaa za Israel na ni wazi kuwa, kuruhusiwa bidhaa za utawala wa Kizayuni kumiminika katika soko la Saudia kuna manufaa makubwa kwa mashirika ya uzalishaji bidhaa ya Wazayuni. Si hayo tu, lakini pia hivi sasa mchakato wa kufunguliwa hekalu la kwanza la Mayahudi katika mji wa Riyadh, Saudi Arabia unaendelea. Eneo hilo litakuwa kituo kikuu cha Mayahudi walioko Saudia na kitatumika kufanyika shughuli zote za kidini za Mayahudi.

Amma swali linalojitokeza ni kwamba, ni jambo gani lililopelekea Saudi Arabia iamue hivi sasa kuendelea kwa kasi na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel?

Kujibu swali hilo, inabidi tuangalie kwanza nafasi ya Marekani katika jambo hilo. Kama ilivyokuwa wakati wa urais wa Donald Trump ambaye aliziamrisha nchi nne za Kiarabu za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, ni vivyo hivyo hivi sasa, Washington ndiyo yenye nafasi kuu katika hatua hizo mpya za Saudia. Mtandao wa Kizayuni wa "Walla" hivi karibuni uliandika kuwa, Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani, tarehe 27 Septemba mwaka huu alionana na Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme za Saudi Arabia mjini Riyadh na walizungumzia suala la Saudia kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni. Feisal bin Farhan, waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia naye alidai hivi karibuni kwamba, (eti) Israel imesaidia kupatikana amani na utulivu katika eneo hili.

[https://media]Mfalme wa Saudia akicheza ngoma na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Sababu nyingine ni mashinikizo ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain katika msimamo huo mpya wa Saudia. Mwaka jana nchi hizo mbili za Kiarabu zilikuwa za kwanza kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel kwa idhini ya Saudi Arabia. Ijapokuwa uhusiano wa siri baina ya Saudia na utawala wa Kizayuni umekuwepo kwa muda mrefu, lakini nchi mbili za Bahrain na Imarati zinaishinikiza Riyadh ifanye haraka kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni kwa tamaa kuwa malalamiko ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi yao yatapungua.

Sababu ya tatu ya uamuzi wa Saudi Arabia wa kuendelea kwa kasi na mpango wake wa kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel, ni kupenda madaraka Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia. Tangu alipoingia madarakani huko Marekani, Joe Biden hajafanya mazungumzo yoyote na Bin Salman na hakuna hata tetesi za kufanyika mazungumzo kama hayo. Hivyo inaonekana kuwa, Bin Salman ameamua kutia kasi mpango wa Saudia wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala pandikizi wa Israel ili kuyafurahisha makundi ya Kizayuni huko Marekani na kunyanyua itibari yake mbele ya wazayuni walaanifu.

View attachment 1992249
 
We safi
Wenye nchi yao wamekubali kufungua balozi Israel na kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili.. Sasa sikilizia waarabu wamatumbi wa Kongowe watakavyolaani taifa “tukufu“ la Saudia kuanzisha mahusiano na taifa la “kikafiri” la Israel…
 
Hivi waislam wa bongo wanaoishobokea Iran ni washia au???nimegundua 90% ya waislam wa bongo hata hawajui wako dhehebu gani ukiwauliza Uislam una madhehebu Gani utasikia "Uislam wa kawaida Na wa bakwata"
Asilimia kubwa ya waislamu wa Tanzania hawajui wapo dhehebu gani?
Kuna mmoja aliniambia ati yeye ni bakwata nikacheka sana.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Hivi waislam wa bongo wanaoishobokea Iran ni washia au???nimegundua 90% ya waislam wa bongo hata hawajui wako dhehebu gani ukiwauliza Uislam una madhehebu Gani utasikia "Uislam wa kawaida Na wa bakwata"
Uislamu sio madhehebu sasa sijui una maana gani unaposema hao waislamu hawajui wako dhehebu gani?
 
Tatizo la wengi hasa waislamu ni kutotaka kusoma na kujua hii inchi ni mali ya nani tangu enzi hizo.
Ni vyema wakasoma ili kujua historia na maandiko ndio pekee yatawatoa ktk kujua ukweli kuliko kulalama.
Unazungumza waislamu kiujumla au unazungumza na waislamu wasio soma?
 
Uislamu sio madhehebu sasa sijui una maana gani unaposema hao waislamu hawajui wako dhehebu gani?
A ha hah inachekeshaga kinoma Kuwa Kila dhehebu la Uislam huwa linasema hakuna Uislam mwingine nje ya hapa wengine Ni makafiri...kwahyo Kila dhehebu linasema Uislam Ni mmoja Tu Hakuna madhehebu...ndomaana mnauana nyie
 
Sijui unaongea nini mkuu kwa sababu muislamu anaswali msikiti wowote hakuna msikiti wa dhehebu la fulani wala fulani, sasa kama ingekuwa hivyo unavyosema basi pia kila dhehebu lingekuwa na linaswali kivyake na msikiti wake ndio maana unaona waislamu hawajui madhehebu yao.
 
Back
Top Bottom