John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Takwimu za Dunia za mwaka 2018 za Shirika la Afya Duniani (WHO) zilionesha Wanawake zaidi ya 570,000 waligundulika kuwa na Saratani ya Shingo ya Kizazi,
Kwa mujibu wa tovuti ya cancer.net ni kuwa kwa mwaka 2020 kulikuwa na Wanawake 604,127 ambayo walikuwa wameathiriwa na ugonjwa huo.
Kwa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni utafiti unaonesha maeneo ya Pwani na Kanda ya Ziwa ndipo kulipokuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo.
Elias Kuyamba, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama bila kutaja idadi ya namba amefafanua kwa kusema:
“Maeneo ya Ukanda wa Pwani yamekuwa na matukio mengi ya wasichana wadogo kuanza ngono wakiwa na umri madogo.
“Upande wa Kanda ya Ziwa kulikuwa na ile tamaduni ya mwanaume mmoja kumiliki wanawake wengi au kuwa na uhusiano na wanawake wengi, inapotokea mdudu wa saratani ameingia kwa mmoja ni rahisi kusambaa kwa wengine,” anasema daktari.
Amesema inasadikika Kirusi cha HPV ndicho kinasambaza ugonjwa huo, kinachosambaa wakati wa kujamiiana.
“Mwanamke anapovunja ungo kisha akashiriki ngono na mwanaume mwenye kirusi hicho anaweza kuambukizwa na kukaa na kirusi hicho kwa miaka mingi bila kuumwa.
“Mwanaume hata akiwa na hicho kirusi mara nyingi baada ya muda huwa kinapotea chenyewe, tofauti na mwanamke akiwa nacho, ndio maana kumekuwa na kesi nyingi za Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa wanawake kuanzia umri wa miaka 35 na kuendelea,” anasema Dkt. Kuyamba.
Amesema kuokoa hali hiyo, Serikali ya Tanzania imepitisha watoto ngazi ya shule hasa wale ambao hawajawahi kufanya ngono kupatiwa chanjo ya kuwakinga na Saratani ya Kizazi, kwa kuwa yeyote ambaye ameshashiriki ngono na ameambukizwa virusi hivyo akiwa anaishi navyo, chanjo haitasaidia.
DALILI ZA SARATANI
-Kutoka damu ukeni baada ya kujamiiana
-Kutoka damu wakati ambao siyo wa hedhi
-Kutoka maji yenye harufu mbaya sehemu za siri
-Maumivu wakati wa kujamiiana
-Haja ndogo na kubwa kutoka hovyo
MATIBABU YA SARATANI
-Mgonjwa anaweza kupona akipata huduma mapema
-Matibabu ya mionzi au upasuaji katika hatua ya awali
KUJIKINGA
-Chanjo
-Kuwe na Awareness kwenye jamii
-Kushiriki ngono salama